TRA acheni ubabe,maguvu,vitisho ktk vamizi

mwanamichakato

JF-Expert Member
Mar 20, 2015
887
705
Kodi ni muhimu kwa maendeleo ya Taifa letu
Wafanyabiashara ni muhimu katika maendeleo ya Taifa letu.
Mahusiano Mazuri baina ya walipa kodi na wakusanya kodi,wasimamia kodi hayaepukiki.

Kumekuwepo na operesheni zinazofanywa na maafisa kodi {Wafanyakazi wa TRA} kwenye makampuni,Viwanda na taasisi za kibiashara.Operesheni husika imekuwa ikihusisha kubeba vifaa mbalimbali kama komputa na vinginevyo.

Nafahamu Maafisa hawa wanayo mamlaka kwa mujibu wa Sheria kuhitaji,kuchukua ama kubeba chechote kinachoweza kufanikisha upatikanaji wa taarifa zihusuzo masuala ya kodi,Hata hivyo pamoja na mamlaka walionayo kisheria bado wanapaswa kutumia hekima kubwa na busara badala ya maguvu/ubabe/vitisho katika utekelezaji wa majukumu yao kuepuka madhara ya kiuchumi.Wengi wa wafanyabiashara kubwa katika taifa letu ni wageni,Na wengi wa hawa wafanyabiashara na wawekezaji wanajitahidi sana kulipa na kuheshimu sheria za nchi yetu ukiacha wachache wenye biashara uchwara.

Ufanyaji biashara chanya/tija na endelevu {maendeleo} unahitaji sana mahusiano mazuri baina mamlaka za nchi na wafanyabiashara/wawekezaji/wajasiliamali.Lakini pia ubunifu ni siri ya mafanikio ya wengi waliofanikiwa kibiashara,kiuwekezaji..Kutokuaminiana,Kukosekana kwa nia njema,amani na ustaarabu ni msingi kuteteleka kwa maendeleo ya kibiashara.

Tusiruhusu wafanyabiashara wakajinyonga, wakahamisha mitaji,wakafunga biashara,wakafirisika,wakakimbia kwenda kwenye mataifa mengine yakiwemo ya jirani sababu tu ya mazingira ya ufanyaji biashara kutokuwa rafiki/Kuwa magumu ikiwemo ukusanyaji kodi usio rafiki kibiashara.Maafisa wafinyangwe kuwa na lugha za kistaarabu,Elimishi,elekezi..Serikali ni mbia kibiashara wa biashara zote ndani ya nchi.

Taifa letu linahitaji maendeleo endelevu si ya miaka kumi pekee,maendeleo endelevu yanaletwa na ulipaji kodi endelevu toka kwa wafanyabiashara.Wafanyabiashara wanapokuwa kibiashara vivo hivyo ulipaji wa kodi uongezeka maradufu lakini wafanyabiashara na wawekezaji wanapodumaa kibiashara vivo hivyo ukusanyaji mapato husinyaa.
 
TRA kuna shida kubwa sana. Sio Taasisi rafiki yenye kuhamasisha walipa kodi kwa vitendo wafanye kazi hiyo

Sent using Jamii Forums mobile app

Wigo wa makusanyo umepanuka kwa TRA,Mbinu rafiki za kukusanya kodi zitaongeza mapato maradufu.Inawezekana sana,Wawe wabunifu katika kupata taarifa pasipo kutumia nguvu na mabavu ambayo huacha makovu ya uchungu na maumivu kwa wafanyabiashara.
 
Nafahamu Maafisa hawa wanayo mamlaka kwa mujibu wa Sheria kuhitaji,kuchukua ama kubeba chechote kinachoweza kufanikisha upatikanaji wa taarifa zihusuzo masuala ya kodi,Hata hivyo pamoja na mamlaka walionayo kisheria bado wanapaswa kutumia hekima kubwa na busara badala ya maguvu/ubabe/vitisho katika utekelezaji wa majukumu yao kuepuka madhara ya kiuchumi.Wengi wa wafanyabiashara kubwa katika taifa letu ni wageni,Na wengi wa hawa wafanyabiashara na wawekezaji wanajitahidi sana kulipa na kuheshimu sheria za nchi yetu ukiacha wachache wenye biashara uchwara.
 
Wigo wa makusanyo umepanuka kwa TRA,Mbinu rafiki za kukusanya kodi zitaongeza mapato maradufu.Inawezekana sana,Wawe wabunifu katika kupata taarifa pasipo kutumia nguvu na mabavu ambayo huacha makovu ya uchungu na maumivu kwa wafanyabiashara.
Wanafikiria kufunga biashara ndio dawa? Kesho kodi atalipa nani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuanzisha biashara katika nchi maskini si jambo rahisi hasa kutokana na changamoto lukuki zilizopo.
Ufanyaji biashara chanya/tija na endelevu {maendeleo} unahitaji sana mahusiano mazuri baina mamlaka za nchi na wafanyabiashara/wawekezaji/wajasiliamali.Lakini pia ubunifu ni siri ya mafanikio ya wengi waliofanikiwa kibiashara,kiuwekezaji..Kutokuaminiana,Kukosekana kwa nia njema,amani na ustaarabu ni msingi kuteteleka kwa maendeleo ya kibiashara.
 
hakuna tofauti kati ya haramu na isiyo haramu biasgara Tz, Mfanyabiashara Tz ni adui na hatakiwi hata kidogo, kila biashara inchi hii ni sawa na kuuza bangi na cocaine so sad.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio TRA tu.TFDA, TBS, NEMC na OSHA wapo kukwamisha wafanya biashara. Utitiri wa tasisi utadhani kuna cha maana wanachofanya kumbe ni kumkamua tu mfanyabiashara na kumkwamisha.
 
Back
Top Bottom