Tozo za miamala zitasaidia ujenzi wa Shule zaidi ya 10,000; zahanati zaidi ya 4,500 na vituo vya afya 570 ifikapo 2025. Uzalendo zaidi unahitajika

Tulipe kodi, mbona sio hela nyingi, tena ukilinganisha na nchi za wenzetu, kodi yetu ya miamala iko chini nitaweka data hapa, watanzania hawana utamaduni wa kutaka kulipa kodi, watumishi wa umma na sector binafsi ndio walipaji wakubwa wa kodi.

Ila wafanya biashara huwa hawataki hata kusikia 1% ya kodi imeongezeka. Watumishi wa umma hulipa hadi 30% ya makato yote ya mshahara. Ila mfanyabiashara akisikia hata 3% ya kodi imeongezeka, ni kelele na hawataki kusikia. Tulipe kodi plz
hakuna asie taka kulipa kwanini wabunge na viongozi mbali mbali hawakatwi? kama kweli ni uzalendo na wao wakatwe
 
Elewa maana ya Bajeti ya nyongeza,

Hii basket fund niekwaajili yaemaendeleo vijijini tu,

Budget zingine zitaendelea kama kawaida
Kuna tatizo gani zahanati nk. zikaendelea kujengwa kama awali bila kuangamiza wananchi?
EEF375B2-D39E-4A11-9F59-82D6A408C1F9.jpeg
4BA49365-D433-4D31-90B9-D74EB61134C4.jpeg
 
Mkuu hayo mazahanati na vituo vya afya havisaidii kitu, wangesema hospital zote za mikoa au wilaya zitakuwa na madktari bingwa wa magonjwa mbalimbali ikiwemo na vifaa tiba kama CT scan, MRI nk hapo ingekuwa sawa, kwenye vituo vya afya na zahanati waganga wanatibu kwa kutabiri tu matokeo yake vifo visivyo vya lazima vinakuwa vingi.Hivi CT scan ni sh ? kwann haipo kila mkoa? mgonjwa ulazimika kwenda km 300 kupata huduma hiyo hamuoni kama ni umbali mlefu sana? nako akienda hiyo gharama sasa!!!! kama sio mtumishi wa huma mwenye bima ya afya anakufa wanamwangalia tu. Hizo tozo zingelenga hapo, vituo vya afya wananchi wanaweza kujenga wenyewe kwa nguvu zao na serikali ikachangia kidogo.
Wazo zuri ila sio kugomea tozo, zitumikaje ni mjadala mwingine
 
Huyu mama anahesabu kali sana huenda akavunja rekodi kwa ujenzi wa miundombini ya maendeleo kwa wananchi.

Japo makato yanauma ila kama mambo ni haya niko tayari.
Punguza ujinga: kama nia ilikuwa njema wananchi walipaswa kujua mnakadiria kupata shilingi ngapi? Kwa muda upi? Na je mgwanyo wa matumizi utakuwaje kwa kila halmashauri.
Waambieni vile vile nini kitafuata endapo mambo yataenda ndivyo sivyo!
Tukumbuke kuwa hii ni tozo ya hiyari siyo kodi ya lazima. Wapo ambao watagoma kuilipa kwa kuacha kutumia mitandao ya simu na hakuna mtakacho wafanya!

NB: mngepata hela nyingi endapo mngeamua kusitisha manunuzi ya magari ya kifahari kwa pesa za wananchi hao hao mnao rudi kuwakamua!
Mmetapeli mengi; sidhani kuwa mna nia njema!
 
Wapunguze matumizi serikalini, hasa kwa viongozi, misafara, safari za nje, magari yenye gharama n.k.
Wabunge waongezewe kukatwa kodi..
 
Punguza ujinga: kama nia ilikuwa njema wananchi walipaswa kujua mnakadiria kupata shilingi ngapi? Kwa muda upi? Na je mgwanyo wa matumizi utakuwaje kwa kila halmashauri.
Waambieni vile vile nini kitafuata endapo mambo yataenda ndivyo sivyo!
Tukumbuke kuwa hii ni tozo ya hiyari siyo kodi ya lazima. Wapo ambao watagoma kuilipa kwa kuacha kutumia mitandao ya simu na hakuna mtakacho wafanya!

NB: mngepata hela nyingi endapo mngeamua kusitisha manunuzi ya magari ya kifahari kwa pesa za wananchi hao hao mnao rudi kuwakamua!
Mmetapeli mengi; sidhani kuwa mna nia njema!
Umefuatilia hii ukaambiwa hakuna unachokizungumza?
 
HIZI HAPA FAIDA ZA TOZO MPYA KWA WATOTO WA MASIKINI WA NCHI

Tupige moyo konde, najua pesa hakuna,najua mzunguko wa pesa hakuna ila tuwaache wenye pesa wasaidie Taifa lao kwa faida ya watoto wetu kesho.

Tuache harakati kwenye maendeleo ya watu, hayupo Mjomba wala shangazi wakutujengea barabara, shule,Zahanati,Hospitali kwaajili yetu na kwaajili ya watoto wetu na watoto wao ila ni sisi wenyewe.

[Hebu angalia faida za tozo kwenye sekta mbili tu za Afya na Elimu]

1. UJENZI WA VYUMBA 10,000 VYA MADARASA

Tunaweza kujenga shule 2,000 za O'level au shule 2,500 za A'level au Shule 1,428 za kidato cha ( I-VI) au Shule 1,250 za Msingi hii ni sawa na katika kila kata 2 itajengwa shule mpya 1 kwenye kata zote 3,956 au nisawa nakusema katika kila jimbo la uchaguzi kwenye majimbo yote 264 zitajengwa shule mpya 8 za Mama Samia likiwemo Jimbo la kaka yangu, "Thadei Ole Mushi " Nakwarejea tu,Tanzania tuna shule 5,330 tu za sekondari,Shule mpya nikaribu nusu ya shule zote za sekondari zilizowahi kujengwa tangu Uhuru,

Nakama tozo hii itaenda mpaka 2025 Mama Samia atajenga shule mpya zinazofikia 10,000 hii ni sawa na kusema karibu kila kijiji kitakuwa na shule mpya ama ya sekondari ama ya msingi kupitia tozo za e-money.

2. UJENZI WA ZAHANATI MPYA 900

Hyt Rais Magufuli kwa miaka mitano alijenga Zahanati 1,198.Leo Mama Samia kwa kutumia Tozo ya Uzalendo atajenga Zahanati mpya 900 kwa mwaka 1 wa fedha|FY 2021/22.Hii ni sawa na Zahanati mpya 4,500 kwa miaka 5 yaani kila Jimbo zitajengwa Zahati mpya 4 katika kila mwaka wa fedha ni sawa na Zahanati 20 kwa miaka 5 ya kwanza ya Mhe Samia Suluhu na hii ni kwamajimbo yote 264,Kwa lugha rahisi ifikapo 2025 kila kata itakuwa na Zahanati Mpya 2 za Mama Samia,

3. UJENZI WA VITUO 114 VYA AFYA

Hyt Rais Magufuli kwa miaka 5 alikarabati na kujenga jumla ya vituo vya afya 487,Leo Mhe Rais Samia Suluhu kwa kutumia Tozo ya e-money atajenga vituo vipya 114 kwa mwaka 1 sawa na vituo 570 kwa miaka 5 ya awamu ya kwanza,Kwa lugha rahisi mwaka 2025 kila Wilaya itakuwa na Vituo vipya 4 vya afya vya Mama Samia vitakavyohudumia watoto wa masikini

Itaendelea, kazi iendelee...

C&P
Tozo kwa ajili ya kulipana posho, kuua upinzani, kuwafanya watz wawe masikini zaidi. Kuiba na kufanya ufisadi, kuvuruga uchaguzi,

Hatutumii miamala si mnasemaga hii nchi tajiri, tafuta vyanzo kwenye madini, na gesi
 
Nadhani hii thread ingefutwa tu sababu hata tozo zenyewe zimefutwa. Huu upupu hauna ishu
 
Pia uzalengo huo uwahusu wao waanze kukatwa kodi kila mbunge akatwe kodi serikali itakusanya zaidi ya milion 500 kila mwezi ambazo zitasaidia maendeleo.

Uzalendo gani ambao una mipaka kwa hao wanawahamasisha wenzao wakatwe kodi kwanini wao hawataki kukatwa.
Mama akigusa wabunge tu kwenye hili afwile!
 
Back
Top Bottom