Tozo na kodi kubwa zinavyoua Uchumi wa Mataifa yanayoendelea

Elizabeth Thomson

New Member
Jul 21, 2021
1
7
Ni wajibu wa kila serikali kuhakikisha wananchi wake wanaishi maisha bora, na ili serikali iwahakikishie wananchi wake maisha bora ni lazima wananchi hao watoe kodi ili serikali ijiendeshe vizuri. Mtu lazima awe anajishuhulisha eidha ameajiriwa au amejiajiri ili aweze kupata kipato cha kujikimu na kulipa kodi kwa serikali yake.

Ni lazima mfumo wa kulipa kodi uendane na hali ya kipato cha mwananchi, ambacho mwananchi hatahisi kukandamizwa akitoa.

Endapo tozo na kodi itakuwa kubwa bila kuangalia kipato cha mwananchi, itamdidimiza kiuchumi na kushindwa kujikimu na hakuna mtu aliye tayari kufanya kazi ambayo inamuingizia hasara kila siku hii itapelekea vitu viwili

1. Aache kufanya hiyo kazi anayoifanya
2. Atafute njia mbadala ya kukwepa kulipa kodi

Mfano mzuri ni baada ya waziri wa fedha na mipango kutangaza tozo mpya kwenye miamala ya simu ambayo ilianza kutumika tarehe 1. 7.2021... tarehe 19. 7. 2021 ilitoka ripoti kwenye gazeti la THE CITIZEN kuwa kufanya mahamisho wa miamala kwa njia ya mitandao ya simu kulishuka ina maana baadhi ya watu walishindwa kumudu gharama na kuamua kutafuta njia mbadala kufikisha miamala hiyo.

maeneo yaliyoathirika zaidi ni vijijini ambako hamna huduma za kibenki hivyo hutumia mitandao ya simu.

Kama kutakuwa na wimbi kubwa la watu wanaotafuta njia za kutokulipa kodi au wanaoacha kufanya kazi uchumi wa nchi utayumba kwa sababu serikali bado itatakiwa iwahudumie watu wake lakini pato litakuwa kidogo hivyo badala ya nchi kuendelea mbele ndiyo hali itakuwa mbaya zaidi.

Kwa hiyo serikali iangalie ni kwa namna gani tozo na kodi zitakuwa rafiki kwa mwananchi ili ihamasishe watu wengi kufanya kazi na kuweza kumudu kulipa kodi.. hata wawekezaji itakuwa rahisi kwao kuwekeza katika nchi na hii itachochea maendeleo chanya katika nchi. Asante.
 
Back
Top Bottom