Tozo za Madini Ujenzi, Muendelezo wa Unyonyaji kwa Wanyonge.

Opportunity Cost

JF-Expert Member
Dec 10, 2020
9,035
6,907
Nawasalimu kwa jina la JMT

Kama mada inavyosomeka hapo juu.Kusema ukweli inasikitisha kuona kwamba bado serikali inazidi kuongeza uritiri wa kodi za kuzidi kuwakandamiza watu wa chini almaarufu wanyonge.

Pamoja na kuwa nchi hii ina madini ya kila aina lakini serikali imeamua kuanzisha kitu kinaitwa tozo ya Madini ya ujenzi yaani kokoto,mchana,kifusi,matofari na udongo.

Materials hayo ni malighafi za kawaida zinazotumiwa na watu wa kawaida kwenye ujenzi wa vibanda vyao.Kama uko mjini ukiagiza tipa ya materials hayo utatozwa sh.5,000-10,000 kutegeana na ujazo,hiyo ni nje ya tozo za Halmashauri.

Sasa nyie serikali huwa mnawaza nini kumuongezea gharama na ugumu wa maisha kwa watu ambao tayari ni maskini? Mbona Nchi hii ina madini ya maana kila kona? Wakandarasi wao wakipewa Kazi kuna items za tozo na kununua materials lakini mwenzangu na mimi hakuna anaekujali.

Kama ni lazima basi tozeni kwa hao wakandarasi na watu wengine wanaofanya biashara lakini sio kutuongezea mzigo sisi walaji wa mwisho.Hiyo tozo halipi mwenye tipper mendel bali mimi consumer wa mwisho maana wao wanaongeza tuu gharama ya materials.

Hii tozo sio sawa unaumiza mtu wa chini ,tunaomba serikali iifute sio kubadili magoli kama mnajali watu wenu
 
Back
Top Bottom