Tozo za Miamala: Dkt. Mwigulu, una hakika Watanzania wanakusoma?

kovai tamil taiga

JF-Expert Member
Sep 28, 2013
1,041
1,425
Mh Rais Mama Samia Suluhu Hassan alitoa Homework Juu ya Tozo la Miamala Wewe na Timu yako Mnaohusika mliangalie Upya Suala hili, sio Kufuta bali kupunguza Makali Ya Tozo.

Badala yake Kwa Kudemka Kabisa unakuja na mahesabu ya Mabilioni Yaliyokusanywa, Kwamba Yamepelekwa kusaidia hiki na Kile.

WaTz hawana shida na Matumizi ya hayo Mabilioni. Ila Wanajiuliza ile Homework Ya Mama Viiipi?
 
Wapinzani wanapewa Kete Ya Nguvu hapa lakini hawaioni. Chama kinaenda kuwekwa Rehani. Hili linamuathiri moja Kwa moja mlalahoi .
 
Anafikiri akileta hiyo ripoti fake ata impress watu wakae kimya the guy is so senseless.
 
Natamani Watanzania tuamue kwa pamoja, na kwa kutumia njia yoyote ile! Tuiondoe ccm madarakani.

Hii serikali tukiiendekeza, itatuzeesha mapema hata kabla ya wakati wetu sahihi. Tozo, tozo, tozo! Everywhere tozo! Tozo!!
 
Mawakala na makampuni Ya simu Wako kwenye kilio biashara Ya miamala Imeshuka lakini Dkt.Mwigulu yeye Kicheko mpaka gego la Mwisho mshiko bila Jasho...!!
 
Mimi nilikuwa nashauri jambo moja la kipuuzi ila litawasaidia kukusanya tozo kama kweli lengo lao ni kukusanya tozo na si kodi basi watumie nje hii.

Waajiri vijana zaidi ya laki moja au laki mbili kote nchini, wawape mafunzo ya unyang'anyi na uporaji, pia wasisahau kuwafundisha mbio (hii itawasaidia baada ya kupora) vijana hawa wawe wanazunguka kila mkoa kwa makundi na wahakikishe kila mtu watakayekutana naye awape hela hata kama hana afanye juu chini awape.

Au kama wataona kuna mtu anahesabu hela kizembe wamkwapue na wakimbie nazo huku wengine wakiwalinda wale wakwapuaji na moja kwa moja waende benki kudeposit ili mapato ya serikali na taifa yawe maradufu.

Hebu fikiria kwa siku wakiweza kukwapua bil 5 si zitasaidia kwenye pato la taifa.
 
Back
Top Bottom