Toyota landcruser Pickup ina nini mpaka iwe bei kubwa?

Kipindi kile nilisikia kuna jamaa wa madini kule Kilosa alikuwa akienda baa na wapambe anaacha Land Cruiser ikiwa silence wakati wanapiga pombe.

Na kuna muda wapambe wanapewa kreti za bia wanasafisha gari yote kwa kutumia bia tuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Duh ......mambo ya kishamba hayo
Tunduru ndy walikuwa wanafanya hivo zaidi

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kipindi kile nilisikia kuna jamaa wa madini kule Kilosa alikuwa akienda baa na wapambe anaacha Land Cruiser ikiwa silence wakati wanapiga pombe.
Na kuna muda wapambe wanapewa kreti za bia wanasafisha gari yote kwa kutumia bia tuu.
Sent using Jamii Forums mobile app
Duh Offshore Seamen na mrangi mmemikumbusha hako kaMji ka Mjerumani vilima vyake vya madini vitongoji vya Manzese, Magomeni, Mkadage na sasa wameingia waTuruki wakichimba reli Mwendo kas, siisahau Golden Folkya Waziri na vimwana wa Kilosa bila gari ya kazi huendeshi barabara za huko na huvipandi vilima vyake
 
shida ya waswahili baada ya kujibu swali wanaanza mastory mengine jibuni swali watu tujifunze
wewe na mwenzio mtakuwa zao la shule za mtakatifu flani, mpewe majibu hamtaki jisomea.

mbona majibu yako wazi humu ama mnataka wayaandike kama point
 
Cheki moja ya sababu ya bei kubwa...


mm nimeshangaa mnyororo wa kumvutia mbwa ?
bora bomba ningeamini hebu tumieni Principal ya acceleration Mass x velocity
basi hata ng'ombe wangu wa kulimia watalivuta hilo lilori
 
Umeongea point kaka. Inabidi watu waangalie na makampuni mengine sio Toyota tu.
1. Gharama Nafuu

Toyota iliyotumika kidogo Japan ni gharama nafuu zaidi ya Ford kutoka marekani (au hata nchini). Pia, serikali ya Tanzania inawaruhusu wauzaji wenyeji kuingiza magari haya kwa gharama za chini zaidi. Kwa, bei yake ya kununua nayo ni chini kulingana na magari mengine.

2. Hazitumii mafuta mengi

Magari madogo ya Toyota yanajulikana kwa kutotumia mafuta mengi. Hata magari yao makubwa mengine (Prado kwa mfano), hayatumii mafuta mengi kukizilinganisha na magari makubwa ya makampuni mengine. Kwa mji kama Dar es Salaam yeneye foleni nying, hii ni muhimu.

3. Upatikanaji wa spea

Kwa kuwa Toyota ni maarufu sana, spea zake zinapatikana kiurahisi zaidi pia, ambayo inapunguza gharama ya utunzaji.

4. Zina wataalam wengi

Kwa kurudia, Toyota ni maarufu sana Tanzania na hivyo, fundi wengi wa magari wana ujuzi wa magari ya Toyota.

Mtu mwenye gari la Volkswagen Polo, kwa mfano, atapata shida sana kutafuta fundi mzuri na pia, matengenezo yatakuwa ya gharama kubwa zaidi.

5. Kuna aina ya gari kwa wote

Swala la kuchagua gari la kununua ikijitokeza, watu wengi wanafikiria aina za Toyota na sio aina za magari. Toyota ina aina nyingi za magari zinazokidhi mahitaji ya watu mbalimbali. Kwa kifupi, mtu yoyote anaweza akaendesha Toyota.

Labda sisi ndio wenye mchango mkubwa nchini kwa umaarufu wa Toyota

Ukweli ni kwamba watanzania wana amua kununua gari kutokana na mapendekezo ya family au marafiki. Kwa kweli, kwa kuwa Toyota ni maarufu kuliko wengine ni rahisi sana kutafuta gari ya kampuni hiyo tu. Ila, kuna faida ya kuangalia magari ya makampuni mengine pia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Urembo ulioongezwa kwenye hili gari gharama yake unaweza kununua kagari kengine
FB_IMG_15497984073372728.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom