TPA madudu matupu, PSSSF imefilisika, NSSF haina fedha, TASAC ubadhirifu mtupu sasa hawa CHADEMA wanapigana na Ufisadi gani?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,867
141,801
Chadema wamekuwa wakijinasibu kwamba wao ni wapambanaji wa ufisadi na rushwa na hawatakaa kimya hadi rushwa itokomezwe.

Sasa jana nilishangaa kila DG mteule wa taasisi aliyesimamishwa na Rais Samia aliambiwa akamalize vitendo vya rushwa na wizi katika taasisi aliyoteuliwa kuiongoza.

Yaani kote TPA, TRA, TASAC, NSSF, PSSSF, Tamisemi BoT Hazina ni vurugu tupu watu wanakwiba tu.

Ndio najiuliza hawa Chadema waliodai wao ni wazalendo na wanapambana na ufisadi kweli kweli, KULIKONI?

Ukinizingua Nitakuzingua!
 
Bwashee vipi dishi limeyumba wakati hata mwezi mama hajamaliza?

Hizo lawama ni za mwenda zake na serikali yake ya CCM hapo CHADEMA unawaingiza vipi bwashee? CHADEMA kama wapinzani kazi yao ni kufichua mautopolo ya chama tawala na serikali yake. Hawana mamlaka ya kupambana na mafisadi bwashee.

Bwashee tukuwahishe India au Nairobi?
 
Sasa mbona hawajafichua hayo mautopolo hadi mama mwenyewe kayafichua?
 
Tatizo ni urasimu na mfumo, kwa maana nyingine hata Hayati pia alikuwa akipigana na matatizo hayohayo ya ufisadi tukiamini ameyamaliza lakini bado.

Wazee wa Tasac wa bodi wamekula bilioni 6 kwa vikao tuu. Wakiongozwa na Profesa Sata na mkinga akiwemo. Bodi wao wanawekewa vikao tuu lakiji wahusika nimkutoka huko Tasac management haswa Finance.
 
Tumia Akili Chadema wanaserikali? Kazi ya Vyama vya Upinzani ni Kuibua Machafu ya Serikali lakini kwa Serikali ya Hayati kila kitu kilikuwa sawa kwani TANZANIA ni TAJIRI sana
Mara ya mwisho Chadema kuibua ufisadi ni wakati wa JK, why?!!
 
Tatizo ni urasimu na mfumo, kwa maana nyingine hata Hayati pia alikuwa akipigana na matatizo hayohayo ya ufisadi tukiamini ameyamaliza lakini bado.

Wazee wa Tasac wa bodi wamekula bilioni 6 kwa vikao tuu. Wakiongozwa na Profesa Sata na mkinga akiwemo. Bodi wao wanawekewa vikao tuu lakiji wahusika nimkutoka huko Tasac management haswa Finance.
Renatus Mkinga ana njaa sana yule mzee!
 
Back
Top Bottom