Tozo mpya kwenye simu zitaua soko kwenye kampuni za simu

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
14,658
2,000
Habari za kusikitisha sana ni kuwa zile tozo kubwa Sana za simu zilizopitishwa kwenye bajeti na Bunge letu, zilizotangazwa na waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, zinaanza kutumika rasmi leo na kuwaumiza sana wananchi wanyonge wa nchi hii

Kwa hakika ni kilio kikubwa kwa mamilioni ya wananchi wanyonge ambao walikuwa wameona makampuni ya simu yamewaletea afueni katika kutumiana miamala ya simu.

Ni jambo linaloshangaza kuona vile wabunge wa CCM waliamua kuipitisha bajeti hiyo ya uonevu mkubwa kwa asilimia 100!

Ndipo hapo Taifa hili linapoona umuhimu wa hali ya juu kuwa na Katiba mpya ya nchi, ambapo wananchi wenyewe ndiyo tutakaokuwa na kauli ya namna ya kuiendesha Nchi hii badala ya mfumo wa sasa ambapo Chama cha Mapinduzi (CCM) ndicho kinachoamini kuwa kina hati miliki ya kutawala nchi hii na kutuona wananchi tuliobakia kukubaliana na maamuzi yanayofanywa na chama hicho cha CCM
 

Mokaze

JF-Expert Member
Aug 3, 2018
9,963
2,000
Wamebuni miradi mikubwa wao wenyewe na hawajui wangepata pesa kutoka wapi, njia walioiona ni kupora fedha zetu kwa nguvu.
 

KikulachoChako

JF-Expert Member
Jul 21, 2013
16,361
2,000
Unategemea jema gani kutoka kwenye uzao wa wezi na wanyang'ang'i?

Hizi ni moja ya alama kuu kuwa CCM wamelewa madaraka na hawajali tena maumivu na machungu ya makali ya maisha wanayopitia wananchi kwa kuwa wanajua wao sio chaguo la wananchi.

Lakini machungu na maumivu haya iwe ukumbusho kwa wananchi kuwa taifa hili kwa hapa ilipofikia tunahitaji mabadiliko ya kikatiba. Katiba ndio sheria mama na italeta msawazo wa madaraka na uwajibikaji wa viongozi kwa wananchi na kuondokana na maamuzi ya kifedhuli kama haya wakijua kwamba siku moja watawajibika kwa maamuzi yao.

Maamuzi haya yanamuweka Rais Samia kwenye kundi la watawala wanafiki wanaongea na kinyume na matendo yao.

Nimkumbushe Samia kuwa uchumi endelevu wa nchi haujengwi kwa kuwakandamiza wananchi kwa mzigo mkubwa kodi huku ukiwaacha wachache wakineemeka bali kwa utawala bora na kuboresha nyanja na sekta za kiuchumi ili wananchi wafurahie matunda ya jasho lao.
 

Bukyanagandi

JF-Expert Member
Jun 24, 2009
9,087
2,000
Wamebuni miradi mikubwa wao wenyewe na hawajui wangepata pesa kutoka wapi, njia walioiona ni kupora fedha zetu kwa nguvu.
Wanapo sema wafanya biashara wakubwa wasifatiliwe fatiliwe sana, walipe kodi kadri watavyo jisikia!! Hapo unategemea nini?

Serikali ikifanya makosa ya kuwapa leeway Wafanya biashara ni wazi makusanyo ya kodi yatapungua exponentially - wala hili haliitaji shahada ya sayansi ya roketi kulitabuwa - hata huko Merikani na Ulaya wafanya biashara wakubwa ufatiliwa fatiliwa na mamlaka kwa karibu sana - hakuna cha win win situation wala nini sijui, Serikali hisipo kuwa tough itaishia kukusanya kodi stahiki (ambayo ni halali) kutoka kwa wafanyakazi Serikalini na mashirika ya UMMA kwa kupitia P.A.Y.E so rahisi kukwepa hilo.

Serikali za wenzetu huko Merikani na Ulaya hawafanyi utani linapokuja suala la ukusanyaji kodi, hata Rais mstaafu wa Merikani bwana Trump wanataka kumburuza mahakamani akishtakiwa kukwepa kodi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom