TRA fanyeni kazi yenu kwa ufanisi! Watu hawaombi risiti na wenye maduka hawatoi risiti kikamilifu!

Kwa nchi zinazoendelea ikiwemo TZ compliance level ya ulipaji kodi iko chini sana kwa hiyo bila minimum enforcement ni sawa na kucheka na nyani mwisho wa siku ni kuvuna mabua!
 
Juma mosi nilienda kariakoo kununua bidhaa kwenye duka linalomirikiwa na mtu mwenye asili ya kichina mara baada ya kufika muuzaji akamiambia yafatayo
▪︎Kitu unachotaka kununua ni cha laki na hamsini ila bila risiti laki na thelathini elfu
▪︎Na ukitaka bila risiti kabisa ni laki na ishirini elfu
Wakati niko pale akaja mtu anachukua pisi kama 20 za hiyo bidhaa yule dada akaniambia kaka unamuona huyu pamoja na kwamba anachukua pisi ishirini tunamwandikia risiti ya laki tano ya kutembea nayo iwapo akikutana na TRA isiwe usumbufu kwake!.
▪︎ Nilijiuliza sana kwa jinsi yule dada wa kichina anavyokuwa akiprint risiti za uongo mbele yetu watanzania na je ingekuwa mtanzania yuko huko kwao akifanya hivo ingekuwaje?
OMBI
•Naomba sana serkali iendelee kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kulipa kodi ikiwa ni pamoja na kuomba risiti na hii itasaidia vijana wetu kukua na mtazamo huo wa kutoa kodi!
•serkali ijikite katika kuwafatilia wafanya biashara pasipo kuchoka maana ukwepaji wa kodi upo kwa kiasi kikubwa sana saizi maana anapouza bila kutoa risiti anaiibia serkali
•Serkali itambue bila kuwazoesha watanzania hususani wafanya biashara kutoa kodi kwa uaminifu itapoteza mapato mengi sana!
•Serkali itambue kama mwananchi wa kawaida a anakatwa tozo hivo hivo na mfanya biashara kama ilivo kwa mfanya kazi ni lazima alipe kodi ya serkali!
•Serkali itambue pia kwenye suala la kodi hakuna urafiki hapo kuna uwajibikaji kwa kila upande bila kupepesa macho.
•Serkali iachane na kujipendekeza kwa watu ili kuomekana kuwa ni serkali nzuri ndio maana Mwalimu Nyerere alisema serkali fisadi haikusanyi kodi!
•RAIS SAMIA kwenye hili uwe mkali na mwelevu tofauti na hapo mambo yatakuwa mabaya sana hapo baadae yaani watu hawaombi wala kutoa risiti!
HITIMISHO
Watanzania tuweni wazalendo pamoja na serkali kufanya kazi yake kikamirifu ya kukusanya kodi kupitia TRA. Na hii itatuepusha kukimbizana na watu wa hali ya chini kwa kuweka tozo zisizo na msingi

Hili jambo sijui limewashinda TRA au vipi? Kama vipi waajiri watu kukagua Kila anaetoka kwenye badhi ya maduka makubwa.

Ukweli ni kwamba watu hawaombi risiti na wauzaji hawatoi,la sivyo wawe wanafanya ukaguzi wa kushtukiza wakibaini wapige faini hapo hapo maana kuna kulega kutoa risiti tofauti na wakati wa Magu..

Pili polisi washirikoshwe kwenye kukagua bidhaa zote ambazo wateje wananunua kama hakuna risiti faini zihusike mbona watu watadai risiti tuu?..

Angalau TFS wameweza kwenye mkaa kwa nini TRA mnakuwa wazembe? Yaani Nina ushahidi kabisa watu hawadai risiti kabisaa na jamaa usipodai hawakupi.
Wakati mwingine tunapenda toa ushauri ambao ulishafanyiwa kazi na malalamiko yakaanza. Nakumbuka TRA waliwahi fanya operation watu wakalalamika na hata polisi wakikagua risiti watu wanalalamika.Lipi bora sasa
 
Achana na walalamishi ,hii nchi huwa nasema siku zote ina watu walalamishi na mdomo Domo Sana sasa ni kuwapuuza ,TRA na Polisi fanyeni Kazi huna risiti ni faini tuu..

Unapata wapi haki ya kudai uhudumiwe na Serikali wakati hutimizi wajibu?
 
Mimi sipo kubishana kuhusu makusanyo kwa mwezi! Maana hata SIASA inaweza kufanya kazi! Kama wanakusanya kiasi hicho tozo za nini? Mara uchumi umeshuka? Hao ni waongo tunataka wakusanye kodi waachane na tozo zisizo na kichwa wala miguu!
unamaanisha kwa sababu friji linachakula basi huendi tafuta pesa
 
Umevuka lengo na nani ? Toa upumbavu wako hapa,wamekusanya kwa 94%

Pesa inayotakiwa takiwa kukusanywa ni nyingi zaidi ya hiyo.
Unajitia kiherehere kuumizwa na fedha inavyoenda kunufaisha bunge la Ndugai lisilokuwa na faida? Hata wasipokusanya yote wewe kinakuuma mini?
 
Bora ikanufaishe hilo Bunge Kuliko kunufaisha watu wasio na msaada na Mimi..
Duh, kazi kweli kweli! Basi tuko tofauti! Mimi ningeumia kama viongozi wangekuwa na nidhamu ya fedha! Unaona wanajilipa mamilioni wakati watumishi wa umma wananyanyasika? Wanawalipa hata wake uviko-19 pesa za bure wakati siyo wabunge halali! Mimi nitaendelea kuwaachia wafanyabiashara!
 
Kwa nchi za kiafrika kila mtu mwizi tena mpaka viongozi wa juu,, si unaona mpaka uchaguzi uliibwa sembuse hizo risiti
 
Juma mosi nilienda kariakoo kununua bidhaa kwenye duka linalomirikiwa na mtu mwenye asili ya kichina mara baada ya kufika muuzaji akamiambia yafatayo
︎Kitu unachotaka kununua ni cha laki na hamsini ila bila risiti laki na thelathini elfu
︎Na ukitaka bila risiti kabisa ni laki na ishirini elfu
Wakati niko pale akaja mtu anachukua pisi kama 20 za hiyo bidhaa yule dada akaniambia kaka unamuona huyu pamoja na kwamba anachukua pisi ishirini tunamwandikia risiti ya laki tano ya kutembea nayo iwapo akikutana na TRA isiwe usumbufu kwake!.
︎ Nilijiuliza sana kwa jinsi yule dada wa kichina anavyokuwa akiprint risiti za uongo mbele yetu watanzania na je ingekuwa mtanzania yuko huko kwao akifanya hivo ingekuwaje?
OMBI
•Naomba sana serkali iendelee kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kulipa kodi ikiwa ni pamoja na kuomba risiti na hii itasaidia vijana wetu kukua na mtazamo huo wa kutoa kodi!
•serkali ijikite katika kuwafatilia wafanya biashara pasipo kuchoka maana ukwepaji wa kodi upo kwa kiasi kikubwa sana saizi maana anapouza bila kutoa risiti anaiibia serkali
•Serkali itambue bila kuwazoesha watanzania hususani wafanya biashara kutoa kodi kwa uaminifu itapoteza mapato mengi sana!
•Serkali itambue kama mwananchi wa kawaida a anakatwa tozo hivo hivo na mfanya biashara kama ilivo kwa mfanya kazi ni lazima alipe kodi ya serkali!
•Serkali itambue pia kwenye suala la kodi hakuna urafiki hapo kuna uwajibikaji kwa kila upande bila kupepesa macho.
•Serkali iachane na kujipendekeza kwa watu ili kuomekana kuwa ni serkali nzuri ndio maana Mwalimu Nyerere alisema serkali fisadi haikusanyi kodi!
•RAIS SAMIA kwenye hili uwe mkali na mwelevu tofauti na hapo mambo yatakuwa mabaya sana hapo baadae yaani watu hawaombi wala kutoa risiti!
HITIMISHO
Watanzania tuweni wazalendo pamoja na serkali kufanya kazi yake kikamirifu ya kukusanya kodi kupitia TRA. Na hii itatuepusha kukimbizana na watu wa hali ya chini kwa kuweka tozo zisizo na msingi!
Unaongea kama mgeni na hii nchi yani ni kama umekuja jana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna Kijiji kinaitwa Mitezaa,huko kata ya Njia Nne - Wilaya ya Mkuranga.
Ndipo unapotoka udongo mweusi ambao ni malighafi ya kutengenezea tiles ya Goodwill.
No CSR.
Malori yanayolipiwa ushuru ni machache ukilinganisha na hali halisi.
Watu wanapiga pesa balaa ambayo ilitakiwa kuingia Halmashauri.
 
Unadhidi kudhihirisha you are stupid kwenye masuala ya Tax.

Ushajua kwann kuna bei ya risiti, bei bila risiti na bei nusu risiti? Ukishajua utaelewa anayekwepa kodi ni nani na anayemsaidia kukwepa ni nani na kwann.

Mfanyabiashara yeye analipa kodi kabla hata hiyo biashara hajaianza kwa njia ya makadirio. Kasheshe inakuja kwenye VAT ambayo yeye anaikusanya ili ampe TRA na kazi anaifanya bure.

Importation zote huwezi kwepa kuzilipia VAT wakati unaingiza mzigo. Kwa bidhaa za ndani pale kiwandani mizigo inachajiwa VAT.

Tatizo linakuja kwa nyinyi wanyonge wapenda mtelezo linapokuja suala la kulipa hiyo VAT. Hamtaki, mnataka mfanyabiashara ile kwake na mfanyabiashara hawezi kubali ile kwake.

Kama kweli unaipenda nchi yako ungependekeza wafanyabiashara wasikusanye VAT bali ziingizwe kama indirect tax na usingeponda TOZO.
Unamuelewesha tena vizuri tu na kwa uweledi lakini huyo jamaa anakujibu kwa matusi ndiyo ujue ameshavurugwa anajifanya mzalendooo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilijiuliza sana kwa jinsi yule dada wa kichina anavyokuwa akiprint risiti za uongo mbele yetu watanzania na je ingekuwa mtanzania yuko huko kwao akifanya hivo ingekuwaje?
OMBI
Hii mkuu kwao hakunaga ujinga wa ivi. Na ndo Mana kizazi chetu Cha kiafrika tutazidi kuwa watumwa milele mpaka Kiama.
USA ukwepe Kodi ama nchi yyte Kama China unakuwa,unataka wajeda,wauguxi walipwe Nini,walimu je itakuwaje
 
itasaidia vijana wetu kukua na mtazamo huo wa kutoa kodi!
Utasikia Kodi yako Posh Queen akapandishwa ndege akaenda bungeni Kama balozi wa utalii Mara amelala Gold Crest ya mwanza room kigogo anaijua.
Ushenzi mwingine Kodi yetu haitumiki kiusahihi watu wanalia Bata tu.
Yaani Ile selfish saivi iko kiwango Cha juu Sana yaani acha tu
 
Watanzania tuweni wazalendo pamoja na serkali kufanya kazi yake kikamirifu ya kukusanya kodi kupitia TRA.
Unajua Kuna mwaka Brazil ilikuja kucheza na Taifa stars ,tukalipa 3Bn Tzs money ama hulijui ili kumfurahisha baba.
Yeye uzalendo gani alitumia hapo.
Wakati Kuna headteacher huko anaishi kwa nyumba mbavu za mbwa ama ya matope afya yako iko matatani.
Unadhani atakuwa na munkari na kazi yake kweli jamani ya kutengeneza vijana kwa vijana wetu
.
 
Duh, kazi kweli kweli! Basi tuko tofauti! Mimi ningeumia kama viongozi wangekuwa na nidhamu ya fedha! Unaona wanajilipa mamilioni wakati watumishi wa umma wananyanyasika? Wanawalipa hata wake uviko-19 pesa za bure wakati siyo wabunge halali! Mimi nitaendelea kuwaachia wafanyabiashara!
Bora hao ni viongozi wa nchi kuliko jitu tuu ambalo linaitwa Tajiri lenye dharau Kwa wasio nacho ,siwezi kujiachia Hela wewe wakati nikiugua siji kwako hata nikija huwezi nisaidia nitaenda kwenye taasisi za serikali..

Usipolipa kodi ukaachwa Kwa bwanyenye hao unaosema watumishi wataongezewaje salary wakuhudumie wewe? Bwanyenye si ataenda Private hospital na wewe jee.
 
Back
Top Bottom