TPDC wazindua mradi wa Kutumia Gas kwenye Magari na Majumbani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TPDC wazindua mradi wa Kutumia Gas kwenye Magari na Majumbani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mpendanchi-2, Jul 15, 2009.

 1. Mpendanchi-2

  Mpendanchi-2 JF-Expert Member

  #1
  Jul 15, 2009
  Joined: Apr 4, 2009
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  WAZIRI wa Nishati na Madini, William Ngeleja, amesema kuwa kuanzia Septemba mwaka huu, kwa mara ya kwanza magari na taasisi za serikali zitaanza kutumia gesi asilia.

  Aliweka hilo wazi jana Dar es Salaam wakati alipokuwa akizindua mradi wa kuzalisha gesi iliyosindikwa wenye thamani ya sh bilioni tatu wa kuzalisha gesi iliyoshindiliwa (compressed gas), wa Kampuni ya Pan African Energy (T) Ltd katika eneo la Ubungo.

  Ngeleja alisema mara baada ya kumpata mtaalamu mwelekezi na kukamilisha kazi ya kutoa upembuzi yakinifu Julai 2007, jumla ya vituo 12 vitajengwa huku nyumba 38,000 zikiunganishwa na jumla ya magari 8,200 yanatarajiwa kurekebishwa mifumo yake ya nishati, ili yaweze kutumia gesi asilia.

  Alisema kuwa mradi huo ni wa awamu mbili - awamu ya kwanza utakuwa katika hatua ya kuhamasisha kwa kuyafanyia marekebisho magari 200 huku hoteli za Southern Sun, Kilimanjaro Kempinski, New Africa, Sea Cliff na Movenpick zitakuwa katika awamu hiyo.

  “Vilevile taasisi za serikali kama Magereza ya Ukonga na Keko, Jeshi Mgulani na Hospitali ya Muhimbili vitakuwamo katika awamu hiyo,” alisema na kuongeza kuwa nyumba 70 katika eneo la Mikocheni, Dar es Salaam, nazo zitajumuishwa katika hatua hiyo.

  Katika mradi huo unaosimamiwa na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kwa kushirikiana na Pan African Energy, unatarajiwa kugharimu kiasi cha dola za Kimarekani milioni tatu.

  Kwa mujibu wa Ngeleja, mradi huo unaotekelezwa kwa kushirikiana na makampuni ya ECO Motors kwa pamoja na BICO ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Taasisi ya Teknolojia (DIT), katika hatua za mwanzo, serikali imefanikiwa kukusanya kiasi cha dola za Kimarekani milioni 74.3, huku ukiokoa kiasi cha dola bilioni 1.9 – kiasi ambacho kingetumika kuagiza nishati ya mafuta nje.

  Mwenyekiti wa Bodi ya TPDC, Jenerali mstaafu Robert Mboma, alimweleza waziri kuwa shirika hilo lingekuwa na ufanisi zaidi katika kubuni miradi endelevu ya nishati, ila tatizo ni ukosefu wa fedha.

  Jenerali Mboma alisema shirika hilo limeshindwa kuchangia miradi kadhaa inayohusu uendelezaji wa nishati kikiwamo kisima namba kumi cha Songosongo.

  Kutokana na kutoonesha uwezo wa kuchangia miradi hiyo, mwenyekiti huyo wa bodi alisema serikali imekuwa ikipoteza mapato huku ikidumaza kasi ya utekelezaji wa miradi hiyo.

  Mkurungezi wa Pan African Energy, Peter Clutterbuck, aliipongeza serikali na TPDC kwa kuonesha nia ya kuinua sekta hiyo, kwani itasaidia ukuaji wa uchumi.

  Source: Tanzania Daima

  ------------

  Ni move ya TPDC ni nzuri kwa maendeleo ya Watanzania, lakini inashangaza Serikali inatamba kukusanya pesa nyingi za mauzo ya Gas ila haitaki kuwekeza kwenye hiyo miradi ziweze kujizalisha zaidi, na ili iwe na control ya uchumi na energy sector kwa ujumla.

  Kwa mfano huu mradi ulikuwa ufanywe na serikali kupitia TPDC pekee ambapo miundombinu yote yaaani Pipeline networking za jiji lote zingemilikiwa na serikali, na hivyo kuwa na control kuanzia bei ya gas kwa wananchi na itakuwa ya kudumu kwa kizazi kijacho. Lakini wameshindwa kutoa pesa hizo zinazokusanywa hadi imebidi TPDC aingie ubia na Panafrican Energy kampuni binafsi ili itoe pesa !!!. wameshindwa kutoa Bil. 3 wakati wamekusanya Bil.70 !!!!!

  Je, serikali inaliona hili??? nchi zote zilizoendelea kama UK, Urusi, China, USA, Canada, n.k gas inasambazwa na kampuni za serikali.
   
 2. e

  eddy JF-Expert Member

  #2
  Jul 15, 2009
  Joined: Dec 26, 2007
  Messages: 9,381
  Likes Received: 3,775
  Trophy Points: 280
  Hapa Ngeleja katuwashia mshumaa tupate mwanga kidogo, iweje TPDC wakusanye 70bn then iwe tabu kupata 3bn + 32bn ya kuendeleza miradi yao? niwakati sasa kwa mashirika kama TPDC NHC TBA kuwa na mitaji yake yenyewe na kujiendesha kibiashara.

  Huu utaratibu wa kupeleka pesa yote General fund ya hazina urekebishwe, serikali ikusanye kodi stahiki tu.

  Lakini haya makampuni ya PanAfrican Energy, Royal Dutch Shell, Chevron, BAE system, Exxon, Baclays mbona yanakuwa kikwazo kwa maendeleo ya Africa? kutwa nzima yanarubuni viongozi wetu! tuje tuyaanzishie kichapo kama cha "The Movement for the Emancipation of the Niger Delta (Mend)"
   
 3. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #3
  Jul 15, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 0
  Hongera sana tpdc. Ingawa mmepigwa marufuku kule zenji
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Jul 15, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  May be these guys are going to be a bit cheaper!
  Lakini kama watakuwa juu ya au sawa na nishati zilizopo, sina la kusema!
   
 5. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #5
  Jul 15, 2009
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Kwa jinsi bongo mambo yalivyo tusichekelee kwanza tusubiri implementation!!!!!!!!!
   
 6. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #6
  Jul 15, 2009
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Ndio maana na wao hawatapeleka gas yao unguja katika awamu zote
   
 7. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #7
  Jul 15, 2009
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Hasa ukizingatia kuwa Mwenyekiti wa TPDC ni Jenerali mstaafu Robert Mboma? nikikumbuka uwizi wa Meremeta,waliokufa na Helicopter ya Jeshi, Magari ya Jeshi yaliyonunuliwa kwa bei mbaya, Boti za Jeshi zisizofanya kazi,Mboma aliyetaka kuwa mbunge......................Mhhhhhhhhhhhhhh tusubirie maumivu tu,[​IMG]
   
 8. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #8
  Jul 15, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,328
  Likes Received: 1,794
  Trophy Points: 280
  Ni mradi muafaka kwa daladala na taxi zinazo operate mjini kama Dar ili kushusha gharama za mafuta. Kwasababu ya ugumu wa storage ya gas kwa wale wanaotaka kutembea masafara marefu, sijajua nini mipango ya baadae ya kuwezesha refilling ili nalo pia liwezekane.
  However, the gas is cheap and clean compared to diesel and petrol. Na kubwa pia ni kuwa sulfur amount in the gas obtained in Tanzania ni ndogo sana kwahiyo even processing kwa ajiri ya matumizi ya nishati kwenye magari haitakuwa ya juu sana.Pia inawezekana gharama nyingine ikawa ni engine conversion kits...kutoka kwenye petrol kwenda kwenye gas. Sidhani kama itawezekana kubadili engine zinazotumia diesel kwa sasa kutokana na jinsi zilivyotengenezwa.
  Lakini Tanzania kila kitu kinawezekana...unaweza shangaa gas ikawa more expensive kuliko diesel
   
 9. Mpendanchi-2

  Mpendanchi-2 JF-Expert Member

  #9
  Jul 16, 2009
  Joined: Apr 4, 2009
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  You are very right, among the cheapest energy on earth ni Natural Gas, ndiyo maana ulaya including UK zimefunga bomba la gas toka Russia kupitia inchi zote. Na ndilo linatoa energy yote kwenye viwanda vya Ulaya. na hata majumbani na kwenye magari. Na haya mabomba yote yanamilkiwa na serikali za nchi husika!! Hivyo hakuna mtu binafsi ambaye anaweza kujibadilishia bei anavyopenda.

  Hili bomba la gas ya Russia ndilo humpa kiburi sana Rais wa Russia. Uingereza akileta kiburi tu , Russia hutishia kufunga bomba na uingereza hubadili misimamo.!! HIVYO hakuna nchi kubwa inayofanya mchezo na Energy na kuiachia sector binafsi. Ukifikia hapo maana yake serikali imechemka au viongozi wana hisa kwenye hiyo kampuni binasfi.

  Kwa mtindo huu Panafrica wanaweza kuamua kupandisha gharama za gas na wakiuulizwa watasema mtikisiko wa kiuchumi!! kumbe wizi mtupu!!!
   
 10. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #10
  Jul 16, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Wazo zuri sana, na ipo mifano ya nchi kadhaa ambazo zinazalisha gasi na kuitumia katika teski na kupunguza gharama za usafiri. Mfano mzuri ni teski za Jiji la Kuala Lumpur na Petaling Jaya.
   
 11. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #11
  Jul 16, 2009
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  wizi, waste of time and money.....
  hela nyingi itatumika kugeuza magari na nyumba kuwa zinatumia gesi
  cha maana hiyo hela ingenunua electricity generator turbines ambazo zinatumia gas badala ya zinazotumia diesel, hapo kungekuwa hamna haja yeyote ya kugeuza nyumba kuwa zinatumia gas.
  serikali inabidi ilekeze nguvu zange kwenye electrification nchi zima na kuongeza capacity ki kweli kweli na sio miradi ya kubebana(kupeana shavu)
  hiyo hela inatosha kugenerate 80MW ambayo inatosha kusupply umeme hoteli zote za dar na nyumba zote za mikocheni na zaidi ya hizo, na sio hoteli teule na nyumba za wateule mikocheni.

  mtera capacity 80mw
  tegeta capacity 40mw (gharama $34m) na ni gas turbine

  siwezi kuamini serikali inaingia gharama $70m kwa ajili ya hoteli 3, nyumba 70 mikocheni na magari 8200


  eti TPDC haina hela alafu imekusanya $70m, hii ni hela nyingi sio TZ hata nje ya TZ...
  hii ni dhairi kabisa watu wanajimilikisha na kujilipa wenyewe through uwekezaji....
   
 12. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #12
  Jul 2, 2014
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,582
  Likes Received: 1,943
  Trophy Points: 280
  Yaa! Cc Ngongo joka kuu, hizi habari ziko wakuu, niliona thread mpya Iiliyoanzishwa na Ngongo.
   
 13. K

  Kinombo JF-Expert Member

  #13
  Feb 22, 2015
  Joined: Feb 24, 2007
  Messages: 332
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  zero bado sijaona unafuu katika maisha ya mtanzania Gas juu. tusubili labda cement ya DANGOTE
   
 14. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #14
  Feb 27, 2015
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Umeona eeh!!!! hii habari kama zingine zilishajifia kimyaaaaaaaaaa!!!!!!!
   
 15. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #15
  Feb 27, 2015
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,341
  Likes Received: 2,668
  Trophy Points: 280
  Ukikutana na habari za kale kama hizi ndipo unapoweza kupata picha namna CCM walivyo waduanzi...
   
 16. rushanju

  rushanju JF-Expert Member

  #16
  Feb 27, 2015
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 2,342
  Likes Received: 1,055
  Trophy Points: 280
  Aliyefukua hii habari ana akili sana. Yaana ina mtiririko mzuri sana. Sinauhakika kama viongozi wetu wanasoma habari kama hizi
   
 17. 9

  999 JF-Expert Member

  #17
  Feb 27, 2015
  Joined: Jan 14, 2015
  Messages: 2,237
  Likes Received: 1,172
  Trophy Points: 280
  Hahahaha, hayo magari yanayotumia gas yako wapi?
  Nchi hii ni kupiga hela tuuu
   
 18. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #18
  Feb 27, 2015
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Siasa kwenye mambo ya kitaalamu wapi na wapi.
   
 19. Capt Tamar

  Capt Tamar JF-Expert Member

  #19
  Feb 27, 2015
  Joined: Dec 15, 2011
  Messages: 6,663
  Likes Received: 3,317
  Trophy Points: 280
  Huo uwekezaji mdogo walioufanya tpdc kwa kushirikiana na pan african energy haukuwa na bank account?? Hakuna pesa iliyowahi kuingizwa kwenye account hiyo??? Je bado account hiyo ipo? Je ina pesa kiasi gani?? Kama haina pesa je zimekwenda wapi? Any way je mradi umefikia wapi???? Najiuliza tu, tukumbuke mradi wa machinjio ya kisasa uliyokuwa ufanyike daressalaam,wilaya zote zilitoa pesa! Wabia wakatoa pesa! Zikfika kama bilioni moja na milioni kadhaa! Wajanja waka pause kidogo!!! Ile mafala tunakuja kushtuka!! Account ina Tsh 50,000!! Elfu hamsini za kitanzania!! Sasa hapo mboma ndio kasimama getini tutegemee nini?
   
 20. More Tiz

  More Tiz JF-Expert Member

  #20
  Feb 27, 2015
  Joined: Mar 28, 2013
  Messages: 2,235
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Tanzania tunayakiwa kufikia mahala pa kuwa na kumbukumbu ya miradi yote iliyopangwa kufanyika na iliyoanza kutekelezwa ili kuongeza nguvu ya kufuatilia na kuona utekelezaji wake ukoje. Nchi imekuwa na miradi hewa mingi mno, pia ilisiyokamilika ndio kabati zote zimejaa mikaratasi. Kwa aina hii ya utendaji hata tuwe na miaka elfu moja mbele hatuwezi kupiga hatua. Tunapaswa kupangilia ubunifu na utekelezaji wa miradi yetu itegemeane, yaani unapoisha mradi mmoja basi utakaofuata utumie plan na miundombinu iloyopo kuendelea sio kila mradi ukija ni kuanza kufumua miundombinu ya mwanzo na kuweka inayoendana na mradi mpya.
   
Loading...