Tozo za simu zisijenge vituo vipya vya afya badala yake zikaboreshe upatikanaji wa dawa na vifaa tiba

Uncle Jei Jei

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
1,643
2,000
Binafsi nimefanikiwa sana kuzunguka mikoa kadhaa ya nchi kwa kazi maalumu za miradi ya afya. Kwa sehemu kubwa nimejionea namna zahanati zilivyojengwa hadi vijijini kabisa

Tatizo kubwa la nchi hii ni zahanati hizo kukosa wahudumu hasa za vijijini, dawa na vifaa tiba

Zahanati ili ikamilike haitegemei jengo pekee. Zahanati/kituo Cha afya/ hospital ni jumla ya jengo, wahudumu, vifaa tiba na dawa.

Jengo hata likiwa zuri kiasi gani na rangi za kupendeza Kama hakuna wahudumu na dawa ni kazi bure!

Tuboreshe vilivyopo kwanza tuokoe maisha ya wananchi wetu! Hebu angalia yule tabibu wa Korogwe aliyefumua nyuzi jeraha la mgonjwa wake kisa tu ameshindwa kulipa hela ya huduma!

Serikali ingewekeza zaidi kwenye upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kirahisi kuliko majengo hata huduma za afya zingekuwa nafuu sana!

Ukija kwenye Shule hali ni hiyo hiyo. Madiwani wamekazana kujenga maboma pasipokuyakamilisha na ukiangalia idadi kubwa ya wanafunzi wanakaa chini kwa kukosa madawati

Shule hazina vyoo bora, hazina ofisi ila zimejaa maboma yasiyokamilika

Madarasa hayakarabatiwi ila wamekazana kujenga maboma

Maabara toka enzi za Lowasa ni maboma kwa sehemu kubwa. Sasa unajiuliza, hizi gharama za maboma zingetumika kuboresha madarasa na kutengeneza madawati si Shule zingependeza na kuvutia wanafunzi kujifunza?

Wanajenga madarasa kwa kisingizio Cha kupunguza msongamano lakini hayakamiliki. Msongamano unabaki pale pale, uchakavu unabaki pale pale na uhaba wa madawati unabaki pale pale kinachoongezeka ni 'unfinished buildings"
 
Serikali ijifunze kuwa strategic kwa kuepuka kufanya Mambo kisiasa. Wanataka kujaza majengo yanayoonekana ili kuhadaa wananchi wakati kiuhalisia majengo hayana msaada sana
 
gachacha

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
2,099
2,000
Basi kama ni hivyo waongeze kwenye miamala ya bank ikatwe tozo ya vituo vya afya na madawa.

Kodi saivi haiwatoshi tuu
 
black sniper

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
18,904
2,000
Hayo ni mambo ya kawaida kwenye nchi masikini ambapo viongozi baadhi hawajali na kujilimbikizia wao mali

Wanajua sana kuwa tatizo kubwa ni madawa lakini wanatudanganya kwa majengo bila wauguzi wala madawa na bado wananchi wanakosa huduma ndogo hata bandage tu
Na kila kitu utanunua

Huko shule ndio usiseme kabisa kwani kila leo wanaandika kuwa wanafunzi wanajisaidia Porini na wengine wanaliwa na Simba

Ila matamko na ufuatiliaji ni mdogo mno kwa sababu hawajali
 
yuzazifu

JF-Expert Member
Oct 6, 2018
5,129
2,000
umepiga kwenye mshono, rais akidili na jambo hili hata tusiompenda tutalazimika kumpenda coz atakua kaleta suluhu ya changamoto ya muda mrefu.
 
Mchigondo

Member
Jul 10, 2021
28
75
Nakushukuru kwa kulisema hili. Hoja nzuri kabisa. Hata zile hospitali za mikoa ambazo sasa zinaitwa za rufaa, hili ni jina tu, lakini zina mapungufu mengi ikiwa ni pamoja na matibabu ya kibingwa. Hivyo hivyo wilayani. Inatakiwa suala hili tuliangalie qualitatively na sio quantitetively
 
pilipili kichaa

JF-Expert Member
Sep 3, 2013
13,375
2,000
Bado nimesikia leo ktk vyombo vya habari tunakwenda kununua tena mindege! Kama ni kweli basi huu ndio uendawazimu uliobakia duniani!
 
Anonymous Caller

JF-Expert Member
Sep 8, 2016
305
500
hivi tukija na policy ya matibabu bure nin kinashindikana.

kwamba, hii exemption iwe japo kwny maradhi ya maralia tu.

hayo mazahanati hayamsaidii asiye na hela.
yaan dharura ya ugonjwa ikitokea kpnd huna hela zahanati haina cha kukufaa.

yani ni bora hiyo trilion itakayokusanywa kwny chanzo hiki ni bora kila mkoa upewe kilomita 100 za lami.
 
Biggs

JF-Expert Member
May 3, 2014
1,072
2,000
Binafsi nimefanikiwa sana kuzunguka mikoa kadhaa ya nchi kwa kazi maalumu za miradi ya afya. Kwa sehemu kubwa nimejionea namna zahanati zilivyojengwa hadi vijijini kabisa

Tatizo kubwa la nchi hii ni zahanati hizo kukosa wahudumu hasa za vijijini, dawa na vifaa tiba

Zahanati ili ikamilike haitegemei jengo pekee. Zahanati/kituo Cha afya/ hospital ni jumla ya jengo, wahudumu, vifaa tiba na dawa.

Jengo hata likiwa zuri kiasi gani na rangi za kupendeza Kama hakuna wahudumu na dawa ni kazi bure!

Tuboreshe vilivyopo kwanza tuokoe maisha ya wananchi wetu! Hebu angalia yule tabibu wa Korogwe aliyefumua nyuzi jeraha la mgonjwa wake kisa tu ameshindwa kulipa hela ya huduma!

Serikali ingewekeza zaidi kwenye upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kirahisi kuliko majengo hata huduma za afya zingekuwa nafuu sana!

Ukija kwenye Shule hali ni hiyo hiyo. Madiwani wamekazana kujenga maboma pasipokuyakamilisha na ukiangalia idadi kubwa ya wanafunzi wanakaa chini kwa kukosa madawati

Shule hazina vyoo bora, hazina ofisi ila zimejaa maboma yasiyokamilika

Madarasa hayakarabatiwi ila wamekazana kujenga maboma

Maabara toka enzi za Lowasa ni maboma kwa sehemu kubwa. Sasa unajiuliza, hizi gharama za maboma zingetumika kuboresha madarasa na kutengeneza madawati si Shule zingependeza na kuvutia wanafunzi kujifunza?

Wanajenga madarasa kwa kisingizio Cha kupunguza msongamano lakini hayakamiliki. Msongamano unabaki pale pale, uchakavu unabaki pale pale na uhaba wa madawati unabaki pale pale kinachoongezeka ni 'unfinished buildings"
Absolutely na hiki ni kilio cha muda mrefu. Pamoja na juhudi inazofanywa katika kujenga na kuboresha vituo vya afya kwa lengo la kusogea huduma hizo kwa wananchi impact haitaonekana kama hatutakuwa na sustainability katika upatikanaji wa kutosha wa Dawa/Vifaa/Vifaa Tiba na Vindendanishi hata kama vituo hivyo vitakuwa na miundombinu na wataalamu stahiki na wa kutosha kulingana na aina ya huduma.
Hivyo ni vyema makusanyo ya sasa kwa sehemu kubwa yangelenga kuiba pengo la upatikanaji wa mahitaji hayo ya kutosha plus wataalamu then kiasi kinachobaki kielekewe kwenye ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya vituo vya kutolea huduma za afya.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom