Tozo hizi za awamu ya sita hazina tofauti na tozo za Bodi ya Mikopo zilizoongezwa karibu mara mbili enzi za Magufuli

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,014
144,371
Jamani tuache unafiki wa kusema eti tutamkubuka Magufuli kutokona na tozo hizi za awamu ya sita kwani huu ni muendelezo tu wa sera za CCM kukamua wananchi bila huruma.

Wote ni mashahid wa makato katili ya Bodi ya Mikopo wakati wa utawala wa Magufuli ambapo makato yaliongezwa kutoka asilimia 8 mpaka kufikia asilimia 15 huku mishahara ikiwa ni ile ile na baadhi ya watu walipongeza huku wakiwakejeli waliokuwa wanalalamika makato yale kwa maneno kama vile dawa ya deni ni kulipa, n.k.

Sasa kwakuwa hili la hizo tozo za Mama Samia zinagusa karibu kila mtu, ndio maana tunaona kelele nyingi kutoka hata kwa wale waliokuwa wakikejeli malalamiko ya makato ya Bodi ya Mikopo plus malalamiko ya retention fee wanasahau waliunga mkono makato yale katili.

Mimi nasema wacha tuendelee kukamuliwa mpaka siku tutapoona umuhimu wa kuungana kama watanzania kupinga watawala kama inavyotokea katika nchi za wenzetu.

Baadhi yetu walizana wako salama wakasahau hakuna alies salama katika tawala za aina hii.

Mama kanyaga twende mpaka tutie akili

Watu wakida katiba mpya, mnaona wanatafuta madaraka, sasa kaeni kimya na mlipe hizo tozo.

Kumbukeni, katiba hii iliyotuletea Bunge hili lisilo na uhalali, ndio inatoa mamlaka na uhalali wa Raisi kulivunja Bunge endapo litakaa kupitisha Bajeti ya Serikali.

Tuendelee kuona kazi ya kudai katiba mpya ni ya CHADEMA tu kwasababu wanatafuta madaraka na wala sisi tusio wanasiasa haituhusu.

Tunavuna tulichopanda kama Taifa kwa miaka mingi, hivyo tuwe wapole maana sisi ni nchi ya amani.
 
Slogan ya HAPA KAZI TU inaendelezwa kwa "KAZI IENDELEE".....

Unaendeleza miradi ya KIMKAKATI iliyoasisiwa na serikali ya awamu ya 5...
(SGR ,BWAWA LA KUFUA UMEME MWALIMU NYERERE ,UJENZI WA VYELEZO ,MELI n.k)

Unawaajiri vijana zaidi ya 8000 (ambao huko nyuma haikufanyika hivyo kwa haraka)......

Unapandisha madaraja watumishi wa UMMA......

Unafuta TOZO YA 6% RETENTION FEE.......

Unawakumbusha TRA kutotumia nguvu iliyopitiliza katika kukusanya Kodi......

YOTE HAYO UNAYAFANYAJE BILA YA KUBUNI VYAO VIPYA VYA MAPATO NA TOZO ?!!!!

MAENDELEO YATATOKA MAWINGUNI KAMA MAJI YA MVUA?!!!!!

#TozoHiiNiSahihi
#TulipeKodiYaMajengo
#NchiKwanza
#SiempreJMT
#SiempreSSH
 
Yote haya ni matokeo ya kuwa na mamiradi makubwa kuliko uwezo wa nchi na Magu ndio wa kulaumiwa zaidi.
 
Back
Top Bottom