Informer
JF-Expert Member
- Jul 29, 2006
- 1,582
- 6,627
Sheria hii imeibuliwa na utawala wa Rais Magufuli. Si ajabu kuwa wapinzani wake wataibuka na kuueleza umma wa watanzania kuwa "Madikteta wengi hutumia sheria kandamizi zilizopo kuhalalisha vitendo vyao dhidi ya wananchi wasio na hatia".
Naamini ni watanzania wengi sana wataathirika. Nahisi magari mengi yataondoshwa barabarani kwa lazima. Nahofia kuwa kuna mkakati maalumu nyuma ya hili na tusipoangalia chuki itakayojengwa dhidi ya serikali toka kwa wananchi itakuwa ya ajabu sana.
Waliowahi na wanaomiliki magari/vyombo vya moto wataishi maisha gani?
Ni kwanini sheria ni ya 2001 lakini inaibuliwa makabatini sasa?
Kwanini haijatolewa grace period?
Kwanini hakujawa na namna bora ya kuliweka sawa hili?