Tra customs & excise dept!

kachumbari

Senior Member
Nov 1, 2010
125
8
Najua siku hizi mnadai mnafanya kazi kwa mtandao,mtu ana lodge document leo inachukua siku 8 mpaka 10 na hapo unafuatilia ,wakati mwingine inasahaulika kabisaaa!,halafu kibaya zaidi wakati mwingine una mjibu mteja wako kuwa SYSTEM IKO DOWN mimi inanihusu nini? kwani mngekuwa mnasimamisha ngarama za storage nisingekuwa na hoja ila huko nyie hampo na wala hamjali sie wateja tufanyaje?
 
I have collected these from the other thread, a few complaints to mention. TRA mgnt please deal accordingly, it is a shamefull and very serious concern of the country. Every qoute represents a unique victim/mlalamikaji:
"..........for the past 8 weeks tumekua tunashuhudia mambo mengi sana ya ajabuajabu kutoka TRA.. personally kuna incidences tatu nimezipata
  1. ya kwanza mliuplift gari na mkalipwa lakini baada ya all clear lile gari likazuiwa getini at hiyo valuation imekosewa... sasa nauliza makosa yenu yanakuwaje adhabu yangu?? je mwaweza beba makosa yangu?? ni wiki ya tano sasa mnajizungusha tu
  2. jingine ni vitu visivyotozwa kodi, mmeleta utaratibu wa kupitia valuation na sasa tuna mwezi na nusu mnashindwa hata ku-clear makopyuta na kila mnapojaribu kuyatoa mnakosea documents
  3. kwa sasa mmeonesha wazi hamna ccordination ya mipango yenu kwani tumehangaika wiki ya tatu sasa na kila idara inaonekana haijui idara nyenzake infanya nini... hivi kweli haya ndio maanalizi ya kuinua uchumi na kutuondolea kero???
  4. Tumekimbilia mikoani, mmecentralise systems ambazo hata nyie wenyewe hamzielewe...
mnatutesa na kutuumiza watanzania wenzenu sana.... AU NI MBINU YA KUCHANGISHA PESA ZA KAMPENI KWA KUTUMIA STORAGE CHARGES ZETU?? HII SI LAANA?"

"Mimi Binafsi ni Muathirika wa hili!! Gari yangu wali uplift kwa Dola $200
Kuepuka usumbufu nikaona nilipe hiyo kodi tu. ila Roho iliniuma sana!
Naomba kuuliza jamani. Ku uplift ni utaratibu wa TRA? Huu Mchezo umeongezeka sana kuanzia mwezi wa Tisa.
CCM you have an Upper hand on this!!
Jamani wadau kama nina TT receipts! E-mail correspondents!! what else do I need to provide ndio hawa mabwege waamini Value Niliolipia gari?
Mimi ni mtanzania ninaye ipenda Nchi yangu. Kuna uozo mwingi sana hapo TRA. Endeleeni kutunyanyasa Tu. Dawa yenu itaiva October 31.
sasa nimeamua kula na nyinyi sahani moja! hizo gari bora niwaachie lakini sitalipa an Extra Amount for someone who need to be bribed so that I get my right!! achaaani upuuzi jamani. "

"Mimi nina mzigo toka mombasa wiki sasa lori lipo horohoro tunasubiri tra waseme lini tulipie!huku wanasema bajeti ni tegemezi,jee fikiri una chemicals za kiwanda si utachanganyikiwa,muda zinatoka zimesha expire!mengi alikimbiwa na watengenezaji wa colgate,lux kutokana na ukiritimba wa tra!ccm inalaumu tpa badala ya tra.uwekezaji ktk mazingira haya ni hadithi "

"Mimi naogopa kuingia ktk madaraka kwa sababu siwezi kuvumilia uzembe kama huu na walah watu watatengana na wapendwa wao endapo ningekuwa kiongozi.

"TRA ni mkono mwingine wa watawala (CCM) kukusanya pesa za kukiendeshea na kupromoti walarushwa. "

"Hapo mkuu Acid naona unashindwa kuunyosha mkono.
Wao wanakutengenezea mazingira ya kuwahonga sasa wewe hujagundua ukikata kidogo mbona fasta.
Ukikomaa gari itaozea bandarini hapo hao jamaa hawafai. ""Suala hili limejirudia mara nyingi sana bila sababu za msingi sana. Mamlaka ya Mapato Tanzania inapaswa kuwa consistent katika kazi zake. Hoja za mada hii zimejitokeza kwa wengi na kwa gharama za wateja hali kwama:
  • ukadiriaji wa kodi hufanyika bila mteja kuonana na mkadiriaji, inakuwaje aadhibiwe mteja?;
  • nyaraka zinazotumika hazitambuliwi na wale wanaoitwa Wharf, wao wanatumia macho kubuni bei
  • hakuna hatua zinazochukuliwa iwapo kulikuwa kweli na makosa ya ukadiriaji kwa "anayekose"a kila mara halafu wale wa getini ndo wanarekebisha kwa makubaliano maalum (this is more serious);
  • ukimuuliza meneja wa Long Room tatizo lilikuwa ni nini mbona anazuiliwa tena kwa kulipa kidogo, anasema hao ni wengine kabisa wala hawezi kuwaingilia;
Hizi concern ni vema zifike kwa Wakuu wa TRA iwapo hawajui ili Nchi iwe na huduma zenye viwango vinavyotabirika kuliko kila mtu ni Mungu kwenye kakitengo"

"Katika taasisi muhimu na nyeti nchini ni TRA, kama hawa jamaa wataamua kufanya kazi yao kwa umakini wa hali ya juu tutasonga mbele mapema, lakini utasikia mizingo mingine inapita bila kulipiwa ushuru, mingine ndo hivyo wanacompensate kupitia kwa wenye kidogo.
Sina hamu na hawa jamaa, bora ukaingizia gari Mombasa kuliko Dar es salaam maana kutoka bandarini tu kuna watu kijiji kizima inabidi uwahonge. "

"Solution is to change top management as it has never considered that this time is not for ubabaishaji rather, it is time for credible determination. "

"Tatizo wapenda hela (wachagga ) ndiyo wajemaa huko ,wanaharibu hata utaratibu wa kazi . nilishawahi kulipishwa kamzigo kangu kutoka Ughaibuni sina hamu . "

"nchi hii hakuna mkubwa. hakuna wa kumkemea mwenzake "

"Kikwete shughulikia hili kabla halija lipuka "

"WANA JF mimi nina mzigo toka mombasa clearing agent wangu ame lodge document tangu tarehe 3 nov mpaka leo sijajua nilipe ushuru kiasi gani!kisa tiscan mkataba umeisha na asycuda inatumia mtandao wa ttcl ambao wamelazimishwa na govt ni un reliable!ni meenda long room ijumaa j3 j4 na leo sijafanikiwa!kila mara JK analaumu TPA lakini tatizo lipo TRA katika ucheleweshaji wa mizigo. "
 
Sina uhakika kama kuna mtu ambae ameshawahi kuagiza kitu kutoka nje ambacho kitabidi kipitie TRA kwa ajili ya kulipa kodi hajawahi kupata maeso na TRA. Kweli TRA imekua ni kituo cha mateso na usumbufu kwa wananchi...! Tena ukitaka kuteseka zaidi wee fuata utaratibu wa kawaida...! Cha moto utakiona...! KIla kitu ni dili na njia ya panya...!
 
TRA ni kitengo chenye rushwa ya hali ya juu sana Tanzania kutokana na kufanya kazi katika mfumo wa rushwa. Sijawahi kukutana na afisa wa TRA amabye siyo tajiri sana hata kama alianza kazi hiyo mwaka mmja to uliopita. Siwalaumu wao ila ni kwa sababu wanafanya kazi na kuishi katika mfumo unatunza rushwa na idara yao ni kati ya idara zinazofaidika sana ba mfumo huo. Ili kuisafisha TRA ni lazima kuanza na Ikulu kabla ya kuingia Hazina, ndipo utafika TRA na kufanya usafi wa uhakika.
 
Naunga mkono kuwa TRA kuna usumbufu na rushwa za hali ya juu na kila namna. Lakini, it takes two to tango, rushwa ni kwa mtoaji na mpokeaji. Kwa nini wateja wa TRA wote wasisuse? I mean kutoa rushwa, kila mmoja agome kutoa rushwa, tuone kama hawajaanza kutafutana mule TRA.
 
Wenzao Uganda wameonyesha njia kwa kuwapunguzia mzigo wanainchi.....

This is to inform about the abolition of the pre-shipment inspection of all vehicles go to Uganda.

According to the notification from Uganda National Bureau of Standards, the government released the registration rule of importing cars from Japan, and it is notified that all vehicles go to Uganda do not need to take any pre-shipment inspection .
Please note this announcement of the regulation change is temporary applied, and there may be possibility that the regulation will be changed again in the future.

For more information, please check the link below, which shows the letter from Uganda National Bureau of Standards.
Uganda National Bureau of Standards
Thank you.

Carview Corporation
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom