Tozo ya Tsh. 100 hadi 200 kila siku kwenye line za simu: Mitandao ya simu isitishe uuzwaji wa Vocha

Mr Q

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
15,999
33,024
Kwanini nasema hivyo? Kwa sababu hakuna mtu ataenda kununua vocha ya Tsh. 1000 dukani wakati anajua kabisa atakatwa kiasi cha Tsh. 100 au zaidi wakati huohuo hakuna kifurushi cha sh 900.

Hayo yanajiri katika marekebisho ya sheria kama kiambatanisho hapa chini kitakavyo onesha.

Majibu ya wadau

Screenshot_20210610-235516.png
 
Wanaimplement vipi?? Nisipoweka vocha wk mwezi?

Hivi hawa waheshimiwa wasio na heshima kwa wananchi kwanini wasije na kipengele cha wabunge wote kukatwa kodi kwenye mishahara ili kuchangia pato la taifa?

Kwanini wasije na sheria ya dharula, wabunge kupunguzwa mishahara kusaidia madeni makubwa ya serikali?

Hutowasikia covid-19 wala wagonga meza wakija na mawazo haya wao daily kuwazia jinsi ya kumnyonga mtanzania.

Nitatumia simu wkend tu.

Nitakuwa mzalendo nitumie S.L.P barua zangu zipitie huko.

Everyday is Saturday............................... :cool:
 
Kwanini nasema hivyo? Kwa sababu hakuna mtu ataenda kununua vocha ya sh 1000 dukani wakati anajua kabisa atakatwa kiasi cha sh 100 au zaidi wakati huohuo hakuna kifurushi cha sh 900.

Hayo yanajiri ktk marekebisho ya sheria kama kiambatanisho hapa chini kitakavyo onesha.
Kwani serikali hawana njia nyingine ya kuongeza mapato? Punguzeni marupurupu ya vigogo wa serikali kuanzia wabunge. Simpo.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom