Tour fupi ya shamba langu la greenhouse

Kuna mbegu za matango ambazo huwa tunaleta Na kuuza ambazo pia ndio Mimi nazitumia katika shamba langu ambazo zinakupa matango zaidi ya 20 kwa mche kwa msimu mzima Wa mwezi Na nusu

Mbegu hizi nimeleta paketi chache. Kwa anayehitaji anipigie 0758 308 193 bei ni sh 115,000

Uzuri Wa kulima matango ni kuwa kwa kuwa msimu wake ni Wa mudafupi inakupa nafasi ya kupata kipato cha haraka wakati ukisubiria nyanya kuwa tayari kuvuna kwani nyanya kutumia muda mrefu kuwa tayari kuuzwa
 
Kuna watu wanauliza maswali na nimeamua Ku share huku labda yatawasaidia na wengine. Swali linaloulizwa ni kuwa km nalima nyanya ambazo zinachukua kuanzia miezi 2.5 - 4 mpaka kuvuna na kuanzia kupata pesa, sasa ktk kipindi nasubiria kuvuna, je napataje pesa za kujimu?

Hili swali nahisi ndio linalotisha watu kuingia ktk kilimo kwa kuwa unachelewa kuanzia kupata pesa.

Jibu langu ni kuwa wakati unasubiria uanze kuvuna nyanya, unaweza Lima mazao ya muda mfupi lkn yenye uzao mkubwa na yanayovumilia mgonjwa. Mi napendelea matango lkn nimegundua Spinach INA soko zuri muda wote. Spinach huchukua wiki 2 - 3 kuvuna na kuanzia kuuza

Mfano: Unapanda spinach ktk mistari. Tenganisha mistari yako futi 2 kutoka mistari na mstari kila mstari una futi 10. Kulingana na ni mistari mingapi unaweka lkn kila mstari utakupa kilo 3.5 ambazo ni takriban mafungu 10 kulingana na sina ya mbegu. Sasa piga hesabu eneo lako lina ukubwa gani na utaweza mistari mingapi. Mfano km una eneo la sqm 21 utakuwa na mistari 14 hivyo x mafungu 10.

Mafungu 140 x Sh. 300 = 42000 kwa ka eneo kadogo hivyo baada ya wiki 3 tu. Hilo eneo ni 3 kwa 7

Hivyo km eneo lako ni kubwa basi utapata zaidi wakati ukisubiria mavuno ya nyanya hivyo kupata fedha wakati ukisubiria nyanya kuvunaa

Wewe nimekusoma sana leooo. Kama nimeanza kukuelewa hivi. yaani nimeanza kukuelewa. Nakuja inbox, maana tayari ninafanya kilimo-biashara.
 
Habari za asubuhi.

Kwa wale waliotaka angalau kuona kwa ufupi shamba langu la greenhouse ambalo nimelima nyanya ndani ya greenhouse na nje pia yaani bila greenhouse ila kwa kutumia formula maalumu ya kitaalamu ya kutumia gharama kidogo ila mavuno mengi na makubwa wanaweza ku click hiyo video hapo chini na kuangalia.



0758 308193



Mkuu kazi nzuri, upo mkoa gani?
 
Kila mwezi may huwa ni mwezi naotumia kuwakumbusha watu kuhusu tabia yetu ya kuogopa kujaribu mambo Na kuchukua hatua

Kuna watu walishawah niandikia miaka miwili nyuma mwezi km Wa Leo wakitaka kuanzisha miradi ya kilimo kwa ajili ya kujipatia kipato. Lkn tokea kipindi hicho hawakuanza huku kila kitu wanacho sababu wanayotoa ni kuwa eti kilimo hakilipi. Lkn kiukweli ni yoga wao walionao kila siku ndio uliosababisha waianze. Sasa Leo Jamaa kati ya hao Leo kanipihia ndio huko tayar Leo kuanzia Na kulipia mafunzo. Nikamuuliza sasa ni kwani ni ulikuwa unajichelewesha akasema ni upga wake tu umemrudisha nyuma.

Point yangu ya kuandika haya Leo ni kuwa tunaacha sana uoga Na hofu zituzuie kutimiza ndoto zetu kisha kujiluta tumepotexa muda sana. Je km huyu kijana miaka hiyo 2 iliyopita angeanza Na hata nusu ema tu Leo angrkuwa wapi hebu jiulize na usipoteze muda
 
I'm on the way Biashara2000 ,nilikupigia simu ukanipa machache kwa maneno ila mengi kwa ujumbe,ijapo wiki lijalo narudi tena kukucall ili unipe kile kitabu kisha tour hatimaye nikijiridhisha kuiva ndani ya mwezi huu basi JULY nalipuka rasmi,kikubwa nilichojifunza ni kuwa kilimo bila elimu hakilipi,ni sawa tu na mtu asiye na taaluma ya udaktari atawezekana vipi akafanya upasuaji? hilo haliwezekani kabisa maana kinachofuata tunakijua,hivyo tujikite kusomea taaluma za kisasa za kilimo cha biashara ambacho kwa imani yangu hata kama bado sijaanza kukifanya naamini kinalipa.
 
Bw. Ngamba umeuliza swali zuri sana, ni swali ambalo watu wengi wamekuwa wanapenda sana kufahamu. Kwa bahati ambayo sio poa wakulima wengi na wale ambao wana mpango wa kulima imekuwa vigumu kwao kupata info sahihi ntalijibu katika vipengele viwili

Mbegu hizi special kama Heirsloom, Corazon, Anna F1, Julia, Carson, Memoneta na n.k zina shelf life kubwa tu na zimeboreshwa kutoka katika nchi za ulaya zenye baridi na zilikuwa maalumu kwa ajili ya kupandea kwenye greenhouse. Sasa waafrika tunafoji na kuamua kuzitumia huku afrika ndio maana wakulima wengi wanalalamika zinawatesa zinashindwa kuvumilia hali ya joto ndio maana zinalimwa Arusha na Nairobi angalau penye kaubaridi

The kick ni kuwa hazikubali nje ya greenhouse yaani kulima kilimo cha wazi. Hii inanyima fursa kwa watu wasio na uwezo wa kifedha wa kujenga gh kushindwa kufanya kilimo cha kisasa na kufanya wakulima wa kawaida kubaki na zile mbegu za kawaida mfano Tengeru na Tanya

Mbegu ambayo mi nawashauri watu waitumia ndio ambayo mie naitumia. Hii imeboreshwa kutoka nchi ya ulaya ambayo iko karibu na bahari ya med. ambalo ni eneo lenye kiwango angalau cha joto. Baada ya hapo ililetwa afrika kusini kuboreshwa Zaidi. Pia ikajaribiwa ktk nchi za afrika ktk gh na kilimo cha wazi. Mbegu hii unaweza ilima ndani ya gh na kilimo cha wazi km ilivyo kwenye hiyo video yangu hapo juu na inavumilia ukame na jotohivyo ni nzuri kwa mikoa yote ya tz
Mwakan nampango wa kujenga greenhouse shy so tutachekiana humuhmu jukwaan
 
Ngoja nikupe mfano. Tuseme unaishi katika nyumba ambayo kwa upande wa nyuma una eneo ambalo lina ukubwa wa upana hatua tano na urefu vile vile. Hivyo 5 x 5 = 25 square meter. Katika kila square meter 1 unapanda miche 4 hivyo x 25 ni miche 100. Kila mche unakupa kilo 15 yaani sawa na ndoo moja na nusu ya nyanya kwa mwezi. Bei ya shambani ukiamua kufanya mia tano x 15 ni sh. 7,500 kwa kila mche kwa mwezi. 7,500 x miche 100 = sh. 750,000 kwa mwezi. Je kwa miezi nane ya uvunaji itakuaje? 6,000,000. Na hii ni bila greenhouse

Je utaendelea kunyanyaswa na bosi wako ulipoajiriwa na kuendelea kumtajirisha mpaka lini?
Aisee saf sana
 
Kuna watu wanauliza watatutibuje mdudu Wa kantangaze. Mdudu yeyote asiyetakiwa mahala popote pale huwa akija anafuata uchafu Wa aina Fulani. Hivyo kabla hujaanza pulizia dawa za wadudu kwanza safisha eneo lako has a majani majani yasiyotakiwa kuwapo yalime yasiwapo.

Hakikisha unafuata utaratibu nzuri Wa upuliziaji dawa Na hii itasaidia sana kumfukuza

Ugonjwa unaoletwa Na mdudu huyu haina dawa lkn unaweza pulizia dawa kupunguza madhara take. Ni kmUkimwi haina dawa lkn ikirumia ARV unaweza punguza madhara take Na kuishi

Pulizia mchanganyiko Wa dawa inaitwa Blast + Ebony inasaidiaviwango tofauti kutoka na ma eneo Na eneo

Ukikosa dawa hizo gunia inayoitwa Spinosad

Wadudu hawa muda Wa mchana hujificha ktk majani Na kutoka usiku Na kula mimea Na matumda hivyo ndio sababu nikasema hakikisha shamba lako zima haina majani ya aina yoyote ile zaidi ya niche yako
 

Similar Discussions

54 Reactions
Reply
Back
Top Bottom