Tozo zote za simu zinapaswa kuondolewa ili kukuza uchumi

Getse

New Member
Jul 29, 2021
1
0
Tozo zote za simu zinapaswa kuondolewa ili kukuza uchumi
Kwa mujibu wa taarifa za mtandaoni inakadiriwa kuwa watu zaidi ya bilioni 5 ulimwenguni wanatumia simu za mkononi katika shughuli mbalimbali za mawasiliano.

Mbali na kuwezesha mawasiliano huduma za simu zinatajwa kama kichocheo kikubwa cha maendeleo katika sekta tofauti, watu huzitumia katika shughuli zao mbalimbali. Kuwa na simu si anasa tena kama zamani bali ni kitu muhimu.

Kutokana na umuhimu huo Serikali imeondoa kodi ya ongezeko la Thamani kwenye simu janja za mkononi, vishikwambi (Tablets) na modemu la thamani ili kuongeza matumizi ya simu hata hivyo imeongeza gharama za uendeshaji ambao huenda ukaathiri lengo hilo.

Katika bajeti ya sasa (2021/2022) Serikali ilianzisha tozo mpya ya miamala ya simu ambapo mtumiaji wa huduma hiyo muhimu anakatwa kiasi fulani cha fedha kila anapotuma na kutoa fedha, Kiwango hicho kinaanzia Sh10 hadi Sh10,000 kulingana na thamani ya muamala.

Serikali inatarajia kukamua Sh1.65 trilioni kama kodi mpya kutoka kwa watumiaji wa simu za mkononi zaidi ya milioni 50 nchi nzima, hata hivyo imeweka unafuu wa kupata vifaa vya mawasiliano.

Kutokana na viwango vilivyowekwa kilele za watumiaji wa huduma za miamala zilikuwa kubwa na kuna hofu kuwa kwa siku zijazo watu wanaweza kushindwa kumudu gharama za huduma na kutafuta njia mbadala za kufanya mawasiliano. Serikali imesema tozo hiyo haitaondoka bali inafanyiwa mapitio.

Miamala ya simu kwa sehemu kubwa ndiyo imechangia tanzania kuongeza wigo wa huduma za fedha jumuishi (financial Inclusion), watu ambao walikuwa hawawezi kufikia huduma za kifedha kupitia benki sasa simu inarahisisha mambo.

Wakati huohuo Serikali inajiandaa hivi karibuni kuanza kutoza Sh10 hadi 200 kila mtu aongezapo salio katika simu yake, jambo ambalo huenda likaongeza gharama ya vifurushi au kupunguza ukubwa wa vifurushi.

Tozo ya muda wa maongezi inakuja wakati ambao wananchi wanalia na gharama kubwa za bando, miezi kadhaa iliyopita kelele za gharama kubwa ya bando zilisababisha Serikali kuingilia kati baada ya hapo kilio kiliongezeka zaidi kwakuwa bado zilipanda mara dufu, uamuzi ukafanyika kurudisha hali ya awali.

Kwanini katika huduma za simu ziondolewe
Kama ilivyoelezwa hapo juu huduma za simu si anasa kama ilivyokuwa siku za nyuma wala simu si kwa ajili ya mawasiliano pekee bali simu ni maisha kwa ujumla, simu ina mchango mkubwa katika nyanja za kijamii na kiuchumi kulingana na matumizi yake.

Uchumi wa kidijitali ndiyo unapigiwa chapuo kote dunia na simu ina nafasi kubwa ya kufanikisha hilo, unafuu wa kuwawezesha wengi kutumia huduma za simu utakuza shughuli za kiuchumi na Serikali itapata kodi zaidi kama mbadala wa mapato yaliyotegemea kutoka katika tozo hizo.

Sekta ndogo ya simu imeajili watu wengi kama mawakala wa huduma zake mbalimbali lakini pia simu kuwezesha mawasiliano na utumiaji wa mitandao ya kijamii kumeibua fursa kubwa ya biashara mtandaoni na masoko ya kimtandao.

Watu wengi huuza na kununua bidhaa zao mtandaoni na malipo hufanyika hukohuko, tozo ambazo hupandisha gharama kubwa za huduma kuna uwezekano mkubwa zikadhoofisha biashara hizo na uchumi kwa ujumla jambo ambalo litaathiri ukusanyaji wa tozo hiyo na hata kodi nyingine kutokana na kusinyaa kwa uchumi wa mtu mmojammoja.

Faida ya kuwepo kwa tozo za simu inaweza kuwa ni ndogo au usiwepo kwa kuwa kama ni mapato, Serikali inaweza isikusanye zaidi kutoka chanzo hicho kwakuwa kuna uwezekano wa matumizi ya watu yakapungua lakini endapo kukiwa na nafuu ya gharama katika huduma watu watatua kwa wingi na wengi zaidi hivyo Serikali itakusanya zaidi.

Tayari kodi katika huduma za simu ni kubwa
Tayari serikali inatoza kodi kwenye gharama za miamala lakini pia kwenye muda wa maongezi, kuweka tozo mpya tafsiri yake ni kutozwa kodi mara mbilimbili, mtu anaweza asione thamani ya Shilingi 5 au Shilingi 10 lakini ukishindwa kupata bado la shilingi 1,000 mpaka uweke shilingi 1,010 ndipo utagundua Sh10 ni kubwa.

Ripoti hiyo iliyotolewa Shirikisho la kampuni za simu (GSMA) mwanzoni mwa Machi, 2021(kabla ya kuanzishwa kwa tozo mpya) inaeleza kuwa miongoni mwa kodi kubwa zinazowaumiza watumiaji wa huduma za simu ni ushuru wa bidhaa ambayo ni asilimia 17 ambayo ikijumlishwa na kodi nyingine zinafikia takribani asilimia 40.

Shirikisho hilo linasema mpaka mwaka 2019 jumla ya mapato ya sekta ya mawasiliano ya simu nchini ilikuwa Sh2.7 Trilioni na kwa mwaka kodi iliyolipwa ilikuwa Sh932 bilioni sawa na asilimia 34 lakini ikijumlishwa na kodi ya zuio inaongezeka na kufikia asilimia 38.

GSMA linasema endapo ushuru wa bidhaa utapunguzwa kwenye vocha kutoka asilimia 17 ya sasa hadi asilimia 12 pekee itasaidia kuinua uchumi kwa kiwango kikubwa na miaka mitano ijayo sekta hiyo itaongeza ajira 44,500 huku pato la taifa likiongezeka kwa dola milioni 438.

“Kupunguza asilimia 5 kwenye kodi ya ongezeko la thamani kutaongeza uwezo wa watu kumudu gharama za simu kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na biashara hivyo watumiaji milioni 2.4 wataongezeka na kati yao asilimia 87 watakuwa wale wa kipato cha chini,” inasema ripoti hiyo.

Ripoti hiyo inasema maboresho hayo ya kodi yakifanyika mitandao ya simu itakuwa na uwezo wa kuongeza dola milioni 3 kila mwaka kuwekeza kwenye ubora na usambazaji wa huduma na kwakuwa jambo hilo litaongeza unafuu wa huduma biashara itakuwa kubwa na uwekezaji katika sekta utaongezeka kwa dola milioni 49.
 
Back
Top Bottom