Tovuti mbaya za serikali zilizotengenezwa na watalaam wa IT wa Tanzania

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
13,107
18,323
Toka Rais Magufuli aseme ataenda kuchukua watalaam wa IT nimeona ni vyema tuanze kuangalia na utalaam wa chini kabisa wa kutengeneza tovuti, na hapa tunaangazia tovuti za Serikali ambazo nyingi zimetengenezwa na watalaam wa IT wa Kitanzania.

Baada ya kuziangalia nimegundua kuwa kuna tatizo la kiutendaji kama si la kiuzalendo. Kazi nyingi katika eneo hili zimelipuliwa sana na zipo katika kiwango cha chini sana ukilinganisha na majirani zetu Rwanda na Kenya hata Uganda.

Tovuti nyingi za Serikali hazijaisha hadi leo, kuna page hazifunguki na wala hazina taarifa zinazohitaji kutokana na design za ovyo zilizotumika na pia hazina viwango kiusalama na hazipo kurahisisha maisha ya mwanachi wa Tanzania zipo kama urembo tuu.

Hata zile zilizotengenezwa na e- government zipo mahututi, zote zimetengenezwa kwa template tena zina fanana na mbaya hazina info za kutosha na too static. Hizi ni site za mazoezi kwa hackers hazina ubunifu wala creactivity yoyote .

Mfano ni tovuti ya National Defence College, sikutegemea kukuta tovuti ya jinsi ile kwa chuo kikubwa na chenye heshima kama kile. Aliyetoa tenda sijui nini kilimridhisha hata akairuhusu iwekwe hewani.

Mbeya university (MUST) admin tafuta kazi inayo kufaa.

Kama unajua tovuti mbaya weka hapa hawa wataalam wa IT wakibongo waone kazi zao mbaya. Wizi mtupu.

Asanteni.
 
1467688893731.jpg
 
mleta mada kuna kitu hujafanyia utafiti,umekurupuka kidogo bila kufanya upembuzi wakina...Yes,zimetengenezwa na watanzania "wakihindi" hawa wakina kemcho,ambao wao ndio walioshikilia hizi tenda zakutengeneza webisite nyingi za serikali wanatumia cheap labour na ulipua lipua ili kusave the amount....huwezi tumi hicho kipimo kupima creativity and art in building website...nenda Buni pale Costech ukutane na vijana uwape tenda uone what will happen! Mleta mada,fanya tafit za kina kabla ya kukurupuka!
 
Embu kajipange vizuri uje na uzi unao eleweka.. mbona website ya ikulu ipo vizuri sana. Una hoja lkn jaribu kuiweka vizuri.. Design na contents ni vitu viwili tofauti.
Unajua tovuti nzuri, tovuti sio picha tuu, ngoja waje watalaam hapa watakwambia
 
mleta mada kuna kitu hujafanyia utafiti,umekurupuka kidogo bila kufanya upembuzi wakina...Yes,zimetengenezwa na watanzania "wakihindi" hawa wakina kemcho,ambao wao ndio walioshikilia hizi tenda zakutengeneza webisite nyingi za serikali wanatumia cheap labour na ulipua lipua ili kusave the amount....huwezi tumi hicho kipimo kupima creativity and art in building website...nenda Buni pale Costech ukutane na vijana uwape tenda uone what will happen! Mleta mada,fanya tafit za kina kabla ya kukurupuka!
Nimefanya utafiti, ivi e government nao ni wahindi?
 
Kuhusu kufanana kwa website za serikali nafikiri ni muongozo waliopewa na e-government. Tovuti za serikali kuna jinsi inabidi ziwe ilikuwezesha kila rika kuweza kuziaccess
 
Nimefanya utafiti, ivi e government nao ni wahindi?
Tovuti gani waliyo design e-government ambayo wewe hujaikubali. Weka mifano, maana usifikiri tofuvuti zote za serikali wamedesign e-government. Alafu e-government wanakazi zaidi ya kudeal na website tu. Nakumbuka waziri mkuu aliwaambia waka audit mfumo wa bandari
 
Toka magufuli aseme ataenda kuchukua watalaam wa IT nimeona ni vyema tuanze kuangalia na utalaam wa chini kabisa wa kutengeneza tovuti , na hapa tunaangazia tovuti za serikali ambazo nyingi zimetwngenezwa na watalaam wa IT wa kitanzania.

Baada ya kuziangalia nimegundua kuwa kuna tatizo la kiutendaji kama si lankiuzalendo. Kazi nyingi ktk eneo hili zimelipuliwa sana na zipo ktk kiwango cha chini sana ukilinganisha na majirani zetu rwanda na kenya hata uganda.

Tovuti nyingi sa serikali hazija isha hadi leo, kuna page hazifunguki na wala hazina taarifa zinazo hitaji kutokana na design za ovyo zilizo tumika.

Hata zile zilizo tengenezwa na e- government zipo mahututi, zote zimetengenezwa kwa template tena zina fanana na mbaya hazina info za kutosha na too static.

Mfano ni tovuti ya National Defence College , sikutegemea kukuta tovuti ya jinsi ile kwa chuo kikubwa na chenye heshima kama kile.

Mbeya university ( must) admin tafuta kazi inayo kufaa

Kama unajua tovuti mbaya weka hapa hawa wataalam wa IT wakibongo waone kazi zao mbaya. Wizi mtupu

Asanteni.

Tanzania hakuna mtu anayeweza tengeneza website kiwango, hili nawahakikishia. Ni wavivu, wana copy na wanalipua. Nimetafuta Dar, Zanzibar, Arusha no creativity hata kidogo. Nikamlipa mtu Russia ukiona website unasema wow!
 
Back
Top Bottom