TRA ilivyofifisha ndoto zangu, kujiajiri Tanzania ni zigo la misumari

impongo

JF-Expert Member
Feb 18, 2015
8,732
7,611
Mwaka 2008 nilipata ajira ya kibarua Cha muda mfupi (miezi 3) katika moja ya taasisi za kimataifa.

Baada ya kumaliza mkataba wa kibarua changu nilipata pesa kidogo ambayo nilijishauri kujiajiri na kuajiri vijana wenzangu kwasababu ya tatizo la uhaba wa ajira ili kuipunguzia mzigo Serikali ilionao katika sekta ya ajira.

Kipaumbele Cha kwanza ilikuwa ni kufanya uvunaji wa miti nilichukua jukumu la kwenda Katika msitu wa Londo Forest uliopo Lindi vijijini.

Nilifika Londo nikafanikiwa kupata kibali Cha uvunaji na kuanza uvunaji wa magogo ili kuchana mbao.

Kwa bahati mbaya baada ya siku Sitini na Saba msitu ulifungwa kwa sababu uvunaji (magogo) miti wa hovyo hali hii ilitishia uhai wa msitu wa Londo.

Kwa muda wa miezi miwili nilishapata faida ya million kumi na moja (11,000,000) na mtaji wangu ilikuwa ni million sita kwenye akaunti yangu tayari nilikuwa Nina million kumi na Saba (17,000,000).

Nilishawishika kwenda Katika msitu wa Sao hill uliopo mafinga Mkoani Iringa ili kufanya uvunaji wa magogo na kuchana mbao.

Mwezi wa kumi na moja nilifika Sao hill nikiwa na timu ya vijana 20 wafanya kazi wangu.

Nilinunua vibari kwa wavunaji wadogo wasio na uwezo wa kuvuna na nikaanza kazi ya uvunaji.

Nilipanua wigo wa biashara na Kuajiri (mikataba mifupi) vijana wengi Katika sehemu mbalimbali nilizofanya uvunaji Katika maeneo ya msitu wa Saohill.

BAHATI MBAYA
Kwa bahati mbaya mwezi wa 10, 2009 ulizuka Moto Katika msitu wa Mwitikilwa uliochoma mbao 15,400 na mashine (9) na magari yangu ya kubeba magogo (4) na kuchoma magogo mita za ujazo 1350m³.

Wavunaji wengi tulipata hasara na hatukupata fidia nakumbuka Mkurugenzi wa Maliasili Mistu na Nyuki Dr. Felician Kilahama alituambia wavunaji wa Saohill (kupitia chama Cha wavunaji wakati huo SAFIA) Kuwa Serikali imepoteza karibu hekta 40,000 nayo imepata hasara Haina msaada wowote kwa hiyo tusidai fidia yeyote, alikataa kutuongezea hata mgao na hivyo binafsi nilikuwa na madeni mengi sikuwa na chaguo niliuza magari niliyobakisha na kuuza rasilimali nyingine ili kulipa madeni na kuwalipa wafanyakazi stahiki zao ili warudi makwao maana wengi wa Wafanyakazi wangu niliwaagiza kutoka Msitu wa Buhindi Sengerema Mkoani Mwanza.

2010-2011 nilirudi Chuo kumalizia elimu yangu.

2012 Nilifungua kampuni ya Usambazaji vifaa vya Ujenzi, Stationery, Ushauri wa Kitaalamu wa Ujenzi, Usanifu Majengo na Ukandarasi wa barabara na Majengo.

Nilifanikiwa kupata miradi mingi ya barabara na Usambazaji vifaa Katika mikoa ya kusini Lindi na wilaya zake, Mtwara na wilaya zake ikiwemo mkoa wa Pwani na Dsm, Singida,Tabora na Kagera.

Mpaka mwaka 2014 Oktoba nilikuwa nadai 779,650,543.45 madeni kwenye taasisi mbalimbali.
2015 Nilifirisika na kufirisiwa na wadai wanaonidai kwa mara nyingine Wafanyakazi zaidi ya 15 wakapoteza ajira zao.
2016 nili fungua shauri la madai ambayo ni gharama kubwa lakini niliishia kupata vitisho.
2017 niliumwa Sana Pressure na kukaribia kufa nilikata tamaa.
2018 niliamua kurudi barabarani nilipata miradi na kuanza kufanya kwa kusuasua hataye hali ikaanza kuwa nzuri.
2019 TRA walizuia hela Katika akaunti shilingi 35,860,000 kwa kisingizio Cha madeni ambayo hata sifahamu.
2019 TRA walizuia 28,167,790.23 kwa kisingizio Cha madeni
2020 TRA walizuia kiasi Cha 8,987,000
2021 TRA walizuia 10,000,000

Mpaka Sasa wamefunga akaunti zangu kwa kisingizio Cha madeni.

Nchi yetu Kama hauna ndugu kwenye system hauwezi kutoboa ni ngumu Sana.
Nina mengi moyoni Ila Sina budi kushukuru Mwenyezi Mungu huenda ndio mapito yangu.
 
Pole... lkn kwenye mtiririko wa maelezo yako ktk biashara ya mbao sijaona maelezo kuwa ulikuwa ni mlipa kodi... Ila pole kwa uliyopitia.. Ni jinsi gn ww ni mpambanaji
 
Wenye account zilizonona kipindi Cha mniombee walipata tabu kupita maelezo

Yaani kilichokuwa kinafanyika ni kukatakata wanavyotaka baadae unapewa kilichobaki, Kuna mzee mitaa yetu biashara zake tairii juu
Kunyanyuka sidhani

Nachoona upande wako ushajua njia za kupita itapendeza Kama ukipata refa mtakayekuwa mnamegeana kidogo
Hii nchi ukishakubalika kwenye line za Hawa vibopa baaasi ni mwendo wa oda tu
 
Vyovyote vile itakavyokuwa, ila jamaa ni mchakalikaji haswa.

Unataka tuwasikilize upande wa pili TRA?
Unadhani watakosa sababu?
Hakuna mahali nimekataa kuwa si mchakarikaji. Nielewe point yangu.
Na kama sababu ipo je, ni sababu ya kulalamikiwa? Mtu asitafute tu sympathy bila kutoa maelezl kamili.
I smell a rat.
 
Pole sana bro....hata hivyo una jicho la biashara ...usikate tamaa endelea kukaza...wanasema awam hii kidogo kuna uafadhali hivyo endelea kupambania hizo heka zako
Asante
Kupata hela hizo ni ngumu Kama mpaka Sasa wamezuia akaunti mpaka za binafsi.
 
system ya tra kuna sehemu inaitaj masahihisho wanaitaji kukaa muda mwingi na wadau wajue namna watu wanavyooendesha biashara. huwezbukafreez akaunt ambayo mtu ndo ambayo anaendeshea biasharaa hata kama mnamdai lazima mkae chin mdraft namna. ya kulipwa maden yenu asilimia 90 biashara zinaebdeshwa na mikopo kuona pesa kidogo mtu anafrez account hajui upo kwenye situation gan toobad mbaya zaid watu ambao. wapo kwenye izo. taasisi hawajawai kufanya biashara mbaya sana
 
Pole... lkn kwenye mtiririko wa maelezo yako ktk biashara ya mbao sijaona maelezo kuwa ulikuwa ni mlipa kodi... Ila pole kwa uliyopitia.. Ni jinsi gn ww ni mpambanaji
Asante
Kiukweli nilijitahidi kulipa Kodi lakini kipindi Cha kuanzia 2014 Hadi 2018 nilishindwa kwasababu Nina dai madeni mengi Serikali sikulipwa mwisho wa siku 2019 walianza kuzuia akaunti zangu Hadi private.
 
Kuna vitu hujaweka wazi. Kwanini TRA izuie pesa kwa madai una madeni? Madeni ya nini?
Wewe kuna jambo pia unatuficha. Sidhani kama unastahili pole bila kusikia upande wa pili.
Ni maelezo marefu siwezi kuweka milolongo ya kila kitu hapa nimejaribu kuelezea kwa ufupi tu ili wanao maliza vyuo, vijana mtaani wajue hali hivyo Mengine nimemwachia Mungu
 
Back
Top Bottom