Tozo ni nini? Je, kuna ubunifu wowote katika kuanzisha tozo?

Kuhusu ubunifu, nadhani hakuna. Kiukweli tozo ziko juu sana. Zishushwe ili zisituumize wananchi wanyonge.
 
Tozo inaweza kukaa kwa sura mbili. Tozo kama adhabu au tozo kama mchango kwa mamlaka kama asante kwa kuwapa fursa ya utafutaji lakini pia kuwapa serikali pesa ya kuendesha shughuli zake .
 
Tena inatakiwa tozo iongezwe iwe nusu kwa nusu,ukitumiwa 50,000/ukatwe 25,000/ huo ndiyo uzalendo na faida ya kuwa na Bunge la kijani.
 
Tozo ni nini na kodi ni nini?

Maana kila muamala nakatwa kodi na tozo, na zote wanasema wanaenda kujenga madaraja vijijini.
Kwanini nakatwa mara 2 na ninachokatwa kinaenda kutumika kufanya jambo moja?
Hapo ndio kwenye msingi wa swali langu.

Maana tozo ingekuwa ni kodi basi wangeongeza tu rate ya vat kwenye miamala.
 
Tozo ni nini na kodi ni nini?

Maana kila muamala nakatwa kodi na tozo, na zote wanasema wanaenda kujenga madaraja vijijini.
Kwanini nakatwa mara 2 na ninachokatwa kinaenda kutumika kufanya jambo moja?
Tangu lini wewe miamala yako ikakatwa kodi??? Kama hujui kitu ni bora uulize pimbi wewe
 
Back
Top Bottom