TPSF, Ewura, NEEC kujadili ajira za wazawa Stiegler’s Gorge

esther mashiker

JF-Expert Member
May 29, 2018
616
552
TAASISI ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la Uwekezaji la wananchi Kiuchumi (NEEC) pamoja na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura),-

zimepanga kukutana na makandarasi wanaotekeleza mradi wa kufua umeme mto Rufiji ili waweze kutoa fursa za ajira kwa wazawa. , aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati taasisi hiyo pamoja na NEEC zikiainisha fursa zitokanazo na uanzishwaji, utekelezaji na ukamilishwaji wa mradi huo unaogharimu dola za kimarekani bilioni 2.9.

Simbeye alisema wameandaa mkutano wa wadau utakaofanyika Juni 11, jijini Dar es Salaam, lengo likiwa ni kuongeza ufahamu kwenye mradi na fursa zilizopo.

“Mkutano huu utahudhuriwa na makandarasi kutoka Misri wanaoutekeleza mradi huo pamoja na timu ya usimamizi kutoka Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) wanaousimamia ambao watatoa mawasilisho kwa wadau siku hiyo,” alisema.

Alisema matarajio ni pamoja na kuwasikiliza makandarasi hao wa Misri kuhusu mpango wao wa kushirikisha wazawa katika utekelezaji wa mradi huo na kuwapanga Watanzania waweze kushiri kikamilifu. Pia alisema matarajio mengine ni kuwafahamisha Watanzania kuhusu fursa zinazotokana na mradi haswa aina ya vifaa na bidhaa zitakazohitajika kutoka Tanzania.

“Kuwataarifu wafanyabiashara ambao wana hamu ya kushiriki katika minyororo ya thamani mbalimbali na kuwapatia ujuzi pamoja na nyenzo zitakazowawezesha kushiriki kikamilifu kwenye mradi,” alisema. Simbeye alisema majarajio mengine ya mkutano huo ni kuwasikiliza wahusika wa mradi kuhusu utaratibu ambao wazawa wanaweza kushiriki katika zabuni mbalimbali. Pia alisema jambo lingine ni kufahamu aina ya kampuni na sekta mbalimbali ikiwamo ya watoa huduma watakaohitajika katika kutekeleza mradi huo wa mabilioni.

 
Mbona kwenye mkataba hawajashirikisha hata wawakilishi wa wananchi?!

Hata kwenye mradi wa gesi hizi mbwembwe zilikuwepo ila leo kimya!!

Hata kwenye mradi wa Bagamoyo na kwenye sifa zilikuwa lukuki ila leo imekuwa kinyume chake!!

Wale poyoyo wa Lumumba huu uzi hapa chinin sijui huwa wanaulewa?!


Alafu ndio hawa hawa wanahoji mbona hatujapelekwa MIGA wakati walikuwa wanadai kodi za matrilioni na sasa wameahidiwa kupewa kifuta machozi na hii ndio maana halisi ya lile neno rubbish waliloambiwa na kamanda.

Ndio maana niliwahi sema:

 
Back
Top Bottom