Tottenham Hotspurs Thread

Come On You Spurs.

Jana tumepokea kipigo nyumbani. Timu iliweza kutengeneza nafasi ila defense ikaendelea kuwa uchochoro.

Ni dhahili sasa ndoto za top four zinazidi kufifia. Ngoja tusubiri tuone.

Sent using Jamii Forums mobile app
Spurs walicheza mchezo mzuri, shida ya umaliziaji bado ipo, defence inamatatizo bado hasa kutokana na full backs kucheza kama mawinger.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Come On You Spurs

Kikosi cha leo ni kama ifuatavyo. Ngoja tusubiri tuone Mourinho magic ijapokuwa based on quality ya vikosi, hatustahili.

Let's hope for the best.
IMG_20200310_222150.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ubora ni depth ya squad inayompa different options kama akiamua kubadili mfumo.

Kwanini Asicheze 4 3 2 1
Lamela akiwa kama target man halafu Geovani/ Bergwijn na Lucas Moura/Delle Ali wakacheza nyuma yake, hao watatu Harry Winks Tanguy Ndombele na Gedson Fernandez.?

Au akacheza 4 4 2 diamond akamtumia Lamela tena kama target man ?
Kikosi siyo bora. Kukosekana kwa wachezaji watatu muhimu KANE, SON na SISSOKO kunaiathiri timu

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ubora ni depth ya squad inayompa different options kama akiamua kubadili mfumo.

Kwanini Asicheze 4 3 2 1
Lamela akiwa kama target man halafu Geovani/ Bergwijn na Lucas Moura/Delle Ali wakacheza nyuma yake, hao watatu Harry Winks Tanguy Ndombele na Gedson Fernandez.?

Au akacheza 4 4 2 diamond akamtumia Lamela tena kama target man ?

Sent using Jamii Forums mobile app
Bergwijn ni majeruhi. Pia Delle Alli na Moura ndiyo pekee wanaweza cheza kama target men angalau. Kwa kasi ya RB Leipzig huwezi mchezesha Ndombele mwenye mwendo wa kobe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lamela amewahi kucheza kama target man enzi hizo Harry Kane hajawa wamoto sana.

Delle Alli na Lucas Moura hawawezi kuwa target man cause they are typical mobile wingers na hawana instincts za striker.

Lamela ana insticts za Striker na ni mrefu you can count on his aerial qualities.

Ana art ya uchezaji ambayo ni ideal kwa Strikers.

Tunazungumzia present mzee. Lamela wa sasa hayuko fiti. Anamwomba kocha acheze dk 20 au 30 za mwisho. Mfuatiliage habari basi.
Lamela amewahi kucheza kama target man enzi hizo Harry Kane hajawa wamoto sana.

Delle Alli na Lucas Moura hawawezi kuwa target man cause they are typical mobile wingers na hawana instincts za striker.

Lamela ana insticts za Striker na ni mrefu you can count on his aerial qualities.

Ana art ya uchezaji ambayo ni ideal kwa Strikers.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
HALI si hali kwa Jose Mourinho tangu atue Tottenham Hotspur mambo yanazidi kumwendea kombo, badala ya kuiinua miamba hiyo ya London Kaskazini anazidi kuizamisha.
Katika mechi sita zilizopita amepigwa kwenye mechi tano, timu imetolewa katika Kombe la FA na Ligi ya Mabingwa Ulaya, nafasi ya nne kwenye Ligi Kuu inazidi kuwa ndoto kwao, lakini je, ni wapi kocha huyu wa Kireno amekosea tangu atue Spurs? Makosa yake haya hapa.

1. Ugomvi wake na Tanguy Ndombele
Kwani kuna mtu hajui kama Mourinho anapenda ugomvi? Kama hujui habari ndiyo hiyo, kila sehemu anayoenda lazima azinguane na wachezaji wake. Inawezekana mwenyewe anaamini hiyo ni njia sahihi ya kuwafanya kuwa bora na kuthibitisha utawala wake, huwezi kujua. Pale Spurs tayari ameshamzingua mtu, Tanguy Ndombele ameingia kwenye orodha yenye watu kama kina Luke Shaw, Paul Pogba, Iker Casillas na Joe Cole kama mmoja kati ya watu waliowahi kuuona ubaya wa Mreno huyo.
Ni ajabu, ukiacha tu kwamba haipendezi kumponda mchezaji wako hadharani, lakini inakera zaidi unapomponda mchezaji ambaye amesajiliwa kwa dau la rekodi na klabu. Usajili wa Ndombele wa Pauni 62 milioni ndiyo unashikilia rekodi pale Spurs.
Sawa, amekuwa na majeraha ya mara kwa mara, lakini kila anapocheza amekuwa mchezaji bora kwenye kikosi cha Spurs. Inawezekana ni kweli kuwa Ndombele hayuko sawa sana, lakini ni jukumu la kocha kumrudisha vizuri na si kumtukana.
Lakini, Mourinho badala ya kumsaidia mchezaji wake mwenye kipaji zaidi kaamua kumzingua - tena kamzingua sana na hili ni kosa kubwa hasa kwa wachezaji wa kileo ambao ukiwazingua kidogo tu wanaacha kujitolea matokeo yake kocha anaharibikiwa.

2. Anakosea kumtumia Dele Alli
Dele Alli amefunga mabao manne katika mechi nne za kwanza chini ya Mourinho pale Spurs. Straika huyo alionekana kama amezaliwa upya kwa sababu takwimu zake zilianza kuzungumza.
Lakini, sasa mambo yamebadilika baada ya Spurs kukumbwa na majerahi wengi, ameamua kumtoa Delle kutoka nafasi ya straika wa pili ambayo amekuwa akifanya vizuri na kumsogeza mbele acheze kama mshambuliaji kamili.
Kilichopo, Delle anachukia sana kucheza kama straika, anapenda kucheza nyuma ya mshambuliaji, yeye aina yake ya soka haina tofauti sana na Thomas Muller, lakini kwa bahati mbaya Mourinho kaamua kumchezesha mbele zaidi.
Delle anaweza kuipa Spurs mabao, lakini ili kufanya hivyo anatakiwa kurudi kwenye nafasi anayoimudu zaidi, kitendo cha Mourinho kuendelea kumkomalia asimame mbele kabisa ni kosa lingine ambalo linamtafuna.

3. Ishu ya golini
Mourinho alipopewa jukumu la kuinoa Spurs kipa namba moja Hugo Lloris alikuwa majeruhi, hivyo Paulo Gazzaniga akakaa golini. Lloris alipokuwa fiti alirudishwa tena golini, safi sana. Lakini shida ikaanza hapa.
Lloris aliumia nyonga na kukosa mechi kadhaa. Wakati huu Gazzaniga alikuwa fiti, hivyo alitakiwa kurudi golini, lakini Mourinho akaamua kumrudisha kikosini Michel Vorm. Vorm hakuwa amecheza kwa miezi 18 wakati Mourinho alipompa nafasi, matokeo yake alitoa boko kwenye mechi dhidi ya Norwich na kuipa timu hiyo bao la kusawazisha kabla ya mechi kwenda matuta na Spurs kutolewa kwa mikwaju ya penalti katika Kombe la FA.
Mechi iliyofuata akamrudisha golini Lloris ambaye hakuwa fiti vya kutosha badala ya kumpa nafasi Paulo Gazzaniga, kilichotokea sasa Lloris aliruhusu bao la kizembe dhidi ya Burnley, mechi iliyofuta aliiruhusu RB Leipzig kufunga mabao mawili. Kama Mourinho angempa nafasi Gazzaniga ni wazi kuwa alikuwa kwenye kiwango bora kuliko wale makipa wawili ambao yeye aliwakimbilia kwenye Kombe la FA na Ligi ya Mabingwa Ulaya.

4. Kumbania Troy Parrott
Mwenyewe akiiangalia safu yake ya ushambuliaji anadai kuwa ni sawa na kwenda kwenye vita na bunduki bila risasi, hii ni kwa sababu Harry Kane na Son Heung-Min ni majeruhi na hao ndiyo wafungaji wakubwa wa mabao ya Spurs.
Mourinho amejaribu kuziba mapengo yao kwa
kuwatumia Lucas Moura na Delle akiamini lolote linaweza kutokea, lakini kosa kubwa analofanya ni kumnyima nafasi Troy Parrott, ambaye ni straika wa asili ambaye yuko kwenye kikosi cha vijana cha timu hiyo ambacho ni zao la Spurs.
Inashangaza kuona Mourinho kila siku analia na kukosa watu kwenye safu yake ya ushambuliaji, wakati hataki kumtumia mtu mmoja ambaye ni straika wa asili aliyefiti katika kikosi chake. Parrott amefunga mabao matatu katika mechi mbili alizoanza akiwa na kikosi cha Spurs chini ya miaka 23 na mabao sita katika mechi nne za michuano ya vijana ya UEFA.
Kumtumia Parrott si tu kutamsaidia kwa sababu dogo anajua, lakini pia kutatoa nafasi kwa Delle kurudi kwenye nafasi yake ya mshambuliaji wa pili ambayo huwa anafanya vizuri zaidi.

5. Anapoteza asili yake
Mourinho alikuwa mpambanaji kwenye, siku zote ilijulikana kuwa timu yake lazima itakuwa na ukuta wa chuma. Si unakumbuka enzi zile yuko Chelsea, kikosi chake kiliweka rekodi ya kufungwa mabao machache zaidi katika Ligi Kuu England (15).
Lakini, sasa amebadilika kikosi chake cha Spurs kina ukuta dhaifu, kinaruhusu sana mabao chini yake kimesharuhusu mabao 23 na hadi sasa kimecheza mechi tatu tu bila kuruhusu nyavu zake kuguswa.
Ukizitazama takwimu hizi unaweza kujikuta ukijiuliza kuwa huyu ni Mourinho kwenye au mfano wake? Maana inashangaza, sawa timu yake haifungi, lakini hata kuzuia kunamshinda, na hili ni kosa hasa kwa kocha ambayo amezoea kushinda idadi ndogo ya mabao.
Miaka ya nyuma alifanikiwa kwa sababu hata alipokufunga bao moja ilikuwa ngumu sana kugusa nyavu zake, lakini pale Spurs watu wanajipigia tu, hivyo kama anataka kurudisha ufalme wake kwanza arudi katika asili yake ya kutengeneza timu yenye ukuta wa chuma ambayo inaweza kujilinda hata kama inashambuliwa kwa dakika 120.

Kwenye hoja ya ugomvi nakubaliana na wewe ingawaje tuliona hata akina Furgerson wakiwapiga wachezaji viatu vya kichwani, lakini pia Mou hata mchezaji akifanya vizuri humsifia hadharani pia.

Kwenye ishu ya magolkipa ni hatujui mazoezini ilikuwaje na jopo la madaktari wa timu lilisemaje kuhusu Lloris, siku zote Mou amekuwa akimsifia Gazaniga. Lakini pia anatoa nafasi kwa kila mchezaji kucheza ili aweze kutoa tathmini sahihi kuhusu msimu ujao, huyu Vermon ni kama anauzwa mwisho wa msimu huu.

Kuhusu defence ni wazi ni eneo ambalo halijapata tiba kwa muda mrefu, ndio maana amejaribu kumleta Tanganga na ameahidi kuendelea kujenga ukuta wa timu, hata ile defence ya Chelsea ilitokana na wachezaji aliowasajili.

Kuhusu Delle Alli ni wazi ameanza kucheza kwenye nafasi hiyo baada ya Son na Kane kuumia, kati ya wachezaji waliopo ni wazi kuwa Delle ndio anastahili kuwa target man.

Tusiwe judgemental kwa sasa, tusubiri majeruhi wapone na usajili ufanyike ndio tutoe verdicts zetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
HALI si hali kwa Jose Mourinho tangu atue Tottenham Hotspur mambo yanazidi kumwendea kombo, badala ya kuiinua miamba hiyo ya London Kaskazini anazidi kuizamisha.
Katika mechi sita zilizopita amepigwa kwenye mechi tano, timu imetolewa katika Kombe la FA na Ligi ya Mabingwa Ulaya, nafasi ya nne kwenye Ligi Kuu inazidi kuwa ndoto kwao, lakini je, ni wapi kocha huyu wa Kireno amekosea tangu atue Spurs? Makosa yake haya hapa.

1. Ugomvi wake na Tanguy Ndombele
Kwani kuna mtu hajui kama Mourinho anapenda ugomvi? Kama hujui habari ndiyo hiyo, kila sehemu anayoenda lazima azinguane na wachezaji wake. Inawezekana mwenyewe anaamini hiyo ni njia sahihi ya kuwafanya kuwa bora na kuthibitisha utawala wake, huwezi kujua. Pale Spurs tayari ameshamzingua mtu, Tanguy Ndombele ameingia kwenye orodha yenye watu kama kina Luke Shaw, Paul Pogba, Iker Casillas na Joe Cole kama mmoja kati ya watu waliowahi kuuona ubaya wa Mreno huyo.
Ni ajabu, ukiacha tu kwamba haipendezi kumponda mchezaji wako hadharani, lakini inakera zaidi unapomponda mchezaji ambaye amesajiliwa kwa dau la rekodi na klabu. Usajili wa Ndombele wa Pauni 62 milioni ndiyo unashikilia rekodi pale Spurs.
Sawa, amekuwa na majeraha ya mara kwa mara, lakini kila anapocheza amekuwa mchezaji bora kwenye kikosi cha Spurs. Inawezekana ni kweli kuwa Ndombele hayuko sawa sana, lakini ni jukumu la kocha kumrudisha vizuri na si kumtukana.
Lakini, Mourinho badala ya kumsaidia mchezaji wake mwenye kipaji zaidi kaamua kumzingua - tena kamzingua sana na hili ni kosa kubwa hasa kwa wachezaji wa kileo ambao ukiwazingua kidogo tu wanaacha kujitolea matokeo yake kocha anaharibikiwa.

2. Anakosea kumtumia Dele Alli
Dele Alli amefunga mabao manne katika mechi nne za kwanza chini ya Mourinho pale Spurs. Straika huyo alionekana kama amezaliwa upya kwa sababu takwimu zake zilianza kuzungumza.
Lakini, sasa mambo yamebadilika baada ya Spurs kukumbwa na majerahi wengi, ameamua kumtoa Delle kutoka nafasi ya straika wa pili ambayo amekuwa akifanya vizuri na kumsogeza mbele acheze kama mshambuliaji kamili.
Kilichopo, Delle anachukia sana kucheza kama straika, anapenda kucheza nyuma ya mshambuliaji, yeye aina yake ya soka haina tofauti sana na Thomas Muller, lakini kwa bahati mbaya Mourinho kaamua kumchezesha mbele zaidi.
Delle anaweza kuipa Spurs mabao, lakini ili kufanya hivyo anatakiwa kurudi kwenye nafasi anayoimudu zaidi, kitendo cha Mourinho kuendelea kumkomalia asimame mbele kabisa ni kosa lingine ambalo linamtafuna.

3. Ishu ya golini
Mourinho alipopewa jukumu la kuinoa Spurs kipa namba moja Hugo Lloris alikuwa majeruhi, hivyo Paulo Gazzaniga akakaa golini. Lloris alipokuwa fiti alirudishwa tena golini, safi sana. Lakini shida ikaanza hapa.
Lloris aliumia nyonga na kukosa mechi kadhaa. Wakati huu Gazzaniga alikuwa fiti, hivyo alitakiwa kurudi golini, lakini Mourinho akaamua kumrudisha kikosini Michel Vorm. Vorm hakuwa amecheza kwa miezi 18 wakati Mourinho alipompa nafasi, matokeo yake alitoa boko kwenye mechi dhidi ya Norwich na kuipa timu hiyo bao la kusawazisha kabla ya mechi kwenda matuta na Spurs kutolewa kwa mikwaju ya penalti katika Kombe la FA.
Mechi iliyofuata akamrudisha golini Lloris ambaye hakuwa fiti vya kutosha badala ya kumpa nafasi Paulo Gazzaniga, kilichotokea sasa Lloris aliruhusu bao la kizembe dhidi ya Burnley, mechi iliyofuta aliiruhusu RB Leipzig kufunga mabao mawili. Kama Mourinho angempa nafasi Gazzaniga ni wazi kuwa alikuwa kwenye kiwango bora kuliko wale makipa wawili ambao yeye aliwakimbilia kwenye Kombe la FA na Ligi ya Mabingwa Ulaya.

4. Kumbania Troy Parrott
Mwenyewe akiiangalia safu yake ya ushambuliaji anadai kuwa ni sawa na kwenda kwenye vita na bunduki bila risasi, hii ni kwa sababu Harry Kane na Son Heung-Min ni majeruhi na hao ndiyo wafungaji wakubwa wa mabao ya Spurs.
Mourinho amejaribu kuziba mapengo yao kwa
kuwatumia Lucas Moura na Delle akiamini lolote linaweza kutokea, lakini kosa kubwa analofanya ni kumnyima nafasi Troy Parrott, ambaye ni straika wa asili ambaye yuko kwenye kikosi cha vijana cha timu hiyo ambacho ni zao la Spurs.
Inashangaza kuona Mourinho kila siku analia na kukosa watu kwenye safu yake ya ushambuliaji, wakati hataki kumtumia mtu mmoja ambaye ni straika wa asili aliyefiti katika kikosi chake. Parrott amefunga mabao matatu katika mechi mbili alizoanza akiwa na kikosi cha Spurs chini ya miaka 23 na mabao sita katika mechi nne za michuano ya vijana ya UEFA.
Kumtumia Parrott si tu kutamsaidia kwa sababu dogo anajua, lakini pia kutatoa nafasi kwa Delle kurudi kwenye nafasi yake ya mshambuliaji wa pili ambayo huwa anafanya vizuri zaidi.

5. Anapoteza asili yake
Mourinho alikuwa mpambanaji kwenye, siku zote ilijulikana kuwa timu yake lazima itakuwa na ukuta wa chuma. Si unakumbuka enzi zile yuko Chelsea, kikosi chake kiliweka rekodi ya kufungwa mabao machache zaidi katika Ligi Kuu England (15).
Lakini, sasa amebadilika kikosi chake cha Spurs kina ukuta dhaifu, kinaruhusu sana mabao chini yake kimesharuhusu mabao 23 na hadi sasa kimecheza mechi tatu tu bila kuruhusu nyavu zake kuguswa.
Ukizitazama takwimu hizi unaweza kujikuta ukijiuliza kuwa huyu ni Mourinho kwenye au mfano wake? Maana inashangaza, sawa timu yake haifungi, lakini hata kuzuia kunamshinda, na hili ni kosa hasa kwa kocha ambayo amezoea kushinda idadi ndogo ya mabao.
Miaka ya nyuma alifanikiwa kwa sababu hata alipokufunga bao moja ilikuwa ngumu sana kugusa nyavu zake, lakini pale Spurs watu wanajipigia tu, hivyo kama anataka kurudisha ufalme wake kwanza arudi katika asili yake ya kutengeneza timu yenye ukuta wa chuma ambayo inaweza kujilinda hata kama inashambuliwa kwa dakika 120.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sijui kama unafuatilia vema mwenendo wa Spurs. Lakini kwa kifupi ni kuwa yeyote anayejua mpira asingempanga Delle Alli namba 10 na kumwacha nje Lo Celso.

Pia Parrott ana utoto mwingi na Mourinho atampa nafasi taratibu mpaka pale atakapokua. Kama unafahamu namna alivyowatransform Frank Lampard na Scott McTominay utaelewa nini namaanisha.

Pia ukiweza kuelewa kwa nini wachezaji kama Danny Welbeck Sir Alex hakukurupuka kuwaingiza uwanjani mapema ndiyo utaielewa vema ishu ya dogo Parrott.

Kuhusu Ndombele ni kwamba Mourinho anapaswa kupongezwa na si kulaumiwa. Ni Mourinho aliyetaka Ndombele aundiwe program maalum ya kumrejesha mpirani ikihusisha benchi, uongozi, madaktari na wataalamu wa lishe. Ni yeye mwenyewe aliamua kuji-Lukaku (overweight) hivyo uwanjani anakuwepo timu ikiwa na mpira.

Mwisho kumlaumu Mourinhyo kufungwa michezi 4 na sare 2 kwa michezo 6 ya mwisho ni dalili ya kutoielewa vema Spurs. Kwa kifupi mpaka wanaumia Sonny na Kane walikuwa wamefunga 49% ya magoli yote ya Spurs msimu huu. Spurs imejengwa kuwazunguka.

Nakupa homework ya kunitafutia mechi ambayo Spurs walishinda bila hao watu wawili tangia 2014. Kazi ya Mourinho ni kulifuta hilo na kuijenga upya Spurs, kazi iliyomshinda kocha wetu kipenzi Pochetino.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ligi ndiyo hiyo imeisha na angalau tutacheza kombe ambalo Jose kasema kufuzu maana yake kulibeba tayari! Kacheza mara mbili na kalibeba mara hizo. Kwa maneno yake mwenyewe kasema siyo mbaya kushiriki kwa mara ya 3 na kulibeba kwa mara hiyo.

Siyo mbaya. Kipi bora? Kushiriki UCL na kuishia fainali au kushiriki UEL na kulibeba? Mafanikio hupimwa kwa vikombe na si idadi ya fainali ulizocheza.

Natarajia kutakuwa na sura mpya dirisha hili la msimu wa korona. Binafsi nadhani kuna maeneo yafuatayo yanahitaji uwekezaji.

1. CD. Hapa tuna Dier, Sanchez, Tanganga, Toby na Foyth. Super Jan anaondoka. Pia inaonesha kocha hajamkubali dogo Foyth. Eric Dier kasaini mkataba mpya kwa sharti la kucheza kama CB. Napendekeza anunuliwe CB mnyumbulifu wa kuimarisha safu ya ulinzi.

2. DM. Hapa tayari dogo Oliver Skipp kasaini mkataba wa kudumu mpaka 2024. Hata hivyo bado tunahitaji holding midfielder wa kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Wanyama/Dier. Hapa nadhani apatikane mkongwe wakati dogo Skipp anaendelezwa mdogo mdogo.

Kwenye DM's wanyumbulifu nadhani Sissoko angeuzwa tu. Nafasi yake ichukuliwe na Sergej Milinkovic Savic wa Lazio. Akawaongezee nguvu Ndombele, Gedson, Winks, na Lo Celso.

3. RW. Hapo Lamela atoswe tupate ingizo jipya umri na calibre ya Steven Bergwijn. Hivyo tutakuwa na Sonny/Bergwijn kwenye LW. RW tutakuwa na Moura na hilo ingizo jipya.

3. No. 10. Hapa kwenye namba 10 tunaye Lo Celso tayari ambaye kimsingi ndiye mbadala wa Eriksen. Wasiwasi wangu ni "The Dele Alli problem" kama anavyosemaga Mourinho. Dele hawezi mbenchi Lo Celso nyuma ya ST. Dele kukaa benchi kutapelekea chokochoko kutoka kwa English media. Ningekuwa Mourinho ningemuuza tu na pesa hiyo plus ile ya Lamela ningenunulia winger mzuri wa kulia.

4. FB. Suala la full backs liko wazi. Ssengnon hawezi kuwa full back karibuni. Anaweza zaidi kama wingback na Mourinho angependa full back. Hivyo ni ama auzwe Ben Davies au dogo C
Sess. Suala la kuleta mabeki wapya kulia na kushoto ni la lazima hslihitaji mjadala.

5. ST. Hapa itategemea na ikiwa Kane ataondoka au laa. Nimesikia tunamnyatia Zaniolo wa AS Roma japo kocha wao kakanusha.

Ngoja tusubiri tuone.
 
Siyo mbaya. Kipi bora? Kushiriki UCL na kuishia fainali au kushiriki UEL na kulibeba? Mafanikio hupimwa kwa vikombe na si idadi ya fainali ulizocheza.

Tafuta ulinganifu wa alichopata Tottenham kuingia finals UEFA vs alichopata Chelsea kwa kushinda Europa.

Utabadili haya mawazo.
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom