Tovuti ya Polisi Huvamiwa na Turky Police Hakers Usiku | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tovuti ya Polisi Huvamiwa na Turky Police Hakers Usiku

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Head teacher, Aug 21, 2012.

 1. Head teacher

  Head teacher JF-Expert Member

  #1
  Aug 21, 2012
  Joined: Mar 10, 2012
  Messages: 1,811
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hii nimegundua hii saa 6:55 usiku wa kuamkia leo pale nilipokuwa natafuta namba ya kamanda wa polisi wa Kinondoni ili niripoti uzembe wa OCS wa Mbezi ambaye ameonyesha uzembe mkubwa wa kazi. Kuna Bar uchwara maeneo ninayoishi, hapa Ubungo Msewe, inaitwa China Town. Bar hii ni kero kubwa katika maeneo haya kwani hupiga mziki wa sauti ya juu sana hata baada ya saa 6 usiku. Mathalani usiku wa Idi bar hii ilipiga mziki hadi saa tisa kasoro za usiku, na jana wembe ni ule ule. Bar hii inasemekana inamilikiwa na aliyekuwa mtangazaji maarufu wa Radio Tanzania, na baadae kuwa mwandishi wa waziri mkuu mstaafu Sumaye. Sasa katika kutaka kuomba msaada wa Polisi kudhibiti hali hii ili tupate usingizi nilimpigia OCS wa Kituo cha Polisi Mbezi Kimara majira ya saa 6:35 kwa kupitia simu yake ya mkononi namba 0713701277 ambapo alipokea taarifa na kuahidi atanipa namba za polisi wa doria. Nilikata simu kusubiri hizo namba, na baada ya dakika saba (6:42) nilimpigia tena na cha kushangaza simu yake ilizimwa. Baada ya hapo nikapata wazo la kufungua tovuti ya Polisi www.policeforce.go.tz , nilishtuka baada ya kufunguka page iliyo na maandishi yanayosema haked by Turky Hakers, na maandishi yaliyojaa katika page ile nadhani yaliandikwa kituruki. Na palikuwa na picha moja tu ya askari polisi mzungu wa cheo cha kamisheni. Hivyo sikufanikiwa. Nikakumbuka kuwa kipindi cha nyuma niliwahi kuwasiliana na aliyekuwa RPC wa Ilala, ambaye inasemekana sasa ni RPC wa Morogoro. Namba yake (0715009980) bado ilikuwepo kwenye simu yangu nikampigia,. Ni wazi RPC huyu nilimwamsha kutoka usingizini, na nilipomwomba namba ya RPC kinondoni alisema "ninayo, acha nitafute nitakupigia.." RPC huyu namwona kama ni mmoja wa maofisa wa polisi ambao hufanya kazi kwa uadilifu wa hali ya juu. Akiwa Dar es Salaam, alikuwa active sana unapomtaarifu tukio la uharifu, namfananisha na RPC huyu na aliyekuwa kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam.


  Baada ya dakika 2, RPC wa Morogoro alinipigia simu na kunitajia namba ya simu ya RPC wa Kinondoni (0784820033).
  Nilipiga namba hii saa 7:08 usiku, ila haikupatikana.Baadae nikawa najaribu namba za emergency kama 112 bila mafanikio.Ilipofika saa 7:14,nibahatika kuiona namba (0732928723)ya trafic police, ambayo nakumbuka niliipata pale sayansi, jirani na rose garden, kwenye kibanda cha trafic. Nilipoipiga, haraka alipokea askari wa kike, na nilimweleza tatizo lililonisibu, alisema nimpe dakika 2 harafu nimpigie anipe namba ya kupiga. Nilipompigia alinipa namba 0787668306, hiyo ilikuwa saa 7:24. Dah, salio la simu ndio lilishaisha na sikuwa na jinsi tena ya kupiga simu.


  Inasikitisha Tanzania, ukivamiwa na majambazi usiku hutapata msaada wa jeshi la polisi. Sana naona umuhimu wa kuwa na siraha binafsi ya kujilinda, na kuchukua namba za simu za makampuni binafsi ya ulinzi...! Ni hatari!!!1
   
 2. PrN-kazi

  PrN-kazi JF-Expert Member

  #2
  Aug 21, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 2,890
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  .....huo ndiyo utandaji kazi wa Jeshi letu la Polisi; kazi wanayojua ni kupambana na wapinzani wa vyama vya siasa hasa wa CDM na kuzuia mikutano yao lakini si kulinda usalama wa raia: mheshimiwa pole sana kwa usumbufu unaoendelea kuupata kutokana makelele ya hiyo Bar.
   
 3. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #3
  Aug 21, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Utakuta mafungu ya kuendeshea hiyo web washakula wakubwa makao makuu pale. wana maana kwani?
   
 4. M

  Maga JF-Expert Member

  #4
  Aug 21, 2012
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 325
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Ndio jeshi letu mkuu, pole sana
   
 5. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #5
  Aug 21, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  Unaweza kuta server inalindwa na askari mwenye silaha ili isiwe 'hacked'
   
 6. papason

  papason JF-Expert Member

  #6
  Aug 21, 2012
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 2,317
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280
  Kulikoni mbona hawa ma haker wa kituruki wanavamia sana websites zetu? au pengine sisi ndo hatuna IT specialists, Juzi juzi waliana website ya wizara ya utalii baada ya siku mbili tatu wakavamia wizara ya afya, haya tena website ya polisi nayo chini ya ulinzi, kulikoni? au kuna ka mchezo kengine alafu tunawasingizia waturuki?
   
 7. tutaweza

  tutaweza JF-Expert Member

  #7
  Aug 21, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 618
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Ungetuma message na kuwaambia kuna wafuasi wa CHADEMA wanaandamana usiku na inaonyesha wanaelekea nyumbani kwa mwenyekiti wa CCM. Hapo wangekuja tu hata kama wapo Bagamoyo
   
 8. LOOOK

  LOOOK JF-Expert Member

  #8
  Aug 21, 2012
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 3,392
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  ha ha ha ha haaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa! lol! Nimeipenda sana u've made ma day.
   
 9. Head teacher

  Head teacher JF-Expert Member

  #9
  Aug 21, 2012
  Joined: Mar 10, 2012
  Messages: 1,811
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Aisee nimecheka sana maana ndio naiona usiku huu, Tanesco walikata umeme mara tu baada ya kuipost hii thread
   
 10. Head teacher

  Head teacher JF-Expert Member

  #10
  Aug 21, 2012
  Joined: Mar 10, 2012
  Messages: 1,811
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Pole mkuu, polisi yetu inalinda usalama wa ccm dhidi ya chadema si usalama wa raia
   
 11. Head teacher

  Head teacher JF-Expert Member

  #11
  Aug 21, 2012
  Joined: Mar 10, 2012
  Messages: 1,811
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Yaani jamaa angesema chadema wanaandamana maeneo hayo, zingekuja difenda 4, ulikosea kuripoti
   
 12. sterling

  sterling Senior Member

  #12
  Aug 21, 2012
  Joined: Aug 6, 2011
  Messages: 163
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  polisi wa tanzania ni washenzi sana wanajua kutuliza maandamano na migomo hata bila kupewa taarifa lakini vitu ambavyo havitishii ulaji wao lakini vina manufaa kwa wananchi hawavipi kipaumbele..... ninafikiri MWEMA na wenzake wanatakiwa wajitafakari kama bado wanastahili kuvitumikia vyeo vyao maan jeshi la polisi limeoza kabisa................
   
 13. Head teacher

  Head teacher JF-Expert Member

  #13
  Aug 21, 2012
  Joined: Mar 10, 2012
  Messages: 1,811
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mwema alianza vizuri, anamaliza kama Mahita
   
 14. Head teacher

  Head teacher JF-Expert Member

  #14
  Aug 21, 2012
  Joined: Mar 10, 2012
  Messages: 1,811
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0

  Aisee, sikujua kama ikifika saa sita usiku nchi inauzwa
   
 15. Head teacher

  Head teacher JF-Expert Member

  #15
  Aug 21, 2012
  Joined: Mar 10, 2012
  Messages: 1,811
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Unashangaa, nchi ilishauzwa long time
   
 16. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #16
  Aug 22, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,132
  Likes Received: 2,157
  Trophy Points: 280
  Inaelekea wameacha kutumia yale ma radiocall au wanayaona ni mizigo? kwani ukimpigia kamanda yeye ni kazi yake kuwafahamisha Askari Doria kwa kutumia Radiocall mara Moja
   
Loading...