TRA, Hili ni zaidi ya jipu

Njaro

JF-Expert Member
Mar 19, 2016
356
787
Ni ukweli ulio wazi Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) iliyoanzishwa mwaka 1996 inafanya kazi nzuri ya makusanyo ya kodi na hivyo kuongeza makusanyo ya mapato ya ndani ya nchi. Hivi sasa TRA imefikia uwezo wa makusanyo ya ndani ya takribani Trilioni 1.5 kwa kila mwezi.

Tumekuwa kila siku tukisikia TRA wakitangaza walipa kodi wazuri ambapo mara nyingi vimekuwa vikitangazwa viwanda ama makampuni ndio vinara wa kulipa kodi.

Lakini hatujawa kusikia TRA wakiwataja matajiri maarufu kuwa ndio vinara wa ulipaji kodi. Tanzania imejaaliwa matajiri wengi maarufu na wanaotambulika kimataifa.

Baadhi ya matajiri tulionao ni Said Salim Bakresa, Mohammed Dewji, Rostaam Aziz, Mafuruki na Rostaam Aziz. Pamoja na matajiri wengineo wengi.

TRA wanataka kutuambia hawa matajiri wetu wanakwepa kulipa kodi? Au wanalipa lakini TRA wanazembea kuweka kumbukumbu sawa? Utajiri wao unachangia kiasi gani kwenye kutunisha mapato ya ndani kupitia kodi? Hili ni jipu.

Kuna kundi lingine ni la Wanasiasa na viongozi wa nchi, hawa nao hatupewi taarifa zao juu ya wanavyolipa kodi. Je, TRA wanataka kusema kuwa wanasiasa wetu nao pia wamo kwenye kundi la wakwepa kodi? Hili nalo ni jipu la taarifa za ulipaji kodi kwa wanasiasa na viongozi wetu kutojulikana.

Ifike mahali Watanzania tuige mfano wa nchi zilizoendelea (mfano Marekani) ambapo kigezo cha mtu kugombea nafasi ya kisiasa ama ya kiuongozi ni namna anavyolipa kodi na kama hana rekodi nzuri ya ulipaji kodi anapoteza sifa ya msingi ya kugombea.

Kwao (walioendelea) mtu ambaye halipi kodi anachukuliwa kama muuaji na adhabu yake ni naye kuuawa. Mtu anayekwepa kulipa kodi wanamuona amechangia hospitali kukosa madawa, barabara kutojengwa na huduma nyingine za kijamii kutopatikana ipasavyo, adhabu yake ni kifo tu.

TRA wawe wanatoa taarifa za ulipaji kodi kwa matajiri wetu na anayelipa kodi kubwa wawe wanampa zawadi na si kuishia kutoa zawadi kwa makampuni tu.

TRA wawe wanatupa taarifa za ulipaji kodi kwa wanasiasa na viongozi wetu ili tumjue nani mkombozi kwa Taifa na nani muuaji! TRA tusaidie kutumbua majipu haya.

Hata wale wanaotaka kugombea inabidi TRA watuletee historia ya ulipaji kodi wake nasi tuichukue kama mojawapo ya sifa ya msingi ya kumpa kura zetu.

Tunahitaji tuwe na matajiri na viongozi wazalendo tutakaowasifia kwa ulipaji kodi wao na si kwa Mali na pesa zao ambazo hazitusaidii.

Emmanuel J. Shilatu
0717488622
 
Bongo haiwezekani , nilipo sikia ICD ya Bakhresa ina shida ya kodi... basi nikajua hii nchi matajiri sio wa kuamini kabisa maana nilikuwa namchukuli mzee yule kama roll model wa wazawa wasio na mbwembwe na wanao lipa kodi...
 
Rostam unampenda mbona umemrudia mara mbili nadhani ulitaka kuweka mengi!
 
Wanajamvi tumsaidie mtoa mada kupata uelewa. Bakhresa na Mohamed ni wamiliki wa makampuni. Utajiri wao unapimwa kupitia makampuni yao na siyo wao binafsi.

Wao wanajilipa mshahara ambao hauwaweki wao kuwa walipakodi wakubwa.
 
Ni ukweli ulio wazi Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) iliyoanzishwa mwaka 1996 inafanya kazi nzuri ya makusanyo ya kodi na hivyo kuongeza makusanyo ya mapato ya ndani ya nchi. Hivi sasa TRA imefikia uwezo wa makusanyo ya ndani ya takribani Trilioni 1.5 kwa kila mwezi.

Tumekuwa kila siku tukisikia TRA wakitangaza walipa kodi wazuri ambapo mara nyingi vimekuwa vikitangazwa viwanda ama makampuni ndio vinara wa kulipa kodi.

Lakini hatujawa kusikia TRA wakiwataja matajiri maarufu kuwa ndio vinara wa ulipaji kodi. Tanzania imejaaliwa matajiri wengi maarufu na wanaotambulika kimataifa.

Baadhi ya matajiri tulionao ni Said Salim Bakresa, Mohammed Dewji, Rostaam Aziz, Mafuruki na Rostaam Aziz. Pamoja na matajiri wengineo wengi.

TRA wanataka kutuambia hawa matajiri wetu wanakwepa kulipa kodi? Au wanalipa lakini TRA wanazembea kuweka kumbukumbu sawa? Utajiri wao unachangia kiasi gani kwenye kutunisha mapato ya ndani kupitia kodi? Hili ni jipu.

Kuna kundi lingine ni la Wanasiasa na viongozi wa nchi, hawa nao hatupewi taarifa zao juu ya wanavyolipa kodi. Je, TRA wanataka kusema kuwa wanasiasa wetu nao pia wamo kwenye kundi la wakwepa kodi? Hili nalo ni jipu la taarifa za ulipaji kodi kwa wanasiasa na viongozi wetu kutojulikana.

Ifike mahali Watanzania tuige mfano wa nchi zilizoendelea (mfano Marekani) ambapo kigezo cha mtu kugombea nafasi ya kisiasa ama ya kiuongozi ni namna anavyolipa kodi na kama hana rekodi nzuri ya ulipaji kodi anapoteza sifa ya msingi ya kugombea.

Kwao (walioendelea) mtu ambaye halipi kodi anachukuliwa kama muuaji na adhabu yake ni naye kuuawa. Mtu anayekwepa kulipa kodi wanamuona amechangia hospitali kukosa madawa, barabara kutojengwa na huduma nyingine za kijamii kutopatikana ipasavyo, adhabu yake ni kifo tu.

TRA wawe wanatoa taarifa za ulipaji kodi kwa matajiri wetu na anayelipa kodi kubwa wawe wanampa zawadi na si kuishia kutoa zawadi kwa makampuni tu.

TRA wawe wanatupa taarifa za ulipaji kodi kwa wanasiasa na viongozi wetu ili tumjue nani mkombozi kwa Taifa na nani muuaji! TRA tusaidie kutumbua majipu haya.

Hata wale wanaotaka kugombea inabidi TRA watuletee historia ya ulipaji kodi wake nasi tuichukue kama mojawapo ya sifa ya msingi ya kumpa kura zetu.

Tunahitaji tuwe na matajiri na viongozi wazalendo tutakaowasifia kwa ulipaji kodi wao na si kwa Mali na pesa zao ambazo hazitusaidii.

Emmanuel J. Shilatu
0717488622

Nchi zilizoendelea wanautaratibu mzuri hata kwa wafanyakazi. Kuna kiwango maalum ambachomfanyakazi anapaswa kulipa kodi kwa mwaka kulingana na mshahara wake. Mfanyakazi anapopata mkataba wa kazi kwa mara ya kwanza huenda ofisi ya Kodi kupeleka taarifa zake. Watu wa kodi watampigia calculations ilikujua ni asilimia ngapi ya kodi anapasa kulipa kwa mwezi. Mfano baadhi ya nchi kodi ni 20% ya mshahara, lakini mfanyakazi anaweza kuomba akatwe 25%.
Mfanyakazi atakayekuwa amelipa zaidi ya kiwango anachopaswa kulipa kwa mwaka basi ile ziada atarudishiwa kwenye account yake kama annual tax return.
 
Back
Top Bottom