GUSSIE
JF-Expert Member
- Dec 2, 2014
- 3,866
- 11,099
Wanabodi kuna vitu ni luxiory na vingine Necessity. Luxiory kwako yaweza kikawa necessity kwa mtu mwingine na hivyo hivyo necessity kwako yaweza ikawa luxiory kwa mtu mwingine.
Kitu au mahitaji kuwa muhimu au sio muhimu inategemea na chaguo la mtu husika
"Serikali iache kutoza bia kila mwaka". Huu ndio usemi ulikuwa wa watanzania serikali itafute vyanzo mbadala vya mapato kwa miaka zaidi ya thelathini( 30).Kutegemea kodi kwenye Bia ni aibu kubwa kwa imani ya baadhi ya watu hapa JF na kwa afya za watanzania bia hazifai zina Madhara mengi kiafya( Viongozi wa afya na dini walihimiza na wanahimiza bia hazifai Tuache)
Maombi yamekubalika, Wanywa bia na watoa ofa walipungua sana enzi za JPM watu waliishia kunywa bia za "Serengeti lite na Castle lite " bei yake imedumu kwa TZS 1,500 kwa miaka mitano ni bei chini ya dola moja za kimarekani, Makampuni ya bia Haya kutengeneza faida kubwa kama watu tulivyozoea kwa miaka mitano
Output ya bia iliyozalishwa *TZS 1500*Idadi ya walevi =Revenue Generated
Kama idadi ya walevi ni Zero hivyo Revenue ni Zero
Bunge la chama kimoja cha ccm wameamua kuwapa watanzania mbadala wa kodi ili Taifa lisonge mbele kwa manufaa, Ni kodi ya hiari kabisa
Una hiari ya kuacha kununua umeme ili kukwepa kodi ya elfu moja TZS 1,000 kwa mwezi, ukaamua kulala giza.
Una hiari ya kuacha kutuma au kutoa pesa kwenye wallet za simu Tigo pesa, M Pesa au Airtel Money. U kaamua kukaa na pesa ndani
Nimeandika hii mada baada ya kutembelea rafiki zangu wakiwa Bar wanaangalia mpira na kukuta mjadala huu kuwa mbona watanzania wanakuwa wagumu kuchangia Taifa Lao wakati wao wameamua kupunguza matumizi ya pombe kwa afya zao
Kutegemea kodi ya pombe huku wale vi wakipungua kwa mahubiri mazuri na wakovu Hakika Taifa litaangamia
Hakuna njia mbadala ya kupata mapato kwa sasa kwa mujibu wa Spika Ndugai, Na amehoji mwenye njia mbadala ya kupata mapato atoe maoni yake ( Spika Ndugai)
Njia tulizisoma darasani zote tumezitumia kama :
kukopa (loans) serikali imekopa mpaka watu wanatukana kwanini tunakopa sana,
Kodi( Taxation) Serikali imetoza kodi mpaka ikaambiwa inabambikia watu kodi
Misaada(Grants) Serikali imepokea na kuwekewa masharti kibao mpaka watu Wakasema ni aibu kuwategemea mabeberu
Mwisho, Serikali imeleta Tozo (Government levy) bado watu Wanalalamika, Tujadili vyanzo vya mapato kulisaidia Taifa.
Sent using Jamii Forums mobile app