Toyota Raum Review: Karibu tupeane uzoefu kuhusu gari hili

RugambwaYT

JF-Expert Member
Jan 11, 2014
1,278
2,000

Toyota Raum ni gari dogo lililotengenezwa na kampuni ya Toyota na kuuzwa kwenye soko la ndani la Japan (JDM) kuanzia mwaka 1997 mpaka mwaka 2011 ambapo uzalishaji wake ulisitishwa rasmi. Gari hili liko kwenye kundi la magari madogo kwa ajili ya matumizi mbali mbali yajulikanayo kitaalamu kama Mini Multi-Purpose Vehicle (Mini MPV).

Muundo wa gari hili ulijipatia umaarufu saana kwenye soko la Japan kutokana na kuwa na nafasi ya kubwa ndani huku nje likiwa na muonekano mdogo ambau unarahisisha uendeshaji hasa kwenye mjini ya Japan yenye msongamano mkubwa wa magari.

Kwenye uzi huu tutajikita zaidi kwenye generation ya pili (2nd Gen) ya gari hili ambayo ilianza kuzalishwa mwaka 2003 mpaka mwaka wa mwisho wa uzalishaji wake.

20200305_223418.jpg
Matoleo ya 2nd Gen Raum
2nd Gen Raum ina matoleo makubwa mawili. Front-Wheel-Drive na All-Wheel-Drive (hizo AWD ni chache sana kwenye used market). Kimuonekano Raum haijabadilika saana tangu ilipotoka. Japo mwaka 2006 kulikuwa na mabadiliko kidogo kwenye design (facelif) hasa fog lights za mbele na ile taa kubwa ya nyuma. Kuna toleo moja lilitengenezwa maalumu kwa ajili ya kusaidia kubeba watu wenye ulemavu ambapo siti ya mbele au ya nyuma ya abiria huweza kutoka nje na kuwarahisishia kupanda au kushuka kwenye gari.

Engine na Gearbox
2nd Gen Raum inatumia moja kati ya engines maarufu kwa magari madogo ya Toyota kipindi hicho aina ya 1NZ-FE. Engine hii cylinder 4, ina cc 1496 (1.5l) na ina mfumo wa VVTi ili kuifanya itumie mafuta vizuri. Kama utakumbuka, engine hii imetumika pia kwenye magari kama Sienta, Premio, Allion, Probox, Ractis, Porte, Belta, Platz, Vitz n.k. So ni very common. Kwa upande wa gearbox, Raum ina gearbox ya automatic yenye gia nne (4 speed automatic) ambayo pamoja na engine inafanya utumiaji wa mafuta wa Raum kufikia wastani wa 10-12km kwa lita mjini na 15-17km kwa lita ukiwa highway kutegemeana na uendeshaji wako.
20200305_223515.jpg
The goods
  • Raum very reliable kiasi kwamba Toyota waliamua kulitengeneza kwa miaka karibu 10 bila mabadiliko yoyote makubwa. Maana jamaa wanasema, if it ain’t broke, don’t fix it. So unaweza litumia kwa mjini na hata safari za mbali bila mawazo kabisa.
  • Nafasi ya kutosha ndani kulinganisha na magari mengi madogo. Watu watano wanaweza kukaa vizuri kwa safari ndefu. It is comfortable enough for its size and price. Pia dereva anaweza kutoka kwenye siti yake ya mbele mpaka siti ya nyuma kwa urahisi bila kushuka kwenye gari.
  • Mfumo wake wa rear sliding doors kwa upande wa abiria na dereva unawezesha abiria wa size tofauti kuingia na kutoka kirahisi kwenye gari. Siti ya mbele ya abiria inaweza kukunjwa kwa mbele na kuacha nafasi kubwa zaidi kwa abiria na mizigo.
  • Low maintenance cost, vile utumiaji wake wa mafuta naoweza sema kuwa ni relatively good kwa aina ya gari hili. Pia engine yake imetumika kwa magari mengi saana, so spare zinapatikana kirahisi. Vile vile Raum inashare parts nyingi na magari mengi madogo ya Toyota.
  • Muonekano wake ni wa kisasa, linafaa kwa matumizi binafsi na biashara pia. Linapendwa na jinsia zote, japo kina dada wanalipenda zaidi, sijui kwa nini? Wenda ni vile wanapenda kusafiri na kundi la watu.
1583438119192.png
The bads
  • Power sliding door mechanism ya upande wa abiria huwa inaharibika mapema, hasa pale jamaa wanapotumia nguvu kufungua badala ya kuacha mlango ufunguke wenyewe.
  • Only room for 5, wakati Spacio ambayo iko kwenye class moja na Raum inaweza kubeba watu 7.
  • Kwa kweli, zaidi ya tank dogo la mafuta, na muungurumo wa 1NZ, hakuna mengi ya kulalamika kuhusu gari hili.
Cha kuzingatia unaponunua gari hili
Tafuta Lenye options nyingi hasa la kuanzia mwaka 2006, utalifaidi zaidi. Liwe na fog lighs, alloy wheels, ukipata ile yenye siti ya abiria ya umeme ni bora zaidi. Suspension system yake iko vizuri kwa kiasi kikubwa, shock absorber ni soft, japo mara nyingi bushes zinakuwa na zimekwish vile ni gari la siku nyingi. Hakikisha power sliding door mechanism inafanya kazi, otherwise utajikuta unakuwa konda wa daladala.

Maoni yangu
Kama unapenda mwonekano wake wa nje wa Raumu, hunatatizo na gearlever iliyokaa kwenye dashboard, na instrument cluster (speed-o-meter) ya katikati ambayo inaruhusu abiria wote kuona taa ikiwaka pindi umeishiwa mafuta, then 2nd Gen Toyota Raum ni gari zuri saana. Hasa wa matumizi ya familia kwenye mizunguko ya mjini. Go for it.

Picha zaidi
20200305_223324.jpg

1583438411136.png

20200305_224008.jpg20200305_223418.jpg
20200305_223515.jpg
1583438119192.png
20200305_223515.jpg
20200305_223324.jpg
1583438411136.png
1583438472483.png
1583438500489.png
20200305_224008.jpg
 

pureView Zeiss

JF-Expert Member
Sep 5, 2016
5,595
2,000
Asante Sana RugambwaYT Kwa maelezo tako, sikuzote hii gari imekuwa Bora Sana hasa 2nd generation Kwa maisha yetu ya kibongo linafaa sana.

Kwa kuongezea na Mimi "tunashauriwa hasa Kwa watumiaji wa engine za 1NZ ukifikisha milage 150,000 Fanya adjustment ya VALVE na ikiwezekana badilisheni ring piston na VALVE SEAL"
Kwa kufanya hivyo engine itaendelea kudumu Sana
 

RugambwaYT

JF-Expert Member
Jan 11, 2014
1,278
2,000
Asante Sana RugambwaYT Kwa maelezo tako, sikuzote hii gari imekuwa Bora Sana hasa 2nd generation Kwa maisha yetu ya kibongo linafaa sana.

Kwa kuongezea na Mimi "tunashauriwa hasa Kwa watumiaji wa engine za 1NZ ukifikisha milage 150,000 Fanya adjustment ya VALVE na ikiwezekana badilisheni ring piston na VALVE SEAL"
Kwa kufanya hivyo engine itaendelea kudumu Sana
Tena vile 1NZ ni engine common saana kwa sasa, nafikiri mafundi wetu wengi wameshapata ujuzi wa jinsi ya kuirepair.
 

wa stendi

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
21,615
2,000
Jamaa yangu analo mke wake anaendaga kulipaki pale nji panda ya cm 2000 anauza net yaani ni gari duka
 

RugambwaYT

JF-Expert Member
Jan 11, 2014
1,278
2,000
Jamaa yangu analo mke wake anaendaga kulipaki pale nji panda ya cm 2000 anauza net yaani ni gari duka
Hehehee! Daa! Wabunifu kweli hao. Maana ukifungua milango yote ya upande wa abiria ukalaza na kiti cha mbele unapata uwazi mkubwa kweli. Safi saana.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom