TPN, Jamiiforums na Michuzi Blog Yakabidhi Tena Misaada Ya Wahanga Wa Mafuriko | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TPN, Jamiiforums na Michuzi Blog Yakabidhi Tena Misaada Ya Wahanga Wa Mafuriko

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sanctus Mtsimbe, Mar 12, 2010.

 1. Sanctus Mtsimbe

  Sanctus Mtsimbe Tanzanite Member

  #1
  Mar 12, 2010
  Joined: Jul 14, 2008
  Messages: 1,812
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
  Gari ambayo ilileta misaada ya namna mbalimbali ofisi za Red Cross


  [​IMG]
  Katibu Mkuu wa TPN Mzalendo Method Bakuza, akikabidhi misaada ambayo imekusanywa na TPN na Wadau wake (Jamiiforums.com na Michuzi.blogspot.com) kwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Msalaba Mwekundu Bw. Peter Mlebusi  [​IMG]
  Mzalendo Sanctus Mtsimbe ambaye ni Rais wa TPN na Meneja Mauzo na Masoko wa SimbaNET (T) Limited akisikiliza maelezo kutoka kwa naibu katibu Mkuu wa Red Cross Bw. Peter Mlebusi

  [​IMG]
  Katika Misaada hiyo SimbaNET Limited ilichangia kiasi cha TZS 1,500,000 ambazo zilitumika kununua misaada hiyo. Misaada hiyo kwa upande wa SimbaNET ilikabidhiwa na Sanctus Mtsimbe, Meneja Mauzo na Masoko wa SimbaNET.


  [​IMG]
  Rais wa TPN Mzalendo Sanctus Mtsimbe, akimsomea orodha ya Misaada itakayokabidhiwa ambayo imekusanywa na TPN na Wadau wake (Jamiiforums.com na Michuzi.blogspot.com) Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Msalaba Mwekundu Bw. Peter Mlebusi  Katibu Mkuu wa TPN Mzalendo Method Bakuza, leo alikabidhi misaada ambayo imekusanywa na TPN na Wadau wake (Jamiiforums.com na Michuzi.blogspot.com) kwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Msalaba Mwekundu Bw. Peter Mlebusi. Misaada iliyotolewa ni pamoja na: Ndoo 40, Magodoro 40, Sabuni Cartoon 5, Vyandarua 40, Mablanketi 200 vyote vikiwa na thamani ya TZS 1,619,000 Pia kulikuwa na misaada ya vitu mbalimbali kama nguo nyingi sana, viatu, vyombo vya nyumbani vyote vikiwa mizigo kama 10 vikiwa na thamani ya TZS 4,600,000 ambavyo vilichangiwa na wadau mbalimbali.

  Katika Misaada hiyo SimbaNET Limited ilichangia kiasi cha TZS 1,500,000 ambazo zilitumika kununua misaada hiyo. Misaada hiyo kwa upande wa SimbaNET ilikabidhiwa na Sanctus Mtsimbe, Meneja Mauzo na Masoko wa SimbaNET. Kampuni ya simu za Mkononi ya Tigo ilichangia kiasi cha mablanketi 200 yenye thamani ya TZS 1,600,000.

  Kampeni ya Kuhamasisha uchangiaji imeshamalizika huku TPN na Wadau wake wakiwa wamechangia misaada yenye thamani ya karibia TZS 20 Million. Jumla ya watu 2000 Walichangia kwa SMS na kiasi cha Shilingi TZS 2,037,332 zimekusanywa.

  Misaada yote ambayo imekabidhiwa ni kwa ajili ya wahanga wa mafuriko katika maeneo mbalimbali yaliyoathirika na mvua kubwa.

  TPN inazindua Mfuko wake wa Uwezeshaji katika Mkutano Mkuu wa Mwaka utakaofanyika siku ya Jumapili Tarehe 14-03-2010 katika ukumbi wa Blue Pearl Hotel Ubungo Plaza.
   

  Attached Files:

 2. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #2
  Mar 12, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Mtsimbe, hongera sana kwa kazi nzuri mnayoifanya.
   
 3. Sanctus Mtsimbe

  Sanctus Mtsimbe Tanzanite Member

  #3
  Mar 12, 2010
  Joined: Jul 14, 2008
  Messages: 1,812
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160

  Mzalendo Mwafrika asante sana,

  Bila ya shaka hizi ni juhudi zetu wote kwa pamoja.

  Walau JF, TPN and Michuzi tumeweza kutoa changamoto kuwa we can. TZS 20 Million si kazi ndogo, Wale wengine na ukubwa wao waliweza TZS 50 Million tu!!!
   
 4. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #4
  Mar 12, 2010
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Hii kampeni inaweza kwenda Magu?
   
 5. Sanctus Mtsimbe

  Sanctus Mtsimbe Tanzanite Member

  #5
  Mar 12, 2010
  Joined: Jul 14, 2008
  Messages: 1,812
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Hakuna kisichowezekana Mkuu.

  Tunapokabidhi Misaada Red Cross, huwa hatuwapangii waipeleke wapi. Tunawaachia wao waangalie priority areas ni zipi.
   
 6. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #6
  Mar 12, 2010
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Nimeona TPN wamerusha ujiko kwa TPN tu, tell mi waliambiwa lakini wao hawakurushwa kuwa michango hiyo ni kwa ushirikiano wa JF na Michuzi.
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  Mar 13, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Hongera Sanctus.. kwa kuonesha uongozi katika hili..
   
 8. Sanctus Mtsimbe

  Sanctus Mtsimbe Tanzanite Member

  #8
  Mar 13, 2010
  Joined: Jul 14, 2008
  Messages: 1,812
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Mzalendo na wewe pia Maxe; Michuzi na Wadau wote hongera sana kwa team work.

  Ninao uhakika wote tumetoa changamoto na kuonyesha njia kwa vitendo!

  Asante wote mliotoa support kwa hali na mali.

  Shukrani kwa wote pia waliotoa kejeli na kutokuwa na imani na kampeni hii kwani wametumia uhuru wao.

  Asanteni pia tuliowashirikisha katika mawazo na mkakati wetu wa kuchangia lakini wakageuka, "kutupiga bao" na kutumia mbinu yetu. Imesaidia pia kupata michango ya kuwasaidia waathirika, maana hilo ndilo lilikuwa lengo letu. Huenda bila sisi wasingetoa misaada wala kufanya kampeni.

  Asante sana Wana JF.

  Nawaalika pia TPN ili kuendeleza mapambano!
   
 9. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #9
  Mar 13, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hongera sana mzalendo Sanctus sasa nafikiri tuwakumbuke hata ndugu zetu wa Mwanza nako kuna mafuriko.
   
 10. Sanctus Mtsimbe

  Sanctus Mtsimbe Tanzanite Member

  #10
  Mar 13, 2010
  Joined: Jul 14, 2008
  Messages: 1,812
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Asante sana Mkuu.

  Tuko pamoja. Tunajaribu kuangalia Strategy ambayo itatupa misaada ya kutosha. Bado iko katika mchakato kuona kama itafaa.
   
 11. O

  Ogah JF-Expert Member

  #11
  Mar 13, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Well done my brother
   
 12. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #12
  Mar 13, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  As a matter of fact.. the whole campaign ya kusaidia Red Cross has raised over 100Million Tanzanian Shillings.. !
   
 13. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #13
  Mar 13, 2010
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  ......Hongera Mtsimbe kuwa mzalendo wa kweli,kusimamia hii kazi sio kazi ndogo.
  God bless you all abundantly.
   
 14. Sanctus Mtsimbe

  Sanctus Mtsimbe Tanzanite Member

  #14
  Mar 13, 2010
  Joined: Jul 14, 2008
  Messages: 1,812
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Tuko pamoja Mzalendo!
   
 15. Sanctus Mtsimbe

  Sanctus Mtsimbe Tanzanite Member

  #15
  Mar 13, 2010
  Joined: Jul 14, 2008
  Messages: 1,812
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Inabidi tufanye Post-Mortam Mkuu!
   
 16. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #16
  Mar 13, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Mzalendo Mtsimbe,

  Shukurani sana kwa kuonyesha ujasiri katika uongozi kwa vitendo na kuwasaidia ndugu zetu. Mungu akubariki.
   
 17. Sanctus Mtsimbe

  Sanctus Mtsimbe Tanzanite Member

  #17
  Mar 13, 2010
  Joined: Jul 14, 2008
  Messages: 1,812
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Asante sana Pretty.

  Nashukuru sana na wewe na wengine kwa michango ya hali na mali mliyoitoa.
   
 18. Sanctus Mtsimbe

  Sanctus Mtsimbe Tanzanite Member

  #18
  Mar 13, 2010
  Joined: Jul 14, 2008
  Messages: 1,812
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Mkuu; nashukuru sana na wewe. nakumbuka sana michango yako uliyotoa. Ubarikiwe sana Mkuu!
   
Loading...