BWANKU M BWANKU
JF-Expert Member
- Jan 12, 2019
- 328
- 414
Mamlaka ya usimamizi wa bandari Tanzania (TPA) Leo Jumatano Machi 16, 2022 imeingia makubaliano ya kibiashara na kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo Mkoani Mtwara yenye lengo la kurahisisha usafirishaji wa Saruji kwa kutumia bandari ya Mtwara.
Makubaliano hayo Yanawezesha kampuni ya Dangote kutumia bandari ya Mtwara , Tanga na Dar es salaam na yanatarajiwa kuongeza uzalishaji wa saruji katika kiwanda hicho kutoka tani 15000 za mwanzo mpaka 43000 kwa mwezi .
Akizungumza kwenye Hafla hiyo ya Utiaji Saini Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Brig. Jen. Marco Gaguti amesema hatua hii ni mafanikio ya Serikali ya Rais Samia kuweka mazingira mazuri na wezeshi kwa Wafanyabiashara na Wawekezaji kufanya biashara bila kugudha yoyote huku mazingira yakiwa yameboreshwa sana.
Makubaliano hayo pia yameshuhudiwa na viongozi mbalimbali wa Mkoa akiwemo Mkuu wa mkoa wa Mtwara Mhe. Brig. Jen. Marco Gaguti, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Dunstan Kyobya na Viongozi wengine mbalimbali.