Toyota Wish Vs Isis

Kashi

JF-Expert Member
Jan 6, 2013
897
741
Wakuu naombeni ushauri, niko mbioni kufanya mchakato wa kupata usafiri. Mimi ni mpenzi wa MPV (Mult Purpose Vehicles) au kwa lugha nyingine Family Cars. Nimependezwa na hizo mbili kwa sababu zote ni 7 seaters na pia injini chini ya 2.0 L. Wadau mnaotumia hizi gari msaada wenu ni muhimu sana ili nifanye maamuzi sahihi. Napenda kufahamu zaidi kuhusu uimara na upatikanaji wa spare parts zake.
 
Muhimu kuzingatia wapi unaishi na njia zake zikoje, muhimu sana. Hizo gari zote ni laini sana, sidhani kama mjapani alizitengeneza kwa ajili ya shuruba.

Wish nyingi ninazoona njiani zinachoka haraka, zimepigwa "ribiti" za kufa mtu.
 
Asante mkuu kwa ushauri, vp kuhusu Ipsum 2.4L japp hapa najua matumizi ya mafuta itakuwa shughuli.
 
Asante sana kwa ushauri mkuu.
Kweli asee... hizi wish zinahitaji kudekezwa sana... yani lami kwa lami. Rough roads inatepeta balaa. Jamaa yangu kaichukua show room haina hata mwaka lakini inasikitisha sana... Kama huna ubishoo kama anko wangu kamata mchuma unaitwa probox ... inafanya kazi kama pickup na daladala...
 
Nashukuru Asprin kwa ushauri, hiyo Isis nayo ni vilevile?
 
IMG_20180325_185737_921.JPG
 
Ipsum ni gari nzuri kuliko Wish kwa upande wangu japo kuwa Ipsum inatumia mafuta zaidi ya Wish. Kwa upande wa ukubwa wa injini siyo shida kwa gari zote mbili kwani ni vvti ingini kwa hiyo kinachobaki ni uendeshaji wako tu ndiyo utaelekeza ulaji wa mafuta utakayotumia japo kwa uzoefu wangu mdogo ipsum inaenda wastani wa 10km/1L ila upande wa Wish sifahamu. Pia Ipsum ina balance sana inapokua unaiendesha kwa speed kubwa. Body ya Ipsum ni imara kuzidi Wish. Pia upande wa muonekano Ipsum ipo vizuri kuliko Wish
 
Asante sana kwa ushauri wako mkuu.
 
Kama humaindi shep na sura chukua pro box/suceed. Ile ni mbadala wa pickup
Hii gari ni imara sana, sema tu shep kama ulivyosema.Harafu kipaumbele changu ni gari yenye siti nyingi.
 
Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom