TOVL - Maktaba ya mtandaoni inayohimiza matumizi ya kompyuta kwa watoto

RobyMi

JF-Expert Member
Mar 4, 2012
848
863
Habari wana JF ..

Nimekutana na hii habari mwananchi nikaona ni vizuri kushare

Rainer Mwashu, mtaalamu wa utengenezaji wa mifumo ya kompyuta, ambaye kwa sasa ni muajiriwa wa Mamlaka ya Bandari, iliyo chini ya Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi , ametengeneza maktaba ya mtandaoni kwa ajili ya watoto kujisomea .

Maktaba hiyo inayoitwa Tanzania Online Virtual Library itawawezesha watoto na vijana wa rika mbalimbali kusoma vitabu mtandaoni kwa kutumia computer au sim zao za mikononi .

Ndan ya makala aliyofanya mahojiano na mwananchi Mr Rainer Mwashu anasema kilichomshinikiza kufanya hii project ni sabab alikua anatumia gharama kubwa sana kwa mwaka kuwanunulia watoto wake vitabu vya kujisomea , gharama ambayo ilikua inakwenda mpaka Tsh 800,000/- .

Taratibu akaanza azma yake ya kutengeneza hii web application ya TOVL , ili kuweza kuwasaidia watoto wake na watanzania wengine kwa ujumla . Anasema ilimchukua muda wa miezi sita kukamilisha azma yake hiyo.

Ukiingia ndan ya tovuti ya www.tovl.ac.tz na kujiandikisha utaweza kujisomea vitabu vya aina mbalimbali , na pia anashirikiana na washapishaji wa vitabu tanzania ili kuweza kushikiana nao katika upatikanaji wa vitabu vyao mtandaon .

RAINER MWASHU : Mbunifu wa maktaba ya mtandaoni anayehimiza matumizi ya kompyuta kwa watoto

Nampongeza sana Mr Rainer Mwashu , na ningependa kutoa pendekezo kwa serikali , itoe support kwenye innovative ideas kama za huyu mwenzetu , japokua lengo bado halijafikia anapotaka , lakin naamin endapo atapata japo support kidogo kwa vyombo husika itakua ni msaada mkubwa sana katika kutimiza hii ndoto yake ya kupeleka teknolojia katika ulimwengu wa elimu ya mtanzania .
 
nimejisajili nimeingia sytem ni nzuri, ipo stable na imekaa ki professional kabisa.

zBM1fli.jpg

itamsaidia mdogo wangu.

vipi kuhusu kupata hela itakuwaje? hivyo vitabu ananunua au watu wanajitolea kuvieka?
 
Kwa sasa anapewa vitabu anapewa na publishers , anafanya mazungumzo na oxford ili kuweza kutumia vitabu vyao .. ana mpango wa ku intergrate system na mobile payments . kwa iyo wasomaji watakuwa wanalipia kwa masaa .. Itakua ni kama subscription plan yenye package mbali mbali ..
 
sio mbaya, nitakua naendelea kuifuatilia hii project
 
Back
Top Bottom