Wananchi wametoa malalamiko yao kwa Serikali lakini bado kimya, watu wengi wameacha biashara ya miamala ya simu na hii inapelekea familia zao kupata shida, hata malengo ya Serikali yaliyotarajiwa hayatafikiwa kwa sababu watu wengi wameacha kutumia huduma hii. Mfano mimi leo nimetuma Tshs.1m/= nimekatwa Tshs.16,000 na yule niliyemtumia nikaelezwa atakatwa Tshs.14,000. Shillingi 30,000 ni fedha nyingi sana.
Kwa matumizi ya kawaida ni kilo 10 ya sukari au nyama kilo 5, nusu gunia la mahindi, mchele kilo 20 n.k. Kutokana na tozo hii ya miamala kama itazidi kuendelea itakuja kuigharimu Serikali ya CCM kwa sababu itapelekea wananchi kutokuwa na imani na Serikali yao. Mhe. Rais chukua hatua za haraka kuhusiana na tozo hii ya miamala.. Sisi ndo tunakaa huku mitaani wananchi hawana raha kabisa.