TOT kutumika kujibu wapinzani..hiki ni kioja!

Kikwebo

JF-Expert Member
Aug 25, 2006
405
204
Katika gazeti la Tz Daima la leo kuna habari kama kikundi cha muziki wa Dansi kinachomilikiwa na chama tawala kitatumia katika safari za mikoani za kujibu tuhuma za ufisadi kama zilivyowasilishwa na upinzani.
Sambamba na TOT wale walioonekana kama ni makapi ya upinzani wakiwemo Akwilombe (CHADEMA na CUF),Hiza (NCCR na CUF)na Msabaha (CUF) watatumika katika kampeni hii. Hawa mabwana ni mabingwa wa uzungumzaji na Propaganda.Analysis yangu ni kuwa serikali imeshikwa pabaya. Nilitegemea wangetumika wanasheria waandamizi, wachumi, nk kuweka wazi uhalisia wa kilichozungumzwa na kambi upinzai. Lakini kumtumia Hiza..form 4 au Msabaha nadhani huyu ni std 4 na elimu ya madrasa..kutaka kuchambua hoja za mambo ya mikataba ni kichekesho. CCM amkeni tuambieni kilichotokea na siyo kutumia vikundi vya uhamasishaji na mabingwa wa propaganda.

Tunajisikia tabu kuweka sura zetu kushabikia chama chetu kikongwe cha CCM, tunahisi hali ya kisiasa imechafuka tusaidieni wanachama wenu.

Kingwele wa kingwele.
 
Kingwele kumbuka kuwa hata Warioba ni Mwanasheria,tena aliwahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na pia Jaji na isitoshe ana ofisi yake ya uwakili (Warioba, Mahalu & Nyalali),nadhani ulimsikia kauli aliyoitia wiki iliyopita,watu tulidhani analeta facts na uchambuzi wa maana wa kisheria kumbe wapi,longo longo tu...sasa kama ukiona hata Warioba naye anapiga danadana tu kwenye hoja za Slaa ujue hapo kazi ipo,so far CCM na Serikali wameshatoa matamko yasiyopungua 7 lakini yote hayana uzito wowote,nadhani hata kwa upande wao hali inazidi kuwachanganya,imagine wanaye Hosea bingwa wa propaganda za vita rushwa,lakini mpaka sasa hajaongea lolote wakati alidai wako fit kabisa (sijui kina Ole Porokwa na laizer wanajisikiaje kwa sasa),wanao kina Manumba (ambaye alijaribu kutoa maelekezo ya uchunguzi wa kauli za Mbowe kule Tabora,sijui amefikia wapi),wanaowanasheria kina Lamwai,Mwakyembe,Mkono (ambaye sasa na yeye anadaiwa bn 10/=)...

hivyo CCM wanatapatapa tu,kama timu yao yote hiyo imeyumbishwa na wabunge wa Upinzani wasiozidi 50,sijui...cha msingi wao walete data na facts tu...
 
Wasipokuwa makini wataishia kuzomewa hata kama watapeleka TOT Plus. Ningekuwa memba wa ZE COMMEDY ningeenda kuongea na mropokaji Makamba awapatie Ze Commedy tenda ya kuzunguka nao, maana hao vijana wako juu. Lakini nina uhakika kwamba wananchi wangeangalia Ze Commedy na wasingesikiliza hotuba za Makamba na hao Mamluki!
 
Onyo kwa Ze Commedy mkijiunga kufanya kampeni za kusafisha mafisadi mjue umaarufu wenu ndiyo mwisho. Tunawaangalia tu na kwa sababu huwa mnafikisha ujumbe ambao watu huwa hawathubutu kuufanya
 
Mnategemea nini kutoka kwa Mgosi Makamba (kama Mtendaji Mkuu) ?
Wanadhani bado raia wa nchi hii wamelala kama 2005 walipowapa kula kwa ajili ya vijembe vya TOT? Maisha bora yaliyoahidiwa yamekuwa Maisha dhiki na sasa wamewekwa wazi anayewala ni nani.
Tusubiri tuone,watu watacheza achimenengule kisha Akina Tambwe wakianza longolongo watuwanazomea na kuondoka. Wamemchachafya EL itakuwa hao wachumia tumbo.Afterall,tuhuma zilipaswa kujibiwa na maofisa wa Serikali kwa vile hoja si za kisiasa bali zinahusu mikataba na ufisadi sasa mtu kama Msabaha atatueleza nini?
 
hahahahaha,TOT tena,mie nilifikiri watawatumia vijana wa bongo flavour?hahah,huhuuhuhuhu,kwikwikwikwi,TOT hilo funiko chafu,watanzania wamewashtukia,mtabakia kuabika,yaani watu wapo serious na issue,nyie mnaleta mambo ya kitoto?
 
Bro, Jay4
Hawawezi kuwatumia Bongo Flava. Umesikia message ya Juma Nature katika ule wimbo Kura Yako? Hawa vijana watawatoa aibu.
 
Bro, Jay4
Hawawezi kuwatumia Bongo Flava. Umesikia message ya Juma Nature katika ule wimbo Kura Yako? Hawa vijana watawatoa aibu.

Bwana Jasusi,najua hawana uwezo wa kushawishi damu mpya,ndo
maana wanakimbilia kwa akina Muumini,damn,aibu tupu.
 
Back
Top Bottom