Tozo kwenye mafuta zimepunguzwa, ila bei imepanda. Kuna sehemu tunakosea?

Mh. Rais amepunguza tozo kwenye mafuta, na wote tumesifu hili suala maana bei ya mafuta ukubwa wake unatokana na tozo na Kodi mbalimbali.

Lengo la kufuta baadhi ya tozo ni kumpunguzia mwananchi mzigo mkubwa. Cha kushangaza baada ya hizo tozo kupunguzwa mafuta yamepanda bei leo.

Hapa ndio bado najiuliza Kuna sehemu tunakosea? Tulitegemea mafuta yangeshuka zaidi kutokana na baadhi ya tozo kufutwa.
Ukiangalia ukiwa kichwa chini miguu huko unakodhani juu, utaona bei imeshuka
 
Hilo suala ndio uongo huwa unaanzia hapo, mwezi uliopita Bei kwenye soko la dunia ilipanda na hapa kwetu ikapanda pia, Ila kesho yake Ewura wakasema wanashusha Bei.
Hapo ndio utapochaganyikiwa zaidi.pia unahisi walivyosema wanaondoa tozo ili kushusha Bei hawajui kuwa Bei ya dunia huwa inapanda?
Walijua bei ya dunia itapanda tena, hivyo mafuta yangepanda mara dufu. Ingeleta kelele. Wakakutana fasta na kukubaliana kuondoa baadhi ya tozo ili bei mpya isilete lawama kubwa. Wamecheza na akili za watu tu.
 
20210809_145036_temp.jpg
 
Sasa mkuu, hayo marekebisho ndio kwanza leo yamechapishwa kwenye gazeti la serikali, na kuna baadhi ya sheria lazima zikabadirishwe bungeni leo tu unataka kuona mabadiriko?hata hivyo huo mzigo wa mafuta ulioingia lazima tozo zote hizo zimo, .kama kweli wana nia ya dhati kutakuwepo na mabadiriko fulani ya bei za mafuta nchi, kwani kuna tozo nyingine, za ajabu eti tozo ya TRA, ya kuchakata data!!tozo ya EWURA, ya kupima kina cha mafuta kwenye meli!!ndii maana tulikuwa miaka yote tunaulizana inakuwaje, MALAWI, DRC, ZAMBIA, mafuta yao yanapita hapa lakini kule kwao bei inakuwa chini zaidi kuliko hapa?!!wakiulizwa wanakimbilia ohooo soko la dunia mafuta yamepanda, kwani hao wengine wanayachukulia soko la angani??hii nchi na wanachi wake ni wakuhurumiwa tu!!
Unahisi tozo zingepanda hii bei ingesubiri mchakato unaosema mkuu au inepanda leo leo?
 
Wakati mwingine muwe mnapitia global issues kwenye mitandao.

Bei ya mafuta imepanda duniani kote, angalia marekani wanalalamika pia uingereza hizi no baadhi ya nchi kubwa .

Mafuta yamepunguzwa tozo Ila bado bei imeongezeka tena kwenye global market, hapo Ina maana isingetolewa hizo tozo nadhani ingepanda maradufu ya hiyo unayoiona hapo.

Ni vema kuwa conversant na global issues ili kuondokana na uwezekano wa kuongea Mambo yanayoweza kujionyesha haupo serious.
Nadhani wapo watu huwa hawatafuti usahihi au sababu ya tukio. Wanatafuta jambo la kulaumu serikali. Wakishapata ni kulaumu tu haijalishi uhalisia ni nn.
 
Unahisi tozo zingepanda hii bei ingesubiri mchakato unaosema mkuu au inepanda leo leo?
Mkuu hii nchi tuiache tu, mala unaambiwa eti ktk bei ya leo ilivyopanda tayari hizo tozo zimeshapunguzwa humo!!!eti bila hizo tozo leo dar tungenunua mafuta kwa karibia 2600!!
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom