Tozo zimezidi, nchi yetu tuiite 'Tozonia' badala ya Tanzania

Kichuchunge

JF-Expert Member
Dec 2, 2020
337
886
Nimeona sehemu fulani Waziri wa Tamisemi Mh Ummy Mwalimu akisitisha tozo ya maegesho ya magari kwa njia ya kielektroniki kutokana na malalamiko ya wengi kuzidi.

Hiyo ni sehemu tu ya malalamiko ya Watanzania walio wengi ambao kwa sasa wanaelemewa na tozo. Tangu serikali hii ya awamu ya sita iingie madarakani, tozo zimezidi kwa kweli. Kuanzia kwa wakulima kuna tozo sijui ya mazao, tozo ya mbolea tozo ya pembejeo, hapo katikati kulikuwa na tozo sijui ngapi zinazokatwa kwenye mafuta.

Si hizo tu, kwenye umeme kuna tozo, kwenye miamala ya simu ndio usiseme, watu wameimba hadi wameamua kunyamaza wakiugulia maumivu kimya kimya. Hata makampuni ya simu nayo yameamua kufanya yao kwa kupandisha hadi bei za vifurushi vyao kimya kimya kisa?

Tozo zimewaelemea na wao wanaamua kumsukumia mlaji wa mwisho ambaye ni mlalahoi.

Kwa kitendo hicho cha kuzidiwa kwa tozo, kwa nini basi nchi yetu tusiibadili tu jina na kuiita 'TOZONIA' badala ya Tanzania maana tozo zimezidi?
 
Amir3.jpg
 
Masika ya mvua za tozo
 
Kwa nini ushuru wa kupaki gari usingelipwa pindi gari inatoka bandarini ukawa renewed ata baada ya miaka 2 au 3. Waweke kiasi rafiki basi tuachane kutukanana na vijana hovyo.
 
NINYI MNAOONA YA KWAMBA TOZO HIZI NI KUBWA MNAWEZA KWELI KUISHI NCHI ZA ULAYA AMBAZO NDIKO BABA YAKE TOZO ALIKO?
 
Back
Top Bottom