Toute za JK mbona hasiendi TZ Vijijini?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Toute za JK mbona hasiendi TZ Vijijini??

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BabaH, Apr 15, 2008.

 1. BabaH

  BabaH JF-Expert Member

  #1
  Apr 15, 2008
  Joined: Jan 25, 2008
  Messages: 703
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Jamani ndugu zangu naomba kuhuliza na kueleweshwa
  Wakati Mkuu akiomba kura alihakikisha anafika walau kila mahali na ambapo ilikuwa ngumu kufika huku akifanya kila awezalo ili kupata kura za wananchi,

  Sasa leo hii baada ya kupata kura za hao walala hoi
  Amekuwa safari zinaishia mijini tena ni chache sana na eti mpaka apelekwe, lakini enzi zile ilifikia wakati aliamua aende wapi pia ambako aliona anaweza kupata kura nyingi pia

  Haya safari sasa zimekuwa nyingi sana za nje kuliko za kuwatembelea wananchi wake ambao walimchagua na kumwamini, wao wanaendelea kutaabika yeye kila kukicha yuko nchi za watu, sasa inakuwaje hapa.

  Pili wakati huo huo wapiga kura wake wakiwa wanataabika na hali mbaya yeye anatumia mijipesa kibao katika kusafiria tuuuuuu, na hata hakumbuki kama kuna watu wanateseka kabisa, mimi nashindwa kuelewa kabisa, hivi wakipewa madaraka huwa wanalewa na kujiona wao ni miungu hao??

  haya ebu niambie hapa, lakini eti 2010 atashinda tena!!
   
Loading...