TRA iangalie gharama za kupitisha Parcel Posta, zinaua Shirika

Mparee2

JF-Expert Member
Sep 2, 2012
2,584
4,264
Kwa ajili ya kufufua shirika letu la posta

Napendekeza kuwe na mfumo rahisi na unaoeleweka wa ukokotoaji wa gharama za kupitisha parcel ndogo ndogo mf:
Mtu akiagiza simu moja kwa ajili ya matumizi alipie gharama za posta na 18% VAT kusiwe na gharama nyingine

Kwa sasa unaweza kutumiwa/Kununua raba, za dola 20 uambiwe unadaiwa Kodi ya shs 50,000 hadi shs 100,000 hivi, sijui wanatumia formula gani.

Nafikiri huu utaratibu unaendelea kulidumaza shirika la posta na mwisho wake litaishia kuendeshwa kwa ruzuku au lifilisike kabisa
 
Delivery ifanyike na makampuni binafsi. Posta ni mzigo kwa watanzania. Posta ilipofika huwezi kuifufua.

Napendekeza serikali ilifanye liwe public listed corporation, kisha iuze hisa asilimia 60 ibakiwe na 40. Bodi mpya imchague CEO ili liendeshwe kwa misingi ya kibiashara.

Serikali kulea mashirika mengi ni kuwatwisha mzigo usiokuwa na ulazima walipakodi watanzania
 
Posta haina uwezo wa kufanya hivyo; hizo kodi Import Duty n.k. zipo katika Sheria ya Kodi ingawa zinaumiza na mara nyingine ni kubwa kupita kiasi ila mataifa mengi mara nyingine yanatumika hizi kodi ili kulinda bidhaa zake za ndani...
 
Sasa sisi tunabidhaa gani ya ndani ya nchi ?
 
Posta haina uwezo wa kufanya hivyo; hizo kodi Import Duty n.k. zipo katika Sheria ya Kodi ingawa zinaumiza na mara nyingine ni kubwa kupita kiasi ila mataifa mengi mara nyingine yanatumika hizi kodi ili kulinda bidhaa zake za ndani...
Sijui kama ni sawa mtu aagize simu moja au Raba pair moja ( ambazo zote hatuzalishi) alipishwe makodi ambayo hata hayalipiki.
Kupanga ni kuchangua;
1. Tuweke kodi zinazolipika na kufufua shirika la posta lililo ajiri watu kwa mamia wanao lipa kodi na pia Nchi ipate ruzuku kutoka shirika hilo
2. au tuendelee na kodi zisizolipika, wafanyakazi wa posta kwa mamia wakose ajira na pia Nchi ikose Kodi kwa mamilioni.
3. Majengo yetu ya shirika la posta yamekuwa magofu lakini sijaona mikakati ya kulifanya liwe Shirika rafiki wa watumiaji hasa wa Nje ya nchi (Diaspora)

mwisho: Hizo kodi zimewekwa na watu hivyo zitaondolewa/badilishwa na watu
 
Sijui kama ni sawa mtu aagize simu moja au Raba pair moja ( ambazo zote hatuzalishi) alipishwe makodi ambayo hata hayalipiki.
Kupanga ni kuchangua;
Uweke kodi zinazolipika na kufufua shirika la posta lililo ajiri watu kwa mamia wanao lipa kodi na pia kurahisishia wananchi maisha
au uweke kodi zisizolipika, wafanyakazi wa posta kwa mamia wakose ajira na pia Nchi ikose Kodi kwa mamilioni

mwisho: Hizo kodi zimewekwa na watu hivyo zitaondolewa/badilishwa na watu
Ndio maana nikasema kupandisha au kushusha Kodi sio suala la Posta; wala hizo kodi haziendi Posta ni Serikali ndio inakusanya; Hata ukishusha Kodi haitasaidia Posta per Se... sababu watu wanatumia kina DHL n.k. kutokana na Ufanisi wao, Hivyo basi kushusha hizi kodi kutatusaidia wanunuzi sawa ila huenda bado nisitumia Posta nikatumia DHL....
 
Labda posta ni shirika la mtu binafsi kwa maana viongizi wengi ni kama hawaoni posta kunatatizo wamekaa kimya ..
 
Ndio maana nikasema kupandisha au kushusha Kodi sio suala la Posta; wala hizo kodi haziendi Posta ni Serikali ndio inakusanya; Hata ukishusha Kodi haitasaidia Posta per Se... sababu watu wanatumia kina DHL n.k. kutokana na Ufanisi wao, Hivyo basi kushusha hizi kodi kutatusaidia wanunuzi sawa ila huenda bado nisitumia Posta nikatumia DHL....
Posta ina miundo mbinu mingi na iliyotapakaa pote Nchini tofauti na shirika lingine lolote.
Hayo mashirika meengi ya DHL, UPS, FEdex na wengine yameanzishwa baada ya kuona kuna fursa (gap)
Namaanisha kodi zikiwa rafiki ushindani utabaki kwenye utoaji wa huduma na wafanyakazi waaminifu. kwa kuwa Posta ina miundombinu tayari bei zake automatically zitakuwa nzuri/rafiki na hayo ya huduma nzuri wamenza kubadilika hivyo wanahitaji kuwezeshwa
 
Posta ina miundombinu within the Country; DHL; UPS FEDEX ni Kampuni Worldwide... Na hata ndani huduma mbovu za Posta ndio zinapelekea watu kutokuwatumia, mtu yupo radhi ampe bahasha Konda kwenye gari na sio kuwatumia Posta; DHL wanafast delivery unaweza ukapata mzigo 3-5 working days, kumbuka ukituma mzigo through Posta unapitia Postal Company ya nchi ile alafu ndio inatumwa kwa Posta ya nchi yako..., In kina DHL ni Door to Door tofauti na Postal
 
Back
Top Bottom