TOP TEN ya wasiohitajika kwenye Baraza jipya la mawaziri...

Hawa ndo wanahitajika. Omary nundu,anna tibaijuka,harrison mwakyembe,samuel sitta,
 
Jamani naona mawaziri wengine tunawazulia tu, kwani Prof. Maghembe kweli kafanya nini! Mbona kateuliwa katika wizara ambayo ana ujuzi nayo - hata wabunge waliwahi kusema kwamba wizara aliyopewa Prof. Maghembe ina madudu chungu mzima kwa hiyo itamchukua muda kuweka mambo sawa, leo hii watu wana mgehuka na kuanza kumshumu na kumzulia mambo ambaye yeye binafsi ahusiki nayo - kwa nini wasiwakabe koo viogozi watendaji wa wizara yenyewe ambao wamekaa pale kwa muda mrefu na kuifanya wizara kama mali yao binafsi, si hilo tu hata mawaziri walio mtangulia walifanya kitu gani cha kujivunia cha kuiwezesha nchi hii kupiga hatua katika mambo ya kilimo?

Wizara anawachia baadhi ya Crop Boards zinaendeshwa kama mali ya UKOO na hakuna anaye wakemea au kuwafatilia, si hilo hata baadhi ya ma-Board chairman wako butu tu - wanakaa kimya hata wakiona mambo yanakwenda ndio sivyo, wanasahau kwamba waliteuliwa na Raisi kusimamamia mashirika hayo, lakini awajali chochote wanaendeshwa puta na wakurugezi wakuu wasiyo na uzalendo wowote au uaminifu kwa Taifa lao lililo wasomesha BURE.
 
majina mengi hapo juu yanatia kichefuchefu,heb.tazama haya, malima,ngeleja,maige,mfutaninisijui...ah.temea pemben
 
Yule aliyeuza TWIGA anaitwa nani?

Yaaani typical wabongo wht is in twiga wewe?twiga wawili wana thamani sawa na madini yanayochimbwa kwenye migodi inayomilikiwa na wawekezaji?siasa ni ugonjwa mbaya kwenye maswala ya maslahi ya kitaifa
 
1.Wiliam ngeleja
2.George mkuchika
3.Ezekiel Maige
4.steven Wasira
5.Halji mponda
6.crilly chami
7.Omary nundu
8.Mustapha mkulo
9.prof Jumanne Maghembe
10.Mary nagu
ziada waweza kuongeza wengine
11.
12.

Mkuu unashida ya R na L?tafuta kitabu kinaitwa soma kwa hatua cha daasa la pili kazana kwe ra re ri ro ru.
 
1.Wiliam ngeleja
2.George mkuchika
3.Ezekiel Maige
4.steven Wasira
5.Halji mponda
6.crilly chami
7.Omary nundu
8.Mustapha mkulo
9.prof Jumanne Maghembe
10.Mary nagu
ziada waweza kuongeza wengine
11.
12.



Ni vyema sana kama uki argue hii kesi vyema. Maana suala si kutaja tu majina, bali pia sababu za kuhalalisha majina hayo yasihusike katika hiyo recycling ya faces za 'watu' wale wale wa chama kile kile, kwa ajili ya kufanya yale yale, kwa namna nyingine tu au vile vile ikibidi.
 
Dizain baba yake Riz alimwekaga huyu kawambwa pale kwenye kile kiti baada ya tuhuma zisizohisha za upande fulani wa kiimani kuwa baadhi ya wanafunzi walioko upande huo wa kiimani kuwa wanafelishwa makusudi na kuwa wanapewa nafasi finyu katika baadhi ya field nyeti za kusomea mf:udaktari na kadhalika na huyu jamaa tangu apate nafasi hiyo mambo ndiyo yamezidi kuwa mabaya kuliko ilivyotegemewa!

Wadau wanasema ilifika mda mpaka baba riiiiiz akamwambia brother shukuru vipi bwana tuseme hujui mimi nimekuweka hapo kwa misingi ipi....asa watu walipo baki hoi ni pale jamaa aliposhindwa kumshuhulikia mfanyakazi wake aliyesimamisha wanafunzi kadhaa wenye hoja zenye mashiko wasifanye mitihani yao ya mwisho ya kadato cha sita!
 
[h=2][/h] [h=3]KAMATI KUU YA CCM YAAFIKI KUVUNJWA KWA BARAZA LA MAWAZIRI[/h]
Rais amepokea taarifa na maazimio ya Kamati ya wabunge wa CCM na Kamati ya uongozi ya wabunge wa CCM juu ya kilichotokea kwenye bunge lililopita mjini Dodoma.
Taarifa hizo zimewasilishwa kwenye kamati kuu na kujadiliwa. Pamoja na taarifa hizo kamati Kuu imepokea taarifa ya jinsi Rais alivyojipanga kuchukua hatua za kuwawajibisha mawaziri na watendaji wa serikali na wale wa mashirika ya umma waliobainika kuhusika na ubadhirifu ulioinishwa na taarifa ya Mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za Serikali, Kamati za kudumu za bunge na wabunge bungeni.

Kamati Kuu imeamua yafuatayo; 1. Kamati Kuu inatambua na kuheshimu haki na wajibu wa wabunge kujadili utendaji wa serikali yao.Inapongeza juhudi za serikali kuhakikisha kuwa ripoti ya mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali inajadiliwa kwa uwazi na hivyo kuibua mapungufu yaliyojadiliwa.
2. Kamati Kuu imeridhika na imebariki uamuzi wa Rais KULISUKA UPYA BARAZA LA MAWAZIRI na taasisi zingine zilizoanishwa katika ripoti hizo. Imesisitiza utekelezaji wa uamuzi huo ufanywe mapema iwezekanavyo.
Aidha kamati Kuu imeipongeza Kamati Teule ya baraza la wawakilishi Zanzibar iliyoundwa kuchunguza utendaji katika sekta mbalimbali kwenye serikali ya mapinduzi Zanzibar kwa taarifa yao.
Kamati Kuu inawapongeza wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa jinsi walivyojadili taarifa hiyo na pia Kamati Kuu inaipongeza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kuipokea taarifa na kuanza kuifanyia kazi.
 
1.Wiliam ngeleja
2.George mkuchika
3.Ezekiel Maige
4.steven Wasira
5.Halji mponda
6.crilly chami
7.Omary nundu
8.Mustapha mkulo
9.prof Jumanne Maghembe
10.Mary nagu
ziada waweza kuongeza wengine
11.
12.

Na mwenyekiti wao (I mean mwenyekiti wa baraza la mawaziri) kikwete.
 
Back
Top Bottom