TPA wakamilisha agizo la Rais Magufuli la kuweka mashine mpya za kisasa za kukagua mizigo

BilioneaPATIGOO

JF-Expert Member
Jun 23, 2012
12,321
11,314
Mpango wa kuweka mashine mpya za kisasa za kukagua mizigo katika Bandari ya Dar es Salaam ambazo zina uwezo wa kusoma na kupeleka taarifa na picha za mizigo kwenye mifumo ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) na Mamlaka ya Mapato (TRA) umekamilika.

Kukamilika kwake kumetokana na maagizo aliyoyatoa Rais John Magufuli kuwa TPA na TRA zishirikiane kuendesha mashine za kukagua mizigo zinazotoa taarifa na picha mubashara, pamoja na kufanya kazi pamoja ili kuhakikisha serikali haipotezi mapato na kupitisha mizigo haramu.

Kuwepo kwa mashine hizo kutazisaidia TPA na TRA kubaini shehena zilizoko kwenye makasha yanayofikishwa bandarini hapo kupelekwa na kutoka nje ya nchi kama inawiana na nyaraka za mzigo huo, hivyo kutozwa ushuru sahihi kwa mzigo stahiki, Lengo la kufunga mashine hizo ni kuongeza mapato kwa serikali.

Meneja wa mradi huo, Zhang Sheng amesema Jumanne hii kuwa mradi huo umekamilika na sasa wako katika hatua ya pili ya mafunzo na skana hiyo mpya inaweza kutumika muda wowote mara baada ya kukamilisha mafunzo.

Kwa mujibu meneja huyo kutoka China, skana hiyo ina uwezo wa kusoma na kupeleka taarifa na picha za mizigo mubashara kwenye mifumo ya TPA na TRA kwa wakati mmoja bila kuchelewa.

Kutokana na kukamilika kwa mradi huo, TRA na TPA zimeanza kuwapa mafunzo watumishi wao namna ya kutumia mashine hizo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa TPA , Deusdedit Conatus Vitalis Kakoko, wakati akifungua mafunzo hayo ya siku tano alizipongeza serikali zote mbili kwa kukamilisha mradi huo.

“Nazipongeza Serikali za Tanzania na China kwa kuwezesha mradi huu kukamilika. Tunatarajia mafunzo hayo yatawaongeza uwezo wafanyakazi, ufanisi wa bandari pamoja na kuongeza mapato ya Serikali,” alisema Kakoko.

Rais Magufuli alitoa agizo hilo baada ya kubaini kuwa kati ya mashine nne za ukaguzi wa mizigo zilizopo, ni mashine mbili tu ndizo zinafanya kazi na hazina uwezo wa kukagua mizigo yote inayotoka na kuingia nchini kupitia bandari hiyo hali inayosababisha kutokuwepo kwa udhibiti wa uhakika wa udanganyifu.

1479905350705.jpg
 
yaani unaziagiza mashine,zinaandaliwa,zinapakiwa kwenye meli.

ili kupata kiki,unaenda bandarini, ukijua kabisa mzigo wa mashine uko njiani na umelipiwa,unapiga mikwara pale,hiki,kile,hiki,kile

kumbe wajua kila kitu
Kama walivyoandaliwa waendesha baiskeli kutoka Mbalali hadi Dodoma kwa Lowassa ili kumshawishi agombee urais...na njia nzima hakuna aliyeona msafara wao.
Maigizo ni upande ule huku ni kazi tu.
 
Back
Top Bottom