Tozo za Miamala: Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano (TCRA - CCC) linataka maoni yako

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,582
6,627
Screenshot 2021-07-16 at 20.27.20.png


Wadau, tutiririke hapa au mnaonaje?

Unaweza kusoma maoni ya wengine kupitia hii TAG on JF: tozo za miamala
 
Kuhusu tozo za miamala ya simu mie bado nipo pamoja na mh. Rais kwani amelazimika kutoka na hali halisi aliyoikuta ya mtangulizi wake.

Tuvumilieni na tumpe matumaini na tumkosoe kwa staha kwakuwa yeye Ni binadam hataacha mapungufu ila sio matusi Kama wafavyo wahuni.

Haya mnayoyaona Sasa Ni matokeo ya mwendazake na lilikuwa Jambo la muda tu lazima yangetokea na nahis yangepita hapa.

Mama amekaa muda mchache ila ameleta matumaini makubwa kwa wananchi,tusimbeze badala yake tunpe muda tu hali itaimarika.
 
Kuhusu tozo za miamala ya simu mie bado nipo pamoja na mh. Raisi kwan amelazimika kutoka na hali halis aliyoikuta ya mtanguliz wake...
"Hizi gharama mpya za mitandao ni dalili kuwa hatujuani hali zetu. Hayo makato sio mzigo kwa wenye uwezo bali kwa "wanyonge" ni mzigo mzito. Hakika matajiri na mali zao na maskini na watoto wao."- Dr. Stephen Munga

Tatizo sio kutolipa kodi tatizo kodi haziangalii hali za watu as if wote tunalipwa 12m kama wabunge.

Kodi zije kulingana na kipato cha mtu na huo unyonyaji kisa wao wana vipato vikubwa. Kwa wasifikiri kupunguza matumizi ya serikali kwanza?
 
"Hizi gharama mpya za mitandao ni dalili kuwa hatujuani hali zetu. Hayo makato sio mzigo kwa wenye uwezo bali kwa "wanyonge" ni mzigo mzito. Hakika matajiri na mali zao na maskini na watoto wao."- Dr. Stephen Munga...
Ndo dunia hii
 
Umeongea vizuri lakini umesahau kuwa Tanzania ni nchi ambayo imejaaliwa rasilimali za kutosha kiasi kwamba kama viongozi wangeumiza vichwa wangeweza kuja na njia nyingine za kuongeza mapato ya kodi. Kukomaa na tozo kweny miamala ya simu ni kuwa wavivu wa kufikiri na kubuni vyanzo mbadala vya kodi.
 
Unawekaje tozo ya shilingi 7,250/= kwenye mwamala wa elf 50......kimsingi kwa pesa ndogo kama hiyo jumla ya tozo haitakiwi kuzidi 700.....

Hii inaashiria serikali imekaukiwa vyanzo vya mapato kuendesha bajeti yake ambayo imelemewa na mzigo wa kulipa mishahara na posho nene nene kwa wateuliwa hasa ma-DC na ma-RC na kugharamia mashangingi yao, bila kusahau kutumia bajeti kubwa kuwalipa wagonga meza ambao hawajachaguliwa na wananchi kwenye uchaguzi huru, hivyo kukosa tija yoyote kwenye kuwakilisha wananchi.

Yaani serikali inafanya matumizi ya anasa kuwazidi hata matajiri. Hivi kuna manufaa gani kumpa DC au RC vii eite, kwani wana value gani kiasi kwamba hawastahili kutumia landrover, land cruiser hardtop au hata corolla ambazo hata wafanyabiashara wanaweza kuwachangia mafuta wanapokuwa na ziara za kwenda kukagua miradi na kuhamasisha maendeleo...

Badala ya kuwalipa wataalamu na kuwabana walete majibu ya changamoto za wananchi mnatumia pesa nyingi zaidi kuwalipa wateule, wanasiasa na viongozi na kugharamia magari yao ya anasa.....hivi mbali na awamu ya Nyerere nchi hii imewahi kuwa na viongozi serious tena? au ni mwendo wa kuchumia matumbo yao tu.....
 
Kuhusu tozo za miamala ya simu mie bado nipo pamoja na mh. Raisi kwan amelazimika kutoka na hali halis aliyoikuta ya mtanguliz wake.

Tuvumilieni na tumpe matumaini na tumkosoe kwa staha kwakuwa yeye Ni binadam hataacha mapungufu ila sio matusi Kama wafavyo wahuni...
Nadhani na ww upo kwenye safari moja na mwendazake
 
Unawekaje tozo ya shilingi 7,250/= kwenye mwamala wa elf 50......kimsingi kwa pesa ndogo kama hiyo jumla ya tozo haitakiwi kuzidi 700.....

Hii inaashiria serikali imekaukiwa vyanzo vya mapato kuendesha bajeti yake ambayo imelemewa na mzigo wa kulipa mishahara na posho nene nene kwa wateuliwa hasa ma-DC na ma-RC na kugharamia mashangingi yao...
Yaan we unarudia walishasema wameishiwa na wamebun chanzo kipya
 
Back
Top Bottom