The Palm Tree
JF-Expert Member
- Apr 13, 2013
- 7,951
- 12,535
Hii tovuti wananchi.go.tz inaendeshwa na iko chini ya Wizara ya habari, utamaduni na michezo.
Lengo lake kubwa ni kwa kila mwananchi mwenye kero, malalamiko, maoni, ushauri, kutoa ripoti za uhalifu, rushwa nk kuandika kero au taarifa yake kwa maandishi na wao wizara wanaipokea na kisha kuipeleka kwa mtu anayelalamikiwa au mamlaka (taasisi au idara ama ofisi ya umma) inayohusika ili waitolee ufafanuzi/majibu/ufumbuzi.
Binafsi, nilishatoa kero na malalamiko na kero nyingi sana kupitia njia hii. Nyingi sijawahi kujibiwa na nakumbuka kuna kero moja ya kiutumishi, ni mwaka wa saba sasa haijawahi kujibiwa. Huwa kila nikifungua kufuatilia jibu langu huwa nashangaa kwani mara zote nakutana na maelezo mafupi tu 'Kero yako Inashughulikiwa'.
Tumekuwa tunasisitizwa tuache kulalamika tu na kuishambulia serikali na badala yake tutumie njia sahihi kuwasilisha kero au malalamiko au ushauri wowote ili ufanyiwe kazi kwa utaratibu unaotakiwa wa Kiserikali.
Sasa mtu afanyeje iwapo anapeleka malalamiko au kero au maoni yake na wahusika badala ya kufanyia kazi na kutoa majibu wake badala yake wao wanakaa tu na kuifungia kero au lalamiko ya wananchi ndani ya kabati zao...?
Huku ni kushindwa kuwajibika kwa taasisi, serikali au idara za serikali. Tafadhali, toeni majibu kwa watu ndani ya muda uliopangwa (ndani ya siku tano za kazi kama mlivyoandika wenyewe) kuanzia siku hoja au kero au lalamiko limepokelewa...
Kinyume chake, serikali itaendelea kulalamikiwa na kutukanwa kwa vitu vidogo vidogo tu vinavyosababishwa na watendaji wachache wazembe na wasio waaminifu toka taasisi, idara na ofisi zote za umma.