TP Mazembe tupo pamoja na nyinyi kwa hali na mali hapo kesho

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
52,073
114,571
Kesho Mungu akipenda pale uwanja wa Taifa, Yanga na TP Mazembe watakipiga. Inashauriwa sana watanzania wote tuweke uzalendo mbele eti Yanga inawakilisha nchi.
Hakuna kitu kama hicho, Yanga inawakilisha Yanga. Nipo huru kuwa timu yeyote na nitakuwa TP Mazembe na wenzangu tunaokerwa na Yanga. Tayari nimesha-bet Yanga itapigwa 0-2.
Sababu zipo nyingi lakini kubwa ni kwamba Yanga wanadharau sana na wamejaa majivuno kwa club za ndani.
Msemaji wao amekuwa akirusha kashfa na matusi kwa kila aliye mbele yake mwenye mawazo kinzani. Kwa kuwa Yanga haijawahi kumchukulia hatua naamini wanamtuma kufanya hayo madudu. Juzi kwa kejeli alitutaka mashabiki wa Simba tuipe sapoti Yanga, lakini akaongeza tusipoipa watatushusha daraja msimu ujao.Hizi ni kauli za Ujuha na upumbavu uliokidhiri.
TP Mazembe tupo pamoja na nyinyi kwa hali na mali hapo kesho
 
Kesho Mungu akipenda pale uwanja wa Taifa, Yanga na TP Mazembe watakipiga. Inashauriwa sana watanzania wote tuweke uzalendo mbele eti Yanga inawakilisha nchi.
Hakuna kitu kama hicho, Yanga inawakilisha Yanga. Nipo huru kuwa timu yeyote na nitakuwa TP Mazembe na wenzangu tunaokerwa na Yanga. Tayari nimesha-bet Yanga itapigwa 0-2.
Sababu zipo nyingi lakini kubwa ni kwamba Yanga wanadharau sana na wamejaa majivuno kwa club za ndani.
Msemaji wao amekuwa akirusha kashfa na matusi kwa kila aliye mbele yake mwenye mawazo kinzani. Kwa kuwa Yanga haijawahi kumchukulia hatua naamini wanamtuma kufanya hayo madudu. Juzi kwa kejeli aliomba kwa kejeli mashabiki wa Simba tuipe sapoti Yanga, lakini akaongeza tusipoipa watashusha daraja msimu ujao.Hizi ni kauli za Ujuha na upumbavu uliokidhiri.
TP Mazembe tupo pamoja na nyinyi kwa hali na mali hapo kesho
Uko sawa, Muro atawaponza Yanga, nami kwa kesho (pamoja na kuwa si mpenzi wa mpira) wapigwe tu! (Mizengo)
 
Tanzania hatuwezi mpira period, sisi tunaweza michezo kama riadha na ngumi pekee. Tunapoteza muda mwingi na fedha kwa kitu tusichokiweza.
 
Mimi Simba damu damu lakini, sijaona sababu zako za msingi hasa, eti dharau na majivuno!!? Sure? Kama hizo ni sababu za msingi, nahisi unaishi, maisha ya kukosa raha mtaani kwa sababu ya watu wenye maendeleo kukuzidi. Usimba na Uyanga kuwa juu ya mwenzio ni kumfunga na kuchukua makombe.. Simba tuchukue kombe makombe tuone kama yanga watakuwa na dharau na majivuno.

NB: tuwaunge mkono yanga na tuwapongeze panapo stahili, lasivyo ni taswira mbaya tunaijenga katika macho ya Dunia.
 
Napenda sana hiyo vishabiki vya simba vyote viwe tp(toilet paper)mazembe ili tuvinyooshe zaidi!!!na vya azamu pia
Azam ni wastaarabu sana siyo kama baadhi ya mikia fc except Katavi et al. Kesho wafurike kuwashangilia hao TP Mazembe, hakuna mjadala TP Mazembe ni lazima afungwe whether anataka au la.
 
Tanzania hatuwezi mpira period, sisi tunaweza michezo kama riadha na ngumi pekee. Tunapoteza muda mwingi na fedha kwa kitu tusichokiweza.
Hiyo stroke yako haijakuua tu hadi leo bado unaongea? Kama hujafa, kesho ni lazima utakufa baada ya Yanga kuibamiza TP Mazembe.
 
Hiyo stroke yako haijakuua tu hadi leo bado unaongea?
Nimeshaacha siku nyingi sana kwenda kuangalia wakata viono uwanjani for nothing..unatoa pesa yako unaingia uwanjani unaishia kua disapointed, sipotezi muda wangu kuangalia mpira wa Tanzania, ule hata sio mpira ni ngoma flani hivi za mdundiko.
 
Kama huo ndio msimamo wako kwa nini unapoteza muda ku-comment vitu ambavyo umeshaachana navyo?
 
Azam ni wastaarabu sana siyo kama baadhi ya mikia fc except Katavi et al. Kesho wafurike kuwashangilia hao TP Mazembe, hakuna mjadala TP Mazembe ni lazima afungwe whether anataka au la.
OK basi kwa sababu kesho ni vita na Mara chache vita huchagua basi hao azamu wachache wastarabu washike kitambaa cha njano au kijani ili kipigo kikianza tuwatambue bila watatulaumu bure!!!!mbumbumbu wao walishakata tamaa na wako tayari kulia
 
Kama huo ndio msimamo wako kwa nini unapoteza muda ku-comment vitu ambavyo umeshaachana navyo?
Natoa msaada kwa wale wasioelewa kua wanapoteza muda na fedha kwenye kitu ambacho, hakitakaa kuleta faida yoyote kwa taifa hili, Tanzania HATUWEZI MPIRA, huo ni Ukweli, na utasubiri sana mpaka uzeeke kusikia tumefika popote. Ndio maana Mataifa ya watu wenye akili zao, wanafanya mambo yale wanayoweza na kwa bidii zote, Ona kenya wao wamekomaa na riadha na imewatoa, ona marekani walivyowekeza kwenye basketball na inawanyanyua, unless tufunguke akili na kufanya kile tunachoweza tutaendelea kufanya yale yale over the years, and trust me, mpira hapa bongo hautakaa utupeleke kokote.
 
Back
Top Bottom