Toyota hizi...!

Mwenyewe unaona Sifaaa...kumbe ushamba wa Gari unakusumbua.
Kila mtu ana starehe yake mkuu, fikiria kuna wanao ona kuwa na mademu ni starehe zao, kuna wanywaji wa pombe ni starehe zao....

Kwangu mim starehe yangu ni kuvunja speed meter... Kifo tumeumbiwa binadamu, gari nimeanza kuendesha nikiwa na miaka 7, na miaka 19 naendesha gari... Enjoy
 
Si kwamba nazikandia hizi gari za kijapan la hasha. Nimewahi kuzimiliki Chaser mayai na balloon GX90. Kila moja imevuma kwa nyakati zake. Zikisifika kwa wepesi mwendo (kuchanganya haraka) kiyoyozi kama Greece land. Zimepita model nyingi.

Tunamalizia enzi za Harrier TAKO LA NYANI zimechuja haraka baada ya nyingi kupiga chini.

TOYOTA crown bado iko juu lakini nayo inaendelea kuchinja watu. Simlaumu mjapani katengeneza kwa matumizi yake na taratibu zake. Huku hatuzingatii hili kabisa

Mwisho tunaishia kulaumu na kusema TOYOTA hizi lakini pamoja na kuwa na viwango vidogo vya usalama kulinganisha na gari za ulaya bado tatizo ni letu sisi wenyewe.

ELIMU JUU YA VYOMBO VYA MOTO hasa gari nyepesi za kijapani tumepoteza damu changa nyingine Kabuku. Damu ya Rchunga... Rip View attachment 1105974View attachment 1105975View attachment 1105976
aisee huyu aliingia chini ya lori ama nini...mbona kapunyuliwa juu tu!!!!?

mbele hapo naona hadi rejeta ipo fresh tu, pole yake.
 
Pole kwa waliofikwa na hayo. Ukiangalia siku hizi madereva wengi wanajua kukanyaga mafuta na break basi. Sheria na alama za barabarani hawazijui, na wanaozijua baadhi hawazifuati kabisa, achilia mbali kujua uwezo wa gari na namna ya kulihandle barabarani ndio shida kubwa zaidi.
leseni zenyewe siku hizi za kupigiwa simu na kwenda kuchukua unategemea hizo sheria na alama za barabarani watazijulia wapi.
 
Ajali ya mtu mwingine haiwezi kunifanya niongope kukanyaga mafuta..... Kesho asubuhi na safari ya Mbeya+Tunduma nikitoka Dar saa kumi na mbili asubuhi nataka saa kumi niwe Tunduma.... Nimesha andaa na hela ya faini kabisa ya matrafiki
kwa huo muda ambao umetoka sidhani kama utafanikisha kufika saa kumi tunduma, haiwezekani.

ungetoka saa nane usiku chief.
 
Back
Top Bottom