TPDC: Kiwanda cha mafuta kwa mabaki ya mazao ( Biofuel & Biochemical = Fuel Ethanol )

Masalu Jacob

JF-Expert Member
Jul 26, 2017
948
1,092
Habari Tanzania !

Tuache kuagiza Petrol na Diesel nje ya nchi. Tunaweza jitengenezea sisi wenyewe na kujiuzia.

Tanzania sasa tunaweza anzisha viwanda na kujenga mitambo yetu ya kuchakata mabaki ya mazao kuwa nishati ya mafuta kwaajiri ya kuendesha vyombo vya moto na mitambo inayotumia hiyo nishati na tukapunguza ama kuacha kabisa kuagiza mafuta nje ya nchi.

Wataalamu wa fani ya Petroleum and Chemical Engineering mnaweza mkatusaidia kama taifa tukasonga mbele kwa ubunifu na kuboresha uchumi wetu kwa kuunganisha sekta mbalimbali mfano kilimo na misitu na tukafikia malengo kama taifa.

Mabaki ya mazao yanayotumika kuchakata nishati ya mafuta ni kama ifuatavyo; mabua ya mahindi na magunzi, mabaki ya ngano, mpunga, pamba, mbao nk

Uzuri kwa hayo mabaki au makapi katika Tanzania ni mengi kwahiyo tunaweza tengeneza ajira nyingi, kuongeza mapato kwa taifa na kujenga miundombinu mbalimbali.

Karibu.
 
Back
Top Bottom