TRA imeendelea kuvunja Rekodi ya Makusanyo kwa mwezi?

All in all mambo yatakaa sawa ila nchi ipo mikono salama haipo kwenye Genge la wezi tena...Gape la kipato limepungua na linaelekea pazuri..hamjiulizi kwanini watu hawagawi mamilion kwenye Band na kuimbwa kwenye Band... tatizo Watanzania wengi wapo kama Bundi hawajui wanachotaka tulitaka Rais wa kudhibiti wezi sasa kapatikana bado hatuishi kulalamika dawa yetu ni kulazimishwa kunywa maji tu cz hatujui tunachotaka. ..Utawala umebadilika na utaratibu wa ujanja ujanja umefutwa sasa Watanzania wengi hususani waliokua wananufaika na mirija ya wizi hawataki kukubali matokeo. ..nawaambia mtabadilika tu baba akiamua mabadiliko kwa nia njema lazima familia ifate tu ata kama mama au baadhi ya watoto hawataki. ..Baadhi ya Watanzania wamebaki kulalamika hawajui wanachotaka hakuna mabadiliko yasiyo na impact/madhara mazuri au mabaya ya mda mfupi.. Mliomba mabadiliko sasa mnalalamika.. any Organisation change ina impact zake za mpito. ..ukifuatilia kwa undani wote wanaoiombea mabaya serikali wamekatiwa wao au ndugu zao mirija yao ya deal/wizi...watu watapga dili adi lini ebu wahurumien Watanzania Maskini na ipendeni Nchi yenu kama Waisrael walivyo Tayari kwa chochote ili kulinda nchi yao
GO JPM..GOD BLESS YOU JPM ...GOD BLESS TANZANIA
 
Kweli nchi imeyumba sana....kiuchumi makusanyo yamebakia transit ya Rwanda pekeee ambapo TRA hawana chao.....shidaaa!!! Local imports zimedumaaa na kusimama kabisa!! Itachukua miaka 5 kurudi tena tulipofikia awali!! Hali ni mbaya!!!
 
Anajiweka kundi lipi kati ya werevu na wapumbavu!?

Badala ya kuwafukuza haraka (maamuzi ya haraka) au kuwaonya hukohuko kimyakimya, anakuja kulialia mbele ya Umma. Nadhani it is obvious yupo kundi lipi.
 
Mtanzania Mzawa na wenzako ambao mnazungumzia "impact" bila ya kuzungumzia "effect" za hizo impact za mabadiliko ya mfumo mnaongea mambo kiporojo zaidi na si kisayansi. Hizo impact zitaathiri vipi maisha ya kila siku ya mtanzania na itachukua muda gani watanzania kuona manufaa ya hayo mabadiliko mnayoyafanya?

Mabadiliko yanayosababisha watu wakose kazi madhara yake yatarekebishwa lini?

Mabadiliko ya kubomoa nyumba za watu madhara yake yatapona lini?

Mabadiliko yanayosababisha watoto wa maskini kukosa mikopo elimu ya Juu, hasara zake ni zipi?

Mabadiliko yanayosababisha wafanyabiashara washindwe kulipa mikopo waliyokopa, madhara yake kwa taifa mnayajua?

Mabadiliko ya kuzuia fao la kujitoa, wafanyakazi waataathirika vipi?

Mabadiliko ya kuzuia kutoa mawazo kwa uhuru yatasaidia nini kwenye taifa letu?
 
Kumbuka Mawaziri wapumbavu Mkuu. Huyu bila shaka ni mmoja wao.
Pumbavu sana hawa jamaa..
Naombea hivi sasa wasipate kabisa mapato maana hizi hela za walipa kodi hazifanyiwi mambo ya maana..
Wanazitumia kupanga na kufanyia mauwaji raia wema kama Lissu.
 
Siwapendi T.R.A pamoja na mkuu wao ......tabia zao za kukusanya kodi mpaka kwa muuza maandazi inakera sana......mchoma maandazi faida yake haizidi 2000 halafu haya majamaa nayo yanataka kodi msiiiiiiiew mlaaniwe wote mloshauriana upuuzi wa aina hii
 
zile mbwembwe ni madeni ya kodi.

watangaze saiv kama wanaubavu.
Hili tulilisema mapema sana kuwa zille trillions kadhaa zilikuwa ni muunganiko wa arrears tu kutoka makampuni binafsi na kodi kiasi tu.

Kuna welevu walikubaliana na hili mapema, sasa hivi hata hiyo kodi kiasi imepungua na nna uhakika hawafiki na 50% ya kile walichokuwa wanatangaza hapo awali.
 
TRA sahv wanawategemea trafik kwenye ukusanyaji wa mapato nao

OvA
 
Achana na mambo ya makusanyo ya mwezi. Nchi ikinyooka yataongezeka na kuvunja rekodi zote..
 
Taarifa za watu wa ndani zinasema kwa sasa TRA ni propaganda tu hata bilioni 800 hazifiki ........, wanaficha maradhi mwisho wake ndio kwenda Suisse funds kukopa hadi mishahara kwa riba ya ajabu.....umeona wapi???

Hizo trilioni 1.4 unapata wapi wakati kuna walipa kodi wakubwa kama Buzwagi,Bulyanhulu,Geita, Williamson .....na wengine wakubwa mapato yao yameyumba sana .....acha walipa kodi wakubwa ambao mapato yao yanategemea mzunguko kama kampuni za simu,pombe,sigara etc

tusubiri tuone
 
Achana na mambo ya makusanyo ya mwezi. Nchi ikinyooka yataongezeka na kuvunja rekodi zote..
Ilipindishwa na nani na tunajuaje kama anayesema anainyoosha kama haipindishi zaidi?

Ielezwe mikakati ya kufufua uchumi na siyo hadithi za kunyoosha nchi!
 
Back
Top Bottom