Toyota Altezza Gita (Wagon) Thread: Karibuni tujuzane ubora na udhaifu wa gari hizi

RugambwaYT

JF-Expert Member
Jan 11, 2014
1,381
1,850
1608112369055.png

Toyota Altezza Gita
Toyota Altezza Gita (wagon) ni moja kati ya magari mazuri na imara kuwahi kutengenezwa na kampuni ya kutengeneza magari ya Toyota kwa kipindi cha miongo kadhaa iliyopita. Gari hili liliingia sokoni mwaka 2001, miaka mitatu baada ya gari la Altezza (sedan) kupata mafanikio makubwa sokoni tangu lilipoanza kutengezwa mnamo mwaka 1998. Altezza na Altezza Gita ni magari yaliyotengenezwa kupambana na magari ya Ulaya kama BMW 3 series, Mercedes C class na Audi A4, ambayo kiutaalamu huwa yanawekwa kwenye kundi la Entry Level Compact Executive Salon/Wagon.

Kwa soko ya Ulaya na Marekani Altezza na Altezza Gita ziliuzwa kwa jina la Lexus IS, na Lexus IS SportCross.

Toyota_Altezza_Gita_001.JPG

Kuna matoleo matatu ya Altezza Gita kutokana na engine zake. Kuna AS200 yenye cc2000 ambazo ndio nyingi. Hizi zinakuja na engine ya 1G-FE, na AS300 ambayo ina engine ya 2JZ-GE yenye cc3000. Hizo engine zote ni 6 cylinder. Pia kuna models chache za Altezza Gita, RS200 zenye engine ya 3S-GE. Hii ni engine ya 4 cylinder, iliyoundwa kwa ushirikiano kati ya Toyota na Yamaha. Hii ina nguvu (200-210hp) zaidi ya ile 1G-FE, na mara nyingi inakuwa kwenye Altezza salon.

Lexus-IS300-SportCross.jpg

UBORA WA GARI HIZI
  • Gari hili lina muonekano mzuri na usiopitwa na wakati kirahisi (ukizingatia lina umri wa zaidi ya miaka 17). Watu wengi wanashawishika kuliita Altezza new model
  • Lina features nyingi kutoka kiwandani kulinganisha na magari ya Ulaya ya kipindi hicho, hasa ukipata Limited edition (yenye seats za leather) mfano power seats kwa dereva na abiria, 6 disc CD changer, 6 airbags etc. Ukibahatisha kupata model ya Lexus ndio utafurahi zaidi. Lina mpaka seat heaters.
  • Japo ni sports car, ila liko comfortable vya kutosha kwa aina ya gari, hasa kwenye barabara ya lami
  • Vile ni rear wheel drive (linasukuma kwa tairi za nyuma) handling inakuwa safi sana, maana tairi za mbele zinabaki na kazi ya kuliongoza gari tuu. Kiukweli linafurahisha kuendesha, hasa kwenye barabara zenye kona.
  • Hizi gari ni very reliable, yaani ni kati ya magari ambayo kiukweli hayana urafiki saana na garage. Yanavumilia shida saana. It is very well made.
UDHAIFU WA GARI HIZI
  • Linakunywa mafuta zaidi ya magari ya Ulaya ya level moja, kama BMW 3 series (E46) na Mercedes C class (W203).
  • Kwa kuwa ni sport car, suspension zake ni ngumu kiasi, na rims za size 17 ambazo zinakuja na gari, tairi linakuwa na low profile, hivyo haliko comfortable saana kwenye barabara za vumbi (rough roads).
  • Seats za nyuma ni finyu kidogo kwa watu warefu, hasa kama dereva ni mrefu pia.
  • Liko chini saana, hasa kwa barabara zetu za mtaani ambazo mara nyingi haziko kwenye hali nzuri. Hii husababisha watu wengi kuligonga sehemu za chini na kwenye bumper kama wakilitumia bila kuliinua. Na ukiliinua linakuwa bayaa, na linapoteza stability.
  • Radio yake ya CD 6 huwa inaharibika kirahisi huo mfumo wa kubadilisha CD hasa inapotumiwa na watu wasio wazoefu.
MAMBO YA KUZINGATIA UNUNUAPO GARI HII
  • Models zote za tangu 2001 mpaka 2005 hazina tofauti kubwa, sababu gari hilo halikufanyiwa mabadiliko yeyote makubwa ndani ya kipindi hicho, zaidi ya mabadiliko madogo (facelift) mwaka kwa model ya mwaka 2003 ambapo, taa na navigation screen ndio vilibadilishwa na vitu vichache vya ndani.
  • Ukinunua likiwa chini ya km 100,000 hakikisha unamuuliza muuzaji kama alibadilisha timing belt, maana huwa zina kawaida ya kukatika baada ya kufikisha km hizo. Na zikikatika zinaweza kuleta madhara makubwa kwenye engine. Kama ni Japan, hakikisha linabadilishwa huko huko.
  • Usinunue ambalo lina dalili za kuwa modified saana kama hauna lengo la kulitumia kwenye mashindano na kupiga misele (drifting). Maana hizi gari zilipendwa saana na racer boys, walikuwa wanazitumia kwenye mashindano, hivyo zilikuwa abused saana.
  • Manual transmission inafurahisha saana kuendesha. Ina gia sita. Japo kiukweli, hizi nimeziona chache saana. Automatic transmission nazo hazina shida. Kuna za gia nne, na gia tano. Ukiwa na auto, hakikisha unatumia ATF ya Toyoto TIV, kama hauwezi, basi bora usibadilishe kabisa.
  • Engine ya 1G inatabia ya kuvuja oil kwenye Valve cover, hasa kama utajaza engine oil kupita kiasi wakati wa kufanya service. Hakikisha oil ya viscosity ya 5W40 au 10W40, na usizidishe lita 4.1. Mafundi wenge huwa wanashauri kuweka lita 5. Ni makosa ina haribu oil seals. Na usitumie oil filter za elfu 5, nunua genuine ;);).
  • Hizi gari hasa zikiwa na km nyingi, bush za low control arms (lower wishbone) za mbele huwa zinaisha, na kusababisha gari kula tairi upande wa ndani. Usijaribu kufanya wheel alignment ukiona inakula tairi. Hilo sio tatizo la alignment. Tafuta hizo wishbone bushes ubadilishe. Hakikisha unaweka alama kwanza kabla ya kufungua wishbone, maana ukikosea kuzirudisha kwenye alignment tu unaharibu handling na litaboa kuendesha..
Maoni yangu
Hizi ni gari nzuri saana, ukizitunza unaweza kuzitumia kwa muda mrefu saana bila kukuletea shida yeyote. Na idadi yake sio kubwa, hivyo ukiwa nalo linakuwa unique kidogo. Ila kama unaishi sehemu yanye barabara mbovu, halikufai, hata kama wewe ni dereva mzuri. Utachoka kuliendesha.

MAONI NA MICHANGO ILIYOTOLEWA NA WADAU WA JF
Hizi gari za alteza tokea zmetoka nazmezea mate Siku nyingi.

Maana mi mwnyw ni mpenzi sana was drifting.

Last 2 week nkawa napitia Fb na site mbalimbali nione kama naweza kumvua MTU.

Aisee,
Bei zake kwa used nmekuta zmekua chini mno, ukilinganisha na Brand New

Nyingi Namba C mpk D zinacheza kwny 4.5mil mpaka 6mil

Mpaka nmestuka, hv hizi gari zinamatatizo gani mpaka watu kibao waziuze bei ya kutupa namna hiyo?

Hebu nisaidie mkuu, japo kwa ushauri.
---
resale value ya gari zote ndogo zenye engine ya 2.0 ltr ni ndogo mno

kwa sababu mtu anafata gari ndogo ili apate fuel economic ila kwa altezza hutopata thats why unaona resale value ni ndogo the same na mark x na brevis and the likes

ukija kwenye resale value IST ipo juu kuliko mark x na tezza kwasababu ya fuel economic lakin hakuna tatizo kiufundi

chengine mkuu kwenye kununua altezza kama unataka isiyokula mafuta sana usidanganyike ukaenda kwenye 3S-GE I4 kisa eti ina cylinder 4 ukaacha 1G-FE I6 yenye cylinder 6 ukizani hii ya 6 ndio inakula mafuta

3S-GE I4 2.0 ltr hii inakula mafuta kuliko 1G-FE I4 2.0 licha ya kuwa hii 1G ni six na hyo 3S ni 4

sababu hyo 3S-GE yamaha waliitengeza kisport zaidi so piston room zake ni kubwa zaidi japo zipo nne kuliko zile za 1G zilizopo sita na hata kwenye power 3S-GE ina 210 bhp huku 1G-FE ikiwa na 160-180 bhp

so kama unataka altezza yenye unafuu wa mafuta usitishike na wingi wa cylinder chukua 1G-FE I6

ila kama unataka altezza yenye power chukua 3S-GE I4 kwa saloon na kwa GITA nenda kwenye badass machine 2JZ-GTE
 
Nadhani yenye hio kitu ya 2JZ itanifaa saaana, shida yangu na altezza gita ni kile kisogo/hatchback yani hapo hamu na ile gari hua inaisha mkuu.
Hehehee, hata mie mwanzo nilikuwa nakichukia kwa kweli. Ila with time nimegundua kinavutia. 2JZ safi saana. Kwanza ile engine kwa kweli, huwa haina shida za ajabu ajabu. Ukizoea mafuta yake, utaifurahia saana.
 
Hahah ntajitahidi kuzoea kile kisogo chake mkuu,umeshawahi kuifuatilia audi rs6?aisee ile hatchback mziki wake ni usipime mkuu.
 
Hizi gari za alteza tokea zmetoka nazmezea mate Siku nyingi.

Maana mi mwnyw ni mpenzi sana was drifting.

Last 2 week nkawa napitia Fb na site mbalimbali nione kama naweza kumvua MTU.

Aisee,
Bei zake kwa used nmekuta zmekua chini mno, ukilinganisha na Brand New

Nyingi Namba C mpk D zinacheza kwny 4.5mil mpaka 6mil

Mpaka nmestuka, hv hizi gari zinamatatizo gani mpaka watu kibao waziuze bei ya kutupa namna hiyo?

Hebu nisaidie mkuu, japo kwa ushauri.
 
Hizi gari za alteza tokea zmetoka nazmezea mate Siku nyingi.

Maana mi mwnyw ni mpenzi sana was drifting.

Last 2 week nkawa napitia Fb na site mbalimbali nione kama naweza kumvua MTU...

resale value ya gari zote ndogo zenye engine ya 2.0 ltr ni ndogo mno

kwa sababu mtu anafata gari ndogo ili apate fuel economic ila kwa altezza hutopata thats why unaona resale value ni ndogo the same na mark x na brevis and the likes

ukija kwenye resale value IST ipo juu kuliko mark x na tezza kwasababu ya fuel economic lakin hakuna tatizo kiufundi

chengine mkuu kwenye kununua altezza kama unataka isiyokula mafuta sana usidanganyike ukaenda kwenye 3S-GE I4 kisa eti ina cylinder 4 ukaacha 1G-FE I6 yenye cylinder 6 ukizani hii ya 6 ndio inakula mafuta

3S-GE I4 2.0 ltr hii inakula mafuta kuliko 1G-FE I4 2.0 licha ya kuwa hii 1G ni six na hyo 3S ni 4

sababu hyo 3S-GE yamaha waliitengeza kisport zaidi so piston room zake ni kubwa zaidi japo zipo nne kuliko zile za 1G zilizopo sita na hata kwenye power 3S-GE ina 210 bhp huku 1G-FE ikiwa na 160-180 bhp

so kama unataka altezza yenye unafuu wa mafuta usitishike na wingi wa cylinder chukua 1G-FE I6

ila kama unataka altezza yenye power chukua 3S-GE I4 kwa saloon na kwa GITA nenda kwenye badass machine 2JZ-GTE
 
Hizi gari za alteza tokea zmetoka nazmezea mate Siku nyingi.

Maana mi mwnyw ni mpenzi sana was drifting.

Last 2 week nkawa napitia Fb na site mbalimbali nione kama naweza kumvua MTU.

Aisee,
Bei zake kwa used nmekuta zmekua chini mno, ukilinganisha na Brand New

Nyingi Namba C mpk D zinacheza kwny 4.5mil mpaka 6mil

Mpaka nmestuka, hv hizi gari zinamatatizo gani mpaka watu kibao waziuze bei ya kutupa namna hiyo?

Hebu nisaidie mkuu, japo kwa ushauri.
Hehehee, hiyo kweli aise. Shida ni moja, walinunua vijana wengi ambao ndio yalikuwa magari yao ya kwanza. Hizi gari zina engine kubwa, hivyo zinakunywa mafuta, na spare parts zake japo zinapatikana ni bei kidogo, sasa vijana vinawashinda, pia, ziko chini saana.

Vijana wanapenda kuzunguka na gari kila wanapotaka kwenda, so wanajikuta wanazigonga kila kona. Na mwisho, vijana wananunua magari kwa fashion tu bila kuyafanyia utafiti.

Maana walipotoka kwenye Altezza, wakahamia Brevis, nalo likawashinda, wakahamia Mark X, huko wamechoka, sasa hivi Crown Athlete ndio habari ya mjini.
 
resale value ya gari zote ndogo zenye engine ya 2.0 ltr ni ndogo mno

kwa sababu mtu anafata gari ndogo ili apate fuel economic ila kwa altezza hutopata thats why unaona resale value ni ndogo the same na mark x na brevis and the likes

ukija kwenye resale value IST ipo juu kuliko mark x na tezza kwasababu ya fuel economic lakin hakuna tatizo kiufundi..
Nilishawaambia watu hilo wakabisha. 3S inanguvu kubwa kuliko 1G. 3S ina 210hp nadhani, kama Mark X, wakati 1G ya 6 cylinder ina 155hp.

2JZ naipenda kweli, basi tu. Na nyingi Limited edition. Ila kwa kweli, mafuta ya cc3000 yanaogopesha. Japo nina jamaa yangu alinunua Crown Athlete ya cc3000 anasema haina tofauti na Brevis yenye 1JZ
 
Hehehee, hiyo kweli aise. Shida ni moja, walinunua vijana wengi ambao ndio yalikuwa magari yao ya kwanza. Hizi gari zina engine kubwa, hivyo zinakunywa mafuta, na spare parts zake japo zinapatikana ni bei kidogo, sasa vijana vinawashinda, pia, ziko chini saana. Vijana wanapenda kuzunguka na gari kila wanapotaka kwenda, so wanajikuta wanazigonga kila kona. Na mwisho, vijana wananunua magari kwa fashion tu bila kuyafanyia utafiti. Maana walipotoka kwenye Altezza, wakahamia Brevis, nalo likawashinda, wakahamia Mark X, huko wamechoka, sasa hivi Crown Athlete ndio habari ya mjini.
Hapo kwenye spea umenistua sana mkuu.
Binafsi ni mvivu sana wa gereji.

Sipendi gari ya kunisumbua kichwa kwenye spea.
 
Nilishawaambia watu hilo wakabisha. 3S inanguvu kubwa kuliko 1G. 3S ina 210hp nadhani, kama Mark X, wakati 1G ya 6 cylinder ina 155hp.

2JZ naipenda kweli, basi tu. Na nyingi Limited edition. Ila kwa kweli, mafuta ya cc3000 yanaogopesha. Japo nina jamaa yangu alinunua Crown Athlete ya cc3000 anasema haina tofauti na Brevis yenye 1JZ

3S-GE ina nguvu sawa na 4GR-FSE ya mark X ...kile ki 1G hakuna kitu

ukija kwenye JZ engine series una hizi natural aspirated nakuna zile gte na get zenyewe ni turbo charged

sasa hizi 1JZ-FSE I6 2.5 na 2JZ-FSE I6 3.0 ni natural aspirated hazili mafuta sana na hazina tofauti ya ulaji wake

balaa lipo kwenyw hizi turbo charged 1JZ-GTE I6 2.5 turbo na 2JZ-GTE I6 3.0 turbo hizi ni more powerful wit huge room for mods and tuning zinakula mafuta balaa hizi
 
Mkuu, unataka kwenda kwenye Majesta, au Supra?
ilikuwa aristo mkuu nakumbuka tuning ya mwisho nilifanya pale kwa jet cruza kijitonyama GTP garaje

niliweka Front Mounted Inter Cooler na nilireplace the stock turbo nikaweka borge warner turbo nikafunga na water meth injection kit nikareplace speed meter nikaweka ya TRD inasoma 320 kph

sikumaliza miezi nilipata ajali maeneo ya bunju na gari ikawa rytoff kabisa
 
3S-GE ina nguvu sawa na 4GR-FSE ya mark X ...kile ki 1G hakuna kitu

ukija kwenye JZ engine series una hizi natural aspirated nakuna zile gte na get zenyewe ni turbo charged

sasa hizi 1JZ-FSE I6 2.5 na 2JZ-FSE I6 3.0 ni natural aspirated hazili mafuta sana na hazina tofauti ya ulaji wake

balaa lipo kwenyw hizi turbo charged 1JZ-GTE I6 2.5 turbo na 2JZ-GTE I6 3.0 turbo hizi ni more powerful wit huge room for mods and tuning zinakula mafuta balaa hizi
Kweli kabisa. 1G ni smooth tu vile ni inline 6. Ila 3S ina nguvu zaidi. Hizo turbocharged zinafaa saana kama unaendesha gari for fun. Ni umasikini tu unatusumbua, ila kuendesha gari lenye nguvu kuna raha yake aise
 
gari yenye power raha sana mkuu... japo watu wanasema AWD ndio mpango mzima ila mimi kwa gari yenye power na prefer sana reel wheel drive asee ukikanyaga unaifeel kabisa power inayota matairi ya nyuma kusukuma gari
 
ilikuwa aristo mkuu nakumbuka tuning ya mwisho nilifanya pale kwa jet cruza kijitonyama GTP garaje

niliweka Front Mounted Inter Cooler na nilireplace the stock turbo nikaweka borge warner turbo nikafunga na water meth injection kit nikareplace speed meter nikaweka ya TRD inasoma 320 kph

sikumaliza miezi nilipata ajali maeneo ya bunju na gari ikawa rytoff kabisa
Duu! Pole saana. Nawish Bongo kungekuwa na race track tuwe tunakwenda kujiachia huko. Sisi magari yetu tunakimbizana kwenye barabara za magari mengine, matokeo yake ajali zinakuwa nje nje.
 
Back
Top Bottom