Mtoa mada anaenadana na jina lake, Jingalao. Unazuga kuwa hujui yanayodaiwa na ZZK.jingalao hata kama kweli Zito ni mmiliki wa Precision au hata kampuni yoyote kama anachoongea ni legit ni legit tu hakitabadilika na kua utumbo/ uongo.
Kwa kushindwa kuelewa hoja ya msingi haswa ya Zito ndiyo kumepelekea uje kuandika uzi ambao haujakamilika vya kutosha kufanya tuhuma zako kwa Zito ziwe na mashiko.
Unafiki na ujinga unaangamiza Taifa.
ZZK ni mwakilishi wa wapiga kura wake wa Kigoma na watanzania. Kazi ya mwakilishi ni ninikwa maoni yako? Ukiulizwa, wewe ni nani na maoni yako yanawakilisha ya akina nani?
1. Sheria ya manunuzi ya umma imekiukwa ktk manunuzi haya,
2. Utekelezaji wa kibajeti umekiukwa,
3. Kumezuka tuhuma za kupiga dili kwenye aina ya ndege na bei,
4. Imetumika pesa taslimu badala ya utaratibu unaotumika duniani kote wa kununua ndege kwa njia ya malipo kidogo kidogo, na
5. Inadaiwa kuwa PS wa wizara ya fedha na Iukulu wana uhusiano wa kidugu.
Hayo ndiyo mambo yayohitaji ukweli (reality) anaodai mtoa mada.