TPSF: Miaka mitatu ya Magufuli yaleta mafanikio katika biashara ya sekta binafsi nchini

kindimba

Member
Apr 2, 2012
22
34
Mkurugenzi wa sera na utafiti wa taasisi ya sekta binafsi nchini (TPSF) Mr. Geliadi Teri amepongeza miaka mitatu ya Serikali ya awamu ya tano kwa kuweka mazingira mazuri kwa wafanyabiashara wa sekta binafsi nchini.

Akizungumza katika kipindi cha Mizani ya Wiki kinachorushawa na AZAM TV Bwana Teri amegusia maeneo manne amabayo ndani ya miaka mitatu ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dr. John Magufuli yamefanikiwa ni kukua kwa soko la Afrika mashariki , kuongezeka kwa uhuru wa biashara ya mazao (na utoshelevu wa chakula) , kupungua kwa kiwango cha umasikini (absolute poverty) pamoja na ujenzi wa viwanda ambavyo vimetoa ajira kwa maelfu ya watanzania.

Zamani nilikuwa sielewi kinachoendelea Congo Burundi Africa kati kwanza nilikuwa nawaona raia wake wajinga wanaruhusu vp yale yote yanayoendelea kwenye nchi zao lkn ss majibu yote ninayo ubinafsi kitu kibaya sna mungu anisamehe lkn Waukae mwenzangu Mzee Wngu Jakaya Mrisho Khalifani Kikwete kwa ili lazima ifikie kipindi utuombe Radhi watanganyika wenzako. kweli Tanzania leo tumekuwa km Shamba la watu fulani tu au nyumba ya mtu anafanya atakalo hii nchi yetu sote lazima tusikilizane sio kuwasikiliza wao tu...
 
Subiri waje mawaziri kivuli wasio na serikali wala ofisi uone watakavyomwaga povu hapa!
 
Uhuru wa biashara ya mazao umekua wapi? 2015 sisi wakulima tuliuza gunia moja la mahindi na kufanikiwa kununua mfuko mmoja wa mbolea ya kupandia DAP wa sh. 65,000, hivi sasa tunalazimika kuuza magunia 3 kwa ajili ya mfuko wa DAP mmoja. Mwakani wasishangae mavuno ya mahindi yakawa kiduchu.
 
Acheni kuwa vibaraka wa kubeza kila kitu mtalaaniwa hii Nchi inasonga mbele kwa hatua kubwa,mtabaki kulaumu mwisho wa safari mtakuwa mmehathilika kisaikolojia.
 
Hii inaitwa awamu ya kusifia.
Ndipo tulipofikia hapo kila kitu ni kusifia tu.
Ngoja azidi kutunyoosha labda akili yaweza kurudi ni tukawa wakweli.
 
Huyo aliye kuwa anazungumza hivyo pamoja na aliye mtuma wote hawana akili zote.
 
Mkurugenzi wa sera na utafiti wa taasisi ya sekta binafsi nchini (TPSF) Mr. Geliadi Teri amepongeza miaka mitatu ya Serikali ya awamu ya tano kwa kuweka mazingira mazuri kwa wafanyabiashara wa sekta binafsi nchini.
Akizungumza katika kipindi cha Mizani ya Wiki kinachorushawa na AZAM TV Bwana Teri amegusia maeneo manne amabayo ndani ya miaka mitatu ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dr. John Magufuli yamefanikiwa ni kukua kwa soko la Afrika mashariki , kuongezeka kwa uhuru wa biashara ya mazao (na utoshelevu wa chakula) , kupungua kwa kiwango cha umasikini (absolute poverty) pamoja na ujenzi wa viwanda ambavyo vimetoa ajira kwa maelfu ya watanzania.

Kila mtu atatumwa kumsifu magufuri kwa sifa asizostahili wakati anajua ukweli anatupeleka shimoni. Tunazikwa huku tukiimbiwa nyimbo tamu
 
Back
Top Bottom