Uchaguzi 2020 TPSF na Siasa za Uchaguzi: Waandaa mkutano kumpongeza Rais Magufuli kwa mafanikio makubwa ya miaka 5 iliyopita

Makumbele

Member
May 9, 2009
65
390
Huu hapa chini ndo mualiko wao uliosambazwa leo:

MUALIKO WA KUSHIRIKI KATIKA MKUTANO MAALUM WA SEKTA BINAFSI KUMPONGEZA MHESHIMIWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT. JOHN POMBE MAGUFULI KWA MAFANIKIO YALIYOPATIKANA KATIKA MIAKA MITANO YA UONGOZI WAKE (2015-2020)

UKUMBI: JULIUS NYERERE INTERNATIONAL CONVENTION CENTRE (JNICC)
TAREHE: 18 OKTOBA 2020

Tafadhali rejea kichwa cha habari hapo juu.
Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) imeandaa mkutano unaolenga kuwakutanisha wadau wa sekta binafsi nchini kwa lengo la kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Joseph Pombe Magufuli na Serikali ya Awamu ya Tano kwa mafanikio makubwa yaliopatikana ndani ya miaka mitano chini ya uongozi wake.

Mkutano huu umepangwa kufanyika siku ya Jumapili tarehe 18 Oktoba, 2020 katika ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere International Convention Centre (JNICC), uliopo Jijini Dar Es Salaam

Katika mkutano huu, Wanachama na wadau wa sekta binafsi watarejea, watatafakari na kusherehekea Mafanikio ya Kiuchumi ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi mahiri wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt John Pombe Magufuli. Hii itaambatana na kumuelezea Mh. Rais maeneo ya kipaumbele kwa sekta binafsi kwa miaka mitano ijayo na mapendekezo ya nini Serikali ifanye ili kuhakikisha ukuaji na ustawi zaidi wa Sekta Binafsi.

Mkutano huu unatarajiwa kuhuduriwa na wadau wapatao 1,000 kutoka sekta binafsi ambao pia wanatoka katika kongani kumi na nne za TPSF na sekta zote za kiuchumi
Mkutano huu ni moja ya Mikutano mikubwa kabisa iliyowahi kuandaliwa na Sekta Binafsi nchini.

TPSF inaiomba Taasisi yako ambayo ni mdau muhimu wa Sekta Binafsi ihamasishe ushiriki wa wanachama na wadau walioko chini ya taasisi yako ili waweze kushiriki kwa idadi kubwa kadiri iwezekanavyo katika mkutano huu muhimu. Tunaomba ufikishe mwaliko huu kwa wanachama wako na uwaombe wathibitishe ushiriki wao kwa kupiga namba (0676 62 72 61 na 0765 19 64 96).

Pia tunawaalika wanachama wako watakaopendelea kushiriki katika maandalizi ya Mkutano huu muhimu kwa kuwa sehemu ya wadhamini (sponsors).

Tunaamini kuwa, ushirikiano wako mathubuti katika maandalizi ya mkutano huu utazaa matunda na kutuwezesha kwa pamoja kama Sekta Binafsi kuwa na Mkutano wenye mafanikio.

49C4C641-4AE7-4DE2-8771-180402E31BB0.jpeg
 
Nadhan ni wapambe maslahi, kwan yeye jpm turufu moja tu aliyobaki nayo ni mbeleko ya nec, nao wakila kibano cha wananchi mtaona mimacho imemtoka babu jpm
Hivi ninani anaeratibu hizi pongezi ni mpongezwaji au wapongezaji? Au wapambe maslahi?

Nachojua sekta binafsi imeyumba na iko dholfulihal sasa hizi pongezi zinapongeza Nini?

Superbug.
 
Niko hapa ukumbini kufuatilia kwa makini mkutano huu muhimu sana wa kumshukuru Mhe. rais, Dr. John Pombe Joseph Magufuli kwa shukrani za maneno na kauli. Shukrani za vitendo tutampa siku ya tarehe 28 October.

P
 
Hao ni sawa na viongozi wa dini, wasanii,na bakwata.
Kila mtu anajua atampigia kura nani kulingana na alivyoumizwa au alivyonufaika,
Uzuri wanufaika ni wachache.
 
Hivi ninani anaeratibu hizi pongezi ni mpongezwaji au wapongezaji? Au wapambe maslahi?

Nachojua sekta binafsi imeyumba na iko dholfulihal sasa hizi pongezi zinapongeza Nini?

Superbug.
Wapambe hata wwe ukiandaa proposal yeyeto ya kupongeza,au kumuondolea stress jiwe unapata pesa
 
Wameamua kumuondolea stress jiwe usikute wote hao ni wanufaika,
Hii sekta binafsi iliyopigwa Hadi ikachakaa kwa sera za ujamaa ina kipi Cha kupongeza.
 
Unaposomesha watu namba means unauwa sekta binafsi ili watu wasimiliki pesa yaani wawe masikini ili uweze kuwatawala. Hakuna dikteta yeyeto duniani mwenye confidence ya kutawala matajiri na wasomi sababu wanaogopa kukosolewa sababu wengi wao ni low thinking yaani weupe kwenye reasoning.
 
Na sisi MAYANG'A Contractors,
Tunasema kwa MENGI MAZURI yaliyofanywa na awamu hii,

Aisee Huu mkutano ulichelewa Sana kuitishwa
 
Kila mutu anatafuta kijikomba ili mtu akibebwa na mbeleko ya neccm wajekumbukwa huko mbeleni. Dr Akwilapo alitoa PhD kwa mpendwa, leo ni Katibu Mkuu wa Wizara nyeti. Kila mchumia tumbo ana macho na anajaribu bahati yake.
 
Niko hapa ukumbini kufuatia kwa makini mkutano huu.
P
Kinachoshangaza sekta binafsi ndio sekta iliyo athirika kwa kiwango kikubwa sana na utawala uliokuika kiapo utawala wa JPM

Sekta binafsi ndio muathirika namba moja kwa unyanyaswaji na ukiukwaji mkubwa wa katiba ya nchi

Kinachonishangaza imekuwaje eti wao ndio wa kwanza kupongeza kwa nguvu ipi, kwa maslahi yapi, kwa mafanikio gani biashara zimefungwa watu wamefilisika

#NI YEYE + PONDA ... TUMEWAMALIZA 2020

Mtabaki NA AL-HADI wenu waislamu tumeikataa BAKWATA na GENGE LAO la kuchumia tumbo jaribuni hukohuko kwenye sekta binafsi labda ila kwa muda huu kuugeuza upepo ni kama mmechelewa ngoma imeshawaelemea

Hongera sana kamati ya Kampeni CDM kwa hili mmefanikiwa kugeuza Tanga pepo za kusi zinawapiga dhoruba wenzetu wameshapotezwa mawimbi ni makali mno ...
 
Back
Top Bottom