Toyota Prado T*** BML kitenda ulichofanya si cha kiungwana!

Majoja

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
612
186
Leo asubuhi nimeshuhudia kitenda kisicho cha kiungwana kabisa kilchofanywa na dereva wa gari aina ya Toyota Prado (old model mayai) Rangi dark blue au nyeusi , yenye maadishi PRADO ubavuni.
Gari hili lilikuwa linatanua kwa kuovateki foleni ndefu sana sehemu za Kawe karibu na roundabout.
Polisi aliyekuwepo zamu akakaa mbele kumzuia kwa tabia hii inayokera madereva wengine watiifu.Bila kujali huyu jamaa wa Prado hakupunguza mwendo na kama si kijana yule wa Polisi Traffic kuruka pembeni angemgonga na kumuua.
Hata hivyoalimgonga kiganja na gari kukwapua ile clip file yake iliyoangukia karibu mita 40 mbele.
Yule Polisi akajinyanyua na kujifuta na kuendelea na kazi.
Hiyo gari mimi nilikuwa nyuma yake magari karibu matano nyuma na kufanikiwa kusoma tu namba za mwisho.
Gari likapiata Mlalakuwa, Mikocheni,Cocacola Rd hadi Mwenge.

Pamoja na kutaka kuwahi, tabia hii ya kutojali amri, kutojali maisha ya mtu aliyekazini imenisikitisha, na hii ni licha ya kuwa huyu dereva alikuwa ana makosa.
Ni tabia ya kukera sana.
 
Mi ndo maana siwezi kutembea na silaha....ningewadungua watanuaji tena wale wanaotanua na kujifanya wanahaki!
 
habari hii inanikumbush ajali niliyoipata hivi karibuni.......... na bado najiuguza majeraha.
 
Mi ndo maana siwezi kutembea na silaha....ningewadungua watanuaji tena wale wanaotanua na kujifanya wanahaki!

Dah! kumbe tuna mawazo mamoja... mimi huwa najitahidi sana nikae mbali na chuma. nahisi murder case zinaninyemelea...
 
Lakini nao polisi inabidi watumie akili, unaweza kufa hivi hivi. Unaweza kukuta labda huyo jama alikuwa jambazi sasa yeye haofii kitu kingine chochote. Ustaarabu ni huu, ukisimamisha gari likakataa kutii chukua namba na kulitolea taarifa kwa ili hatua zaidi zichukuliwe halafu uone polisi wapenda rushwa watakavyo kunyonyoa manyoya baada ya kukukamata.
 
Ungemuanika humu ndani tumtukane matusi yote ya nguoni atupeleke polisi tukamnyonyoe manyoya! shenzi type!
 
jiulize kwa nini yule traffic hakusoma namba za gari alijua ni mkubwa ama mtoto wa mkubwa maana wao ndo wanao ongoza kwa kuvunja sheria uckute hata alikuwa riz1
 
Huyo dereva asubiri tu siku yake, atakuja kupatwa na balaa ambalo hatalisahau maishani... what goes around comes around
 
Umeharibu ari yangu ya kufuatilia gari/tukio hilo kwa kutoweka namba za hiyo prado mkuu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom