TPA yafanya upembuzi bandari za Ziwa Nyasa

elivina shambuni

JF-Expert Member
May 31, 2018
462
500
1577345284318.png


MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari (TPA), imesema inafanya upembuzi yakinifu katika bandari zote za Ziwa Nyasa unaolenga kuboresha miundombinu na kuimarisha shughuli za kibiashara katika ziwa a waandishi wa habari katika Bandari ya Kiwira iliyopo wilayani Kyela mkoani Mbeya.

Alisema wameamua kuboresha miundombinu ya ziwa hilo ili kurahisisha usafirishaji kwa wananchi wanaozunguka maeneo hayo na kuimarisha shughuli za kibiashara na kukuza uchumi.

Alisema kwa miaka miwili iliyopita, hakukuwa na ongezeko la shehena kutokana na ukosefu wa meli na kwamba kufanyika kwa maboresho hayo, kutasaidia kukuza biashara kwa kasi kuanzia Januari mwakani.

Alisema wanatarajia kuanza kupitisha shehena za makaa wa mawe, tani 4,000 kila mwezi kuanzia mwaka "Mwezi wa kwanza (Januari) 2020, tutaanza kupitisha shehena za mkaa wa mawe, na baada ya hapo, tunatarajia kwamba biashara itakuwa nzuri zaidi, na tunaendelea na mikakati ya kimasoko ili watu waanze kutumia njia ya maji badala ya barabara," alisema.

Aliongeza kuwa miaka mitano iliyopita, walikuwa wakihudumia kati ya tani 5,000 hadi 10,000 kwa mwaka na mapato yalikuwa yanafikia Sh. milioni 300 kwa mwaka na kwamba kwa sasa baada ya kuboresha miundombinu na uwekezaji wa meli walioufanya, wanatarajia kuanza kusafirisha mizigo zaidi na kuzalisha faida kubwa.

"Lakini, kwa mipango tuliyonayo kwa sasa, tunatarajia kwamba tutafikia hadi kuhudumia tani 76,000 kwa mwaka na mapato kufikia Sh. bilioni tatu kwa mwaka.

"Mwanzoni shida iliyokuwa inachangia kutokusafirisha shehena nyingi, ni kukosekana kwa vyombo vya kusafirishia mizigo, bandari siku zote haiwezi kufanya kazi kama hakuna vyombo vya kusafirishia.

Kwa hiyo, uwekezaji wa meli uliofanywa na serikali kwa sasa ndiyo unakwenda kuchagiza ongezeko hilo la shehena pamoja na mapato," alisema.

Alibainisha kuwa Ziwa Nyasa lina bandari rasmi 15, huku asilimia 90 ya mizigo inayosafirishwa katika bandari za ziwa hilo ikiwa ni makaa wa mawe.

Alitaja bandari hizo kuwa ni pamoja na Itungi, Kiwira, Matema, Lumbila, Ifungu, Nsisi, Makonde, Lupingu, Manda, Liuli na Mbamba Bay
 

Mwadunda

JF-Expert Member
Aug 14, 2013
1,743
2,000
Mkaa mwingi unachimbwa wilayani Mbinga na Nyasa Mkoani Ruvuma hivyo sehemu ya msingi kujenga bandari ilikua ni Liuli, na kuimarisha bandari ya Mbambabay na sio vinginevyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Top Bottom